Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kuhusu kupambana na ufisadi kwa vitendo, hilo anastahili pongezi.
Kuhusu kuzuia kutoa maoni au kupata habari, au demokrasia kwa ujumla hilo ni vema likaangaliwa kwa usahihi wake
 
Hahaa you looks empty minded kama huelewi kuhamia Dodoma kunamhusu vipi mlipakodi basi dikteta Kazi anayo
WATANZANIA HANGAIKENI NA MAENDELEO YA FAMILIA ZENU SIASA, KUHAMIA DODOMA WEWE VINAKUHUSU NINI?
 
kwenye maslah ya nchi hakuna ccm wala chadema nashangaa watu wanakurupuka kuwadharau viongoz wa chadema huku wengine wakiwaponda wa ccm jaman kuwen serious kujipendekeza sio dili naamin kabisa mnajua waz kuwa kwa sasa nchi inaongozwa kwa kumfurahisha mtu mmoja tu yaan kila kiongoz anajitahd kufanya kila awezalo kumfurahisha kaka mkuu haijalishi anavunja sheria au la ilimrad kesho aongezewe madaraka lkn kwa wananchi tusubir sana
 
INA MATATIZO YAFATAYO.

KUSITISHA AJIRA
KUVUNJA DEMOKRASIA
KUNYANYASA WATUMISHI WA UMMA KUTOWAPA STAHIKI ZAO ZA MSINGI
WAKULIMA KUKOSWA MASOKO
MIGOGORO YA ARDHI KILA KONA
MAISHA YA WATANZANIA KUWA MAGUMU
SERIKALI KUTOFAUTIANA KWENYE MATAMSHI HASA VIONGOZI WA SERIKALI
SERIKALI IKISHINDWA KITU INAKAA KIMYA MFANO BEI YA SUKARI NK

MWISHO RAIS KARIBU MKOA WETU WA KILIMANJARO LAKINI NJOO NA HOJA ZA MAENDELEO SIYO KUPONDA WAPINZANI JUKWAANI MAANA HATUNA FAIDA NA MANENO HAYO TUNATAKA MAENDELEO
 
  1. MAHAKAMA YA MAFISADI.
  2. WATANZANIA WA KAWAIDA WANA FURAHA.
  3. SHISHA MARUFUKU.
  4. MAFISADI WANABUGIA VIDONGE VYA PRESHA KAMA KARANGA.
  5. NDEGE MBILI MPYA.
 
Kuhakikisha wagonjwa hawalali chini
Kuhakikisha wanafunzi hawakai chini
Kuhakikisha mafisadi wanalipa kodi
Kutumbua majipu (kama mletamada)
Kuhakikisha wanafunzi wanasoma bure hadi kidato cha 4
Etc
 
Habarini Wadau,

Nimeamua kushare na ninyi maajabu ninayotafakari na maswali ninayojiuliza mara kwa mara na nashindwa kujua hatma ya Baba yangu na ya nyumbani kwetu kama familia.

- Baba mkali, Dikteta na Fashisti ila hawezi kukubali hilo kirahisi ila wanawe tunaona kila dalili za sifa hizo.

-Mtu mzima lakini Hashauriki asilani.

Geniouses na Watu maarufu wenye uzoefu wa kutunza familia na uelewa mkubwa ulimwenguni wanashaurika namshangaa huyu mzee hapa home.

- Anapenda sifa huyo...ukitaka atoe matamko mpaka ikifika usiku aote anatoa matamko basi msifie tu.

-Hajui kiingereza...teh teh teh, hapa ndipo baba anaponishangazaga sana...yaani yeye ananisisitiza kujua kuzungumza kiingerezea fasaha ili niweze kuwasiliana na walimwengu na kupata uelewa mpana, kujifunza kwa wengine na kukaribisha maendeleo nyumbani kwangu Lakini YEYE HAJUI na napata aibu awasilianapo na wageni...aibu nakuwa naipata mimi.

Hivi si ni maajabu haya?

Walllah, Natamani ningeweza kumbadilisha huyu baba nipate mwingine.

Nimshaurije huyu baba na namheshimu sana isiwe namchochea tu kwenu.
 
Tutakimbilia kwa baba halisi yaan biological,huyu ni wakufikia ndiyo maana hafanani na sisi na wala hatujali na utu wa familia yetu yeye hana,ndiyo maana anataka tuishi kama mashetani
 
Si useme tu unamzungumzia mtu fulani ngosha wa pande za ziwa ambaye siku hizi amehamia kwenye nyumba nyuepe iliyoko karibu na wakaanga samaki wa pale fee
 
Walimu waliokuwa wameajiriwa Udom kuendesha program ya walimu 8000

Watu wa clearing and forwarding pale bandarini waliokuwawakishusha sukari na watu wa malori waliokuwa wakisafirisha sukari kwenda mikoani!!

Ajira za kutembeza watalii hazipo tena baada ya watalii kupunguza na madereva wa malori ya tour and travel zimepungua!!

Wafanyakazi wa vitengo vya VIP vya serikali ndani ya ndege za kwenda nje wamepunguzwa kazi maana hakuna wateja tena waziri anayesafiri ni mmoja tu waziri wa mambo ya nje!!

Ajira za machinga Mwanza na Dar zipo mashakani baada ya kutimuliwa town!!

Wakati huo yeye ajatengeneza ajira hata moja zaidi ya Mawaziri,wakuu wa mikoa,wilaya,Makatibu tawala wa mikoa na wilaya!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom