Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Huyu Rais sijui alifikaje hapo.. In short tumelamba galasa.. Nchi inaweza kuingia kwenye machafuko.. No vision ni mwendo wa visasi.. Rais ambaye ana kibri, anayefurahia wengine wakiumia.. Hata wale wanaomshangilia soon wataanza kupigika na wataanza kuumia pia. Lets stay and watch.
 
Kwa mwendu huu anao enda Hata nikijaribu kujipa matumaini nashndwa
Huyu mkubwa ata feli sana labda abadilike hapo baadaye
 
Kiukweli kwa mujibu Wa ratiba za Mbinguni JPM ndiye alyekusudiwa kuwa raid kwa wakati huu,,,,, sasa hayo mengne ni washauri wake ndo wanashindwa kutumia nafasi zao.
By Pastor Illovo
 
Tukutane hukohuko baada ya miaka mitano kama Mungu atatufikisha. Ila asipobadilika!! Eiiiiiiii!
 
Bora useme wewe. Wengine tulisema kitambo tukapuuzwa.
 
Bei za Bidhaa zitapaa.
Tutaanza kupanga mistari kununua bidhaa zitokazo nje .
 
TCRA is following
 
Tanzania kuwa maskini zaidi, kukimbiwa na wawwkezaji, ccm kugawanyika, chadema lupango wote, maandamano kila kona yakianzia Zanzibar, jeshi na police kuongoza nchi
 
TUTAZIPIKU MAREKANI NA CHINA...NA TANZANIA ITAKUWA NAMBA 1 KTK UCHUMI MKUBWA DUNIANI...

OVA
 
Baada ya miaka 5 Tz bilashaka ni uchaguzi ma raisi au?
hapana 2021 miaka mitano ijayo utakuta ni kipindi cha pili cha Rais Magufuli
naona Upinzani utakuwa umekuja wa sira mpya
hivi vyama vyenye fujo atakuwa keshavisambaratisha
vitakuwepo km Green party, Republic, Islamic, Chriss Democratic
 
Reactions: iw8
Baada ya miaka 5
Tanzania itakua ya viwanda

Magufuli atashinda kwa kasi

Wapinzani tutaelewa nini magu anataka
 
najiuliza tu,
1. anatangaza watu wasipopenda kupitisha mizigo bandari ya dsm, wakwende zao

2. watalii wasiolipa waende zao bora tuwakose tu

3. natetea wananchi masikini, lakini mtaani masikini maisha ni magumu kuliko wale wanaotumbuliwa

4. makusanyo ya kodi ni yaleyale

5. mizigo bandarini imepungua, hakuna mapato.

6. sitaki maandamano, hapa kazi tu.

7. mahotel yanafunga mengine yanabadilishwa kuwa hostel(mt.meru arusha)

8. hakuna kupandisha mishahara ya wafanyakazi pamoja na kuahidiwa meimosi kupunguziwa kodi, hakuna safari, bajeti yote imeelekezwa kwingineee, kwa wafanyakazi masikini hakuna bajeti ya kutosha wanalala njaa. wafanyakazi wa umma sio masikini labda.

swali ninalojiuliza, kwani, kukusanya kodi kunakohitajika ni kule toka kwa watalii tu au kwenye migahawa na hotel watakazolala wakifika hapa. hivi hotel nazo wanatoka nazo kwao, si za watz hivyo hela itakuwa inaingia mifukoni mwa watz na hotel, safari companies etc zimeajiri watz, kufa kwa utalii ni kuua ajira za watu rundo kuanzia madereva wa magari ya utalii, petrol station wanakojaza mafuta, wafanyakazi mahotelini, wauza vyakula mahotelini n.k. hicho wanachotarajia kutoa watalii ni kikubwa kuliko kile wanachospend kwa watz wakishafika hapa?

ofisi za serikali, watu wote wanatamani uongozi wa kikwete ufike, na kila mtu anaomba Mungu 2020 ifike haraka.

hakuna tumaini, lini maisha au uchumi wa nchi utatengemaa. kenya uchumi unazidi kupaa, utalii unapaa despite ugaidi. hapa kwetu hatuna lugha nzuri na wafanyabiashara, tunataka tu kuwatumbua na hapohapo tunasema tunataka tz ya viwanda na tunakaribisha wawekezaji. hivi tunaelewa tunachoongea au?

utumbuaji majibu hauendi kisheria, leo mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa au waziri yeyote akiamua anakusimamisha kazi bila kukupatia nafasi ya kusikilizwa. hizo kesi wakiamua kuifungulia serikali, nani atawalipa? si kodi zetu?
 
Ndio vilio vimeanza,mkuu analeta ubishi kwenye mambo ya kiuchumi. Pesa kwenye mzunguuko imepungua,Bandarini mizigo imepungua,biashara zinafungwa na wengine wanaziuza.Ni katika kipindi hiki ndio viwanja na majumba mengi yanauzwa na pesa za kununulia hakuna,waliokopa miezi kadhaa nyuma wameshindwa kulipa mikopo wanaishiwa kufilisiwa na bado baadhi ya mali hazinunuliki hali inayopelekea wakopeshaji nao kupata pesa iliyo chini ya malengo.

Nini mh rais hafanye kuinusuru hali hii ............maana mambo ya kiuchumi yanatugusa wote,sio wanasiasa tu.
Mh rais anasema pesa zimefichwa,inawezekana hii ni kweli, hebu tumpeni ushauri mh rais nini kifanyike na ni wapi alipokosea.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…