Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Serikali tukufu ya awamu ya 5 ni Serikali ambayo haikosei ndo mana haitaki kukosolewa, ndo mana haihitaji vyama vya UPINZANI wala chombo chochote kinachoikosoa maana yenyew haikosei na inawaridhisha wananchi na watumishi wake hivyo kwa UTUKUFU wake huna haja ya kuikosoa.

# Mungu Ibariki Tanzania mana ipo katika kipindi kigumu cha MOVEMENT kama za Luddism na Chartisim #
 
Niweke wazi kwamba mimi nilikuwa na imani kubwa sana na kiongozi wangu ila ghafla nimepoteza imani naye mpaka sasa sijanufaika chochote biashara hakuna wateja, wanafunzi vyuoni hawajapewa pesa zao za field, wafanyakazi hawajapewa Increments zao, ajira hatoi vijana wamepigika sasa Dr Magufuli nijivunie nini kwa uongozi wako bora baba riz mkopo ulipatikana kwa wakati biashara zilikuwa zinatoka mzeee fanya hima mambo yanyoke.....
 
Na bado hali inaweza kua ngumu sana, kwa kukosa wawekezaji. Huwezi ukaingia kufanya uwekezaji mkubwa katika nchi ambayo viongozi wake wa juu kabisa hujui kesho watalipuka nini, Mara waseme from now onward elimu ni bure kwa watoto wetu huku akifanya maamuzi ndani ya kipindi ambacho hana budgeti na anataka utekelezaji uanze mara moja, Hujakaa vizuri anaibuka ana amuru bei ya bidhaa flani ishushwe haraka sana bila kufanya uchambuzi wa kina wa taarifa za Demand and Supply alizopewa, ukiwa unamshangaa kwa hilo unasikia anahamisha makao makuu ya nchi bila mkakati wowote wa kibajeti.
 
Pole sana mkuu, ndiyo kwanza hata mwaka bado hajatimiza[emoji4]
 
nyie si ndo mlikuwa mnaruka mdundiko kwenye kampeni zake?

sasa mnalia nini..?

hakika sijutii kura yangu kumpa Lowasa
 
Mshauri wake mkuu ni Kagame mtu mwenye inch yenye watu 8m, mtu mwenye inch ndogo kuliko mkoa wa Pwani. Mtu alie ingia madarakan kwa mtutu!!! Magufu anajiandaa na Uchaguzi
 
Niweke wazi kwamba mimi nilikuwa na imani kubwa sana na kiongozi wangu ila ghafla nimepoteza imani naye mpaka sasa sijanufaika chochote biashara hakuna wateja, wanafunzi vyuoni hawajapewa pesa zao za field, wafanyakazi hawajapewa Increments zao, ajira hatoi vijana wamepigika sasa Dr Magufuli nijivunie nini kwa uongozi wako bora baba riz mkopo ulipatikana kwa wakati biashara zilikuwa zinatoka mzeee fanya hima mambo yanyoke.....

Mbona alivyokuingia haukutuambia?
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Pola yako ulidhani hutafikiwa na mkono wa ukombozi. Wengi ndio anazidi kukita mioyoni mwetu!
 
Anatupeleka Chato!
 
Kwa siku za karibuni nimekuwa nikiangalia mno hotuba na mikasa ya Idi Amini alipokuwa akiitawala Uganda kidikteta...hakika niseme wazi, anafanana kwa kila kitu na Magufuli, tofauti yao huyu bado hajaanza 'kupoteza' watu, lakini alishaahidi hilo wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM wacha tusubiri tuone!
 
Kuna watu walisema tutaikumbuka msoga wengine maswali sanaa wengine eti labda kwa safari nyingi!!
Ila saa hiz kila mtu ana majibu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom