Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Ukiona Baba akiulizwa swali anakuwa mkali ujue hana jibu,
Hajui akujibu nini,
Hajui anakifanya kitamfukisha wapi,
Amepoteza mwelekeo anatafuta pa kutokea.
CCM sasa hivi Polisi ndio kimbilio lao,

Mwananchi akihoji kitu Jela,
Mwaandishi wa Habari akiandika kitu kuhusu Serikali Jela,
Vyama vya Siasa haviruhusiwi kufanya Siasa, Vikifanya Jela,
Na tena hii ni mbaya maana CCM wao kila siku wanafanya mikutano ya Kisiasa kupia Raisi, wakuu wa mikoa, Wakuu wa Wilaya, kiujumla CCM inafanya Siasa pekeyake kwa kutumia nguvu.

Ukiishiwa Sera ndio nguvu hutumika, CCM nguvu huwa zinazidiana kuweni makini.
mie wameniacha hoi hata hao wapinzani kutembelea majimbo yao napo kosa, hawataki, sasa sisi wananchi tumewachagua wao wameteuliwa na mtu 1, tunataka tupeleke kilio chetu kwa wabunge wetu tuliowachagua na sio walioteuliwa ili waweze kufikisha malalamiko yetu mbele, napo hawataki, mie naona wanahisi wananchi tumelala, tupo macho tunajua kila kitu kinachoendelea
 
Naona wanachonga wenyewe kinyago ambacho baadae kitakuja kuwatisha, na hakika watakikimbia
 
Mtoa Mada hii nimeipenda maana umeelezea jinsi mambo yanayotokea ndani ya nchi yetu,na hii ni hatari mno for the next generations,hawa wanasiasa wetu kwa uelewa wao au lau wanatutengenezea kizazi cha watu watakaokuwa na hasira na watakaoamini kuwa ufumbuzi wa kila kitu ni kutumia nguvu,vitisho;mama au baba unatakiwa uilee familia yako kwa upendo,show to your childrens how u love them,how to respect,na mwishowe tutapata taifa lenye upendo.few kms beyond our borders haya yanatokea because walilelewa na kuwa treated hivyo kuwa to sort out the problems its only violences;angalia maandamano yao,tumeshuhudia watu wakichomwa moto alive reason behind sio wazawa wa nchi hiyo;kumbuka our father of the national alihubiri upendo ,na upendo huo tukawa nao ndio maana wageni wetu tuliwaheshimu mno na kuishi nao vizuri;kitendo alichokifanya LILIAN DUBE,ukikifanya kwenye nchi aliyotoka uatakuwa umeshajihukumu death penalty.please my leaders tujenge nchi yenye upendo na kuthamini utu na haki za binadamu.
 
Haswaaaaaaaa, nguvu tumia, lakini ikifika muda unaemtesa kuchoka na yeye atatumia nguvu,
wewe sio mungu tuseme utajua nani anataka kutumia nguvu kabla ya nguvu kutumika, utakuja kujua tayari keshaleta madhara.
 
Mlio karibu na Rais Magufuli mwambieni serikali yake imeajiri watu wasiozidi laki tano (500,000) kati ya walipa kodi milioni 50 (50,000,000). Sawa na mtu mmoja kati ya mia moja.
Awe na heshima kwa sekta binafsi.
jamaa hawezi kukusikia kwani anashindilia na kubughia ugali wa bure . Shibe ina nyodo nyinyi
 
Sitaki kuamini kwamba hata humu ndani kuna vihio kiasi cha kushindwa kuelewa simple logic ya lema juu ya uzalendo wa My Magufuli. Au niamini kwamba hizi zinazoendelea Ni propaganda za CCM walijitia ujuha kwamba katika hotuba yake alimsifu Magufuli.

Hebu jamani jaribuni kuangalia philosophy iliyotumiwa na Lema, lema amejua kabisa mkuu ukitaka uende naye usimkosoe. Hebu jibuni wataalamu wa maswala ya philosophia; ana maamisha nini mtu anayesema Nataka kuamini?

Wote mkishindwa ntajibu mwenyewe..ila humu najua wapo wenye bongo kubwa
 
Ni ukweli usiopingika kuwa vita au mgogoro ndani ya nchi haukuwahi kuanzishwa na vyama vya upinzani bali serikali ya chama kinachokuwa madarakani.

Migogoro hiyo huibuka pale chama kilichopo madarakani kinapotaka kufunga midomo vyama vingine, kuvizuia kuendesha siasa zao za ndani au za kukutana na wafuasi wao au ukabila uliopitiliza ndani ya nchi

Vitu hivi nilivyovitaja hapa Tanzania vimeanza kushika kasi kiasi kwamba hatuitani tena watanzania bali kuitana kwa kutumia kabila la mtu, chuki za kisiasa baina ya chama na chama, uhasama baina ya chama kinachotawala na upinzani wa kweli kutoka vyama vingine, uhuru wa kuongea unapotea siku hadi siku manyanyaso yasiyo na kichwa wala miguu kutoka kwa chama kilichopo madarakani kwa vyama vya upinzani wa kweli.

Manyanyaso hayo yameonekana dhahiri kwa miaka 10 sasa na sio jambo la kushangaza kusikia vyombo vya dola kama police,mgambo,jwtz na vingine vikitumwa kwenda kuvikomesha vyama vya upinzani popote vinapotaka kufanya shuhuli zaoza kisiasa.

Utamsikia rais wa nchi akionyesha chuki hadharani dhidi ya upinzani
Bunge nalo likionyesha chuki hadharani dhidi ya upinzani
Mambo haya sio ya bahati mbaya ni mambo yaliyopangwa namna ya kuusambaratisha upinzani
Lakini mwisho wake ni nini?

Ni kuibuka vita visivyoisha ndani ya nchi vya wenyewe kwa wenyewe pale uvumilivu wa mambo haya utakapofika kikomo

Tanzania hatuna na amani japo wengine hulazimisha bali tuna utulivu tu ambao ipo siku utatoweka kama mambo haya hayataangaliwa
Watu wanajenga visasi na siku vikikomaa tutakuja kutafutana na kutafuta wa kumlaumu tumkose

Uhuru na umoja ndio nembo ya taifa letu lakini sasa havipo tena huu ni mwaka wa kumi sasa toka vitoweke

Yangu macho

Na Edeni kimario
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom