Anayekubali kushindwa hakika ni mshindani

Anayekubali kushindwa hakika ni mshindani

Elpaul

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2018
Posts
922
Reaction score
692
Poleni na weekiendi mashabiki wa kandanda popote mlipo ndani na nje ya Tanzania, Hii ni moja ya Jumapili iliyokuwa inasubiliwa kwa hamu kutokana na mechi iliyokuwa inawakutanisha miamba ya soka nchini Simba na Yanga.

Kwa kawaida mechi hii huvuta hisia za mashabiki wa kandanda kote nchini, Tambo za hapa na pale kutoka pande zote mbili na wengine hudiriki kuweka dhamana vitu vyao vya thamani, kutokana na mtazamo wa muhusika, Mechi ya leo ilikuwa mojawapo ya Mechi iliyofuatiliwa na mashabiki wengi Barani Africa, hasa kutokana na kiongozi wa ngazi za juu kabisa barani Africa kwenye soka kuwepo uwanjani.

Mbali na rais wa caf kuwepo uwanjani lakini pia Dr. John Pombe Joseph Magufuli alikuwa uwanjani kushuhudia mtanange huo, Unaweza kuona kwa jinsi gani mchezo huu ulivyokuwa na uzito kwa namna moja au nyingine, Kilichonifanya kuleta uzi huu Kuna mwanachama mmoja alikuja na utabiri kwamba Simba angeshinda kwa kishindo lakini matokeo yakatoka kinyume chake.

Ni moja Kati ya matokeo ambayo wengi hawakuyatarajia kutokana na klabu ya Simba kuwa katika kiwango bora msimu huu, Lakini ndio hivyo mnyama alivutwa mkia, Nashindwa kuamini Kama Simba alipokwa ushindi na very powerful people ama la.

Mimi Kama shabiki wa mpira nasema Simba Kama mashujaa tukubali kushindwa ili ushindani wetu udhihihirike Ahsanteni.
 
"Eti kiwango bora"

Mlishaambiwa msiingie na matokeo uwanjani.

Yanga ya Dar es salaam bingwa wa kihistoria aendeleza ubabe kwa wanyonge wao Mikia fc.
 
Back
Top Bottom