najiuliza tu,
1. anatangaza watu wasipopenda kupitisha mizigo bandari ya dsm, wakwende zao
2. watalii wasiolipa waende zao bora tuwakose tu
3. natetea wananchi masikini, lakini mtaani masikini maisha ni magumu kuliko wale wanaotumbuliwa
4. makusanyo ya kodi ni yaleyale
5. mizigo bandarini imepungua, hakuna mapato.
6. sitaki maandamano, hapa kazi tu.
7. mahotel yanafunga mengine yanabadilishwa kuwa hostel(mt.meru arusha)
8. hakuna kupandisha mishahara ya wafanyakazi pamoja na kuahidiwa meimosi kupunguziwa kodi, hakuna safari, bajeti yote imeelekezwa kwingineee, kwa wafanyakazi masikini hakuna bajeti ya kutosha wanalala njaa. wafanyakazi wa umma sio masikini labda.
swali ninalojiuliza, kwani, kukusanya kodi kunakohitajika ni kule toka kwa watalii tu au kwenye migahawa na hotel watakazolala wakifika hapa. hivi hotel nazo wanatoka nazo kwao, si za watz hivyo hela itakuwa inaingia mifukoni mwa watz na hotel, safari companies etc zimeajiri watz, kufa kwa utalii ni kuua ajira za watu rundo kuanzia madereva wa magari ya utalii, petrol station wanakojaza mafuta, wafanyakazi mahotelini, wauza vyakula mahotelini n.k. hicho wanachotarajia kutoa watalii ni kikubwa kuliko kile wanachospend kwa watz wakishafika hapa?
ofisi za serikali, watu wote wanatamani uongozi wa kikwete ufike, na kila mtu anaomba Mungu 2020 ifike haraka.
hakuna tumaini, lini maisha au uchumi wa nchi utatengemaa. kenya uchumi unazidi kupaa, utalii unapaa despite ugaidi. hapa kwetu hatuna lugha nzuri na wafanyabiashara, tunataka tu kuwatumbua na hapohapo tunasema tunataka tz ya viwanda na tunakaribisha wawekezaji. hivi tunaelewa tunachoongea au?
utumbuaji majibu hauendi kisheria, leo mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa au waziri yeyote akiamua anakusimamisha kazi bila kukupatia nafasi ya kusikilizwa. hizo kesi wakiamua kuifungulia serikali, nani atawalipa? si kodi zetu?