Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
sasahivi tu, mataifa ya nje yanatuangalia halafu yanashangaa kwanini tulimwaga sifa zote zile. na hakika yake mzee anakazi nzito sana kuwaaminisha wananchi kumchagua tena 2020, kwasababu ujue kupata kura hakuji tu kwa kutamka maneno kwamba "mimi nipo pamoja na masikini", manake hayupo pamoja na matajiri, kumba nyuma ya matajiri na wafanyakazi kuna msururu wa masikini wanamtegemea. maisha mtaani ni magumu sana na huu ni mtaji mzuri sana kwa ACT WAZARENDO au CHADEMA 2020.
 
Watu walikuwa wanaimba Tu Kama Wimbo wa Taifa...

Sasa Wao ndo Wanaisoma Namba Vizuri..

Wako wapi wasanii waliomsupport Hata IkUlu hawajawahi Kanyaga tena..
 
Magufuri ni mbabe!! Uchumi una njia zake!! Watendaji wake wanafanya kazi kumridhisha kutokana na ubabe wake!! Raia jiandaeni na mbonyeo wa ukata!!!
Acheni kulialia nyie...Polisi wetu wapo vizuri na wamewwzeshwa ili waweze kurekebisha na kukuza hali ya Uchumi.
huwezi ukaongoza taifa kibabe kama unavyotaka
 
labda tuendelee kujipa moyo, ila maisha magumu wandugu, kwa wafanyabiashara, wafanyakazi, hata wasio na kazi. sijui itakuwa hivi hadi lini. ni kweli tumejipanga vya kueleweka kweli?
 
Atachapisha hela nyingine ili ziwe nyingi wale masikini anao wapenda wapate angalao kidogo.
 

Nimekuelewa, kumbe dola ikiwa juu export inaweza kuongezeka sababu dola kidogo kwa pesa ya ndani nyingi ambapo wafanya biashara wengi watakimbilia kufanya biashara

sasa kwanini wanauchumi wao wanapima uchumi kwa kupanda kwa thamani ya pesa wakilinganisha na dola? Na mimi ndo niliwakariri wao, ukiona tu uchumi umeyumba wanawahi kusema dola imepanda.
 
Halafu ana mgao wa umeme wa kimya kimya,maana sisi huku wa Tegeta -Bunju ni wiki 3 sasa umeme hausomeki.
 




Bandiko hili laweza kuwa ni dhihaka kwa "mtakatifu" na linapaswa kupewa kesi ya uchochezi. Mtu mwenye daraja la utakatifu au umalaika huwa hakosei na wala hashauriwi. Hakuna mwanadamu awaye yote awezaye kumshauri "mungu wetu" yeye ni alfa na omega.

Kumshauri mtakatifu mwenye heri kunaweza kuchukuliwa kuwa ni kumjaribu, kumjaribu ni kiashiria cha fyokofyoko kinachoweza kukufanya "upotee" ndani ya dk.5. Hizi ni zama za kushughulikiwa ndani ya dk. 5 hivyo ni vema kabla hujaleta jukwaani hoja yenye viashiria vya kuhoji "utukufu" wa baba mtakatifu uandike wosia ili ukipotea ndani ya dk5 familia yako isiparaganyike kwa kugombea mali ulizoziacha.
 
Acheni kulialia nyie...Polisi wetu wapo vizuri na wamewwzeshwa ili waweze kurekebisha na kukuza hali ya Uchumi.
Duh hiyo mpya nlikuwa Sijajua Kama police ndiyo wanakuza uchumi...

Ova
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…