Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Rais wetu amelewa madaraka, amesahau kuwa yeye ni Rais wa Watanzania na ni lazima atusikilize na apange kulingana na matarajio yetu. Nafikiri ni wakati muafaka sasa watanzania kuanza kuzitafakari kauli za Rais kwa kuwa zina athari kwa maisha yetu. Haiwezi kuwa sawa eti kwa kuwa alikwenda kuchukua fomu mwenyewe anaweza kufanya atakavyo. Ni lazima awe tayari kujibu hoja zinazomkabili Makonda, akumbuke yeye ndiye aliyeanzisha mchakato wa uhakiki wa vyeti na makonda ni mtumishi wetu anayelipwa kwa fedha za Watanzania. Nilitarajia nisikie Rais hatamchukulia hatua kwa kuwa tuhumu alizoelekezewa hazina ukweli wowote na siyo kuonyesha ubabe na kiburi kilichokithiri.
 
well inawezekana hatumuelewi lakin ajuwa kule anatupeleka maana anaijuwa njia vizuri hivyo kuingia kwake vichochoron ambako mimi na wewe hatujuwi njia isiwe ndio sababu yakusema hajuwi kule anatupeleka. Tumpe muda na kwa kuwa uchochoro anapita sisi hatuujuwi ila bila shaka tutafika na tusipo fika tutakuwa na nguvu kumwambia umetupoteza achia uskani
Tatizo lako hutaki kumweelewa mhe rais yeye kasema acha acha ulofaaa Fanya Kazi Kazi kazi hakuna dili wala unga wala viroba no Kazi tuuu
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Nidhamu ya watumishi.imeongezeka.! Wanafiki wanajulikana na kuumbuliwa dili zimepungua.! Wauza madawa wanatengeneza timu zao za kufitisha watu kwenye mitandao. Mange kimambi ni Mungu wa upinzani..fly over inajengwa Tazara nyingine imezinduliwa ubungo leo..treni zinasafirisha zaidi mizigo kuliko malori. Tuna ndege zetu wenyewe japo ndio tunaanza.!! Wenye mimba za ENL. Wanapata kichefu chefu na kuhangaika na madhara ya mahaba pasipo kinga..! Kwao kila move ya Magufuli inawaumiza... [HASHTAG]#tunaiona[/HASHTAG] kesho yenye matumaini zaidi#
 
Kwanza kabisa nianze kwa kupongeza serikali iliyopo madarakani.naipongeza kwa sababu
1: imeongoza na inaendelea kuongoza kwa kudhihirisha unafiki wa chama tawala kwa wanachi wake.kilichohubiriwa na kinachofanyika ni tofauti..

2: serikali inaendelea kuanika wazi UJINGA wa watanzania kuwa walichagua hovyo bila kutafakari

USHAURI KWA WAPINZANI
Kwanza kwa wale mliobahatika kusoma HISTORY kuna kanuni moja iliyokuwa ikizikuta nchi ambazo zilikuwa zinahitaji ukombozi.. Kanuni hiyo inasema hivi "IN ORDER TO HAVE A REAL REVOLUTION THERE SHOULD BE COMMON PROBLEMS TO ALL "
Wapinzani , huu mwendo wa mheshimiwa mtukufu umeanza kuwatisha na wale wenzake waliokula na kunywa pamoja .wameanza kugundua kuwa yule siyo type yao..

Sasa ni wakati wa upinzani kunyamaza kimya. Kimya hiki kiwe cha mikakati Sana. Lakini kimya hiki kilenge kuwaacha wenzetu waonje joto la jiwe vizuri..hii iatatufikisha kwenye ile kanuni ya MAPINDUZI YA KWELI.

wakati wapinzani mnawaeleza ukweli watanzania hawakuwaelewa sasa muwaache kwa muda waonje joto ili miaka ijayo tuvute kamba kwa pamoja..
Kwangu mm naomba kila uchwao mheshimiwa akaze ili wale wengi wasiolewa waelewe...

UHAKIKI WA VYETI UNAENDELEA!!!!!!
 
Wakati wa uchaguzi walituaminisha kuwa mgombea wao ana ujasiri wa kupambana na ufissdi kuliko yule wa Ukawa.
Mara tukaambiwa ataunda mahakama ya ufisadi huku akipiga push ups jukwaani.
Leo ndio amtetee mtuhumiwa wa vyeti eti akisema ni maneno ya mitandao?
Bado kuna wanaomkubali kwa kupambana na ufisadi?
 
  • Thanks
Reactions: MTK

Hakuna kitu kama hicho,jamaa yeye mwenyewe ni wale wale.Hakuna cha Rushwa,wala ufisadi ni mwendo wa kula tu.

Jiulize tuhuma zote with facts na evidence bado unamtetea mtuhumiwa,lazima tujiulize uka kwa ajili ya Taifa au tumbo??Ngoja tusubiri wenye chama chao.
 
Mtaani pesa ngumu, umefukuza watu maelfu kwenye ajira zao, wahitimu vyuo vikuu hutaki kuwaajiri na hauna mpango huo sababu kama kiongozi hufuatilii tena maendeleo ya nchi yako, wewe upo bize kufuatilia nani kasema nini, imekuwaje (Shilawadu) na wasomi wengine unawapeleka wakafanye kazi nchi jirani (Kenya) wakati hapa kwetu penyewe wanahitajika na hawatoshelezi mahitaji!! @Unakwepa kuajiri?.

My dear President:
Ni kichaa pekeyake anayeweza kuwaambia watanzania hawa waliojazana mitaani kwa kukosa ajira kwamba wafanye kazi waachane na mambo ya mitandaoni unayoyaita Umbea, fursa ziko wapi?.

Wewe unakula na kunywa bure.... Ukitaka kuamini haya kabidhi kiti uje mtaani..... Kuzaa si kazi bwana Sizonje, kazi kulea.

Forgo #Jf
 
Mpendwa Rais Dr shain. Naomba sana hebu weka mashine ya ukaguzi bandari ya Zanzibar kwa abiria wanaotoka DaresSalaam au wanaokwenda DaresSalaam. Inatia aibu unafungua begi wale maaskari wanaangalia mpaka machupi machafu alafu hawajavaa hata groves hii wanahatarisha Afya zao alafu pia Zanzibar ni tourism attraction unapokea mataifa mengi sana basi naomba ufunge hizo mashine.
Nimeongea na mmoja wa Askari amesema wamesema weee lakini hawasikilizwi wanaomba nasi tuwasemeee.
Hii inatushushia hadhi
Kwanza hata upekuzi wenyewe sio mzuri huwezi ona chochote wanachokikusudia kwa upekuzi ule uliopo bandarini.
Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Zanzibar
Mungu akubariki Dr again Rais wa Zanzibar
Ahsante kwa kuchukua hoja hii na kuifanyia kazi kwa haraka na kwa unyeti wa jambo hili.
 
majibu yake mkafanye kazi
serikali haina mashamba
mlikuwa wapiga dili kheee

hahaha kazi gani wakati maelfu kashawasababishia wako mitaani?
 
Mpendwa Rais Dr shain. Naomba sana hebu weka mashine ya ukaguzi bandari ya Zanzibar kwa abiria wanaotoka DaresSalaam au wanaokwenda DaresSalaam. Inatia aibu unafungua begi wale maaskari wanaangalia mpaka machupi machafu alafu hawajavaa hata groves hii wanahatarisha Afya zao alafu pia Zanzibar ni tourism attraction unapokea mataifa mengi sana basi naomba ufunge hizo mashine.
Nimeongea na mmoja wa Askari amesema wamesema weee lakini hawasikilizwi wanaomba nasi tuwasemeee.
Hii inatushushia hadhi
Kwanza hata upekuzi wenyewe sio mzuri huwezi ona chochote wanachokikusudia kwa upekuzi ule uliopo bandarini.
Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Zanzibar
Mungu akubariki Dr again Rais wa Zanzibar
Ahsante kwa kuchukua hoja hii na kuifanyia kazi kwa haraka na kwa unyeti wa jambo hili.

Hapa cjakuelew!!hizi ni stress au nn
 
Hali ngumu kweli leo kwenye biashara yangu nimepata 200/= (Two hundred only) [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kina kitu ambacho sikielewi kabisa kabisa. Magufuli anafanya mambo mengi kinyume na matakwa ya waliomchagua- yaani wananchi. Hivi huyu baba, kichwani mwake anawaza kwamba anawajibika kwa Yupi? Hivi ni vigumu kwake kuelewa kuwa alichaguliwa kwa kura za wananchi na hivyo anatakiwa kuwajibika kwao?

Kuchukua fomu za kugombea ni utaratibu wa kumfanya mgombea apigiwe kura na wananchi ili akipata madaraka awajibike kwao. Kwani kuna mtu anafikiri kuwa anawajibika kwa Mungu au kwa shetani. Mtu huwezi kuwajibika kwa Mungu au shetani maana hawapigi kura. Ni lazima Magufuli atambue kuwa cheo ni dhamana asipojishusha na kuwajibika kwao wananchi waliomchagua watatumia njia za kikatiba kumwondoa madarakani. Kama Magufuli ana masikio na asikie, vinginevyo patachimbika, itakuwa ni mtanange kati yake na waliompatia madaraka- wananchi na anajua wazi mshindi atakuwa ni nani.
 
Yeyote anayempinga na kumshauri Bw.Magufuli basi huyo hapendi maendeleo, na atakuwa ni mwanachadema tu(In magufulis voice)
 
Yeyote anayempinga na kumshauri Bw.Magufuli basi huyo hapendi maendeleo, na atakuwa ni mwanachadema tu(In magufulis voice)
MUSSA, nadhani ni sababu ya personality ya huyu Bwana. Huyu mtu ni wa ajabu kama alivyosema TL. Huwezi kuwapuuza watu waliokupia kura kukuweka madarakani, hii haihitaji ushauri.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom