Anayemjua Refa Kayoko amsomee hii

Anayemjua Refa Kayoko amsomee hii

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Posts
20,649
Reaction score
4,786
Hakuna refa profesional anaefoka hivi uwanjan, ni mpuuzi anayelazimisha kutisha ili aogopewe, ndiyo anaweza fanya hivi.

Refa siyo adui wa mchezaji ni rafiki mkubwa wa mchezaji, ukimuiga Corina kutumbua mijicho hivyo haimaanishi kuwa wewe utakuwa Corina, lakini ukumbuke Corina vile ndivyo alivyo.

Mwenye namba ya huyu lofa amwambie marefa wenye akili Duniani wanacheka na wachezaji uwanjani kwa maana pale ni ofisini kwao na wale ni waajiriwa wenzie. Ukiona mfanyakazi anamfokea mfanyakazi mwenzie kazini namna hii, basi huyo anatafuta kiki na kujikomba kwa mabosi.

Halafu ajifunze kutoa maamuzi ya ushindi kwenye mechi zenye mvuto kama zile na siyo kusawazisha mchezo kwa kumwaga mikadi ili ipatikane suluhu na yeye ajivue lawama toka kila pande.

FFFE411F-2B36-4DFE-B1E3-C1DD30F6995A.jpeg
AACA9D57-C517-40BC-88C9-302C45278334.jpeg
CA444853-1B3B-4919-8A89-0BE61B529120.jpeg
2D1A5CAD-AA67-4262-8DB7-93D324064515.jpeg
 
Unless una shida personal tu, kadi zimetolewa kutoka na makosa yanayohitaji kadi ya njano kuoneshwa.

Kutoa macho tu unaogopa mtoa mada. To me kayoko amejitahidi sana. Dawa ya wachezaji wajinga ni kadi tu ili mpira uchezwe vizuri.
 
Ni refa mzuri akiacha utoto wa kujadiliana na wachezaji na kupiga story hovyo kila akitoa maamuzi. Mtaani atakuwa muongeaji sana huyu, akibadilisha hilo ni refa mzuri tu. Hiyo ya kuwa mkali na kutoa kadi nyingi ni style yake, kuna marefa huvumilia madhambi na wengine huwa strict. Apunguze kidogo kuna kadi mbili sikuona kama zilikuwa lazima
 
Ungejikita zaidi kwenye kuonyesha makosa ya kimaamuzi aliyoyafanya suala la ukali, kumgeza collina, kufoka n.k iyo na hulka au mbwembwe tu za mhusika as long as katekeleza majukumu yake ipasavyo hayo mengine hayana shida
 
Mpira una pressure ule wewe unaandika huku umeweka miguu juu ya sturi na karanga pembeni unaweza ukamkosoa chochote ndio maana wachezaji wakiwa ndani ya uwanja anaweza akafanya tukio la ajabu sana hata kupelekea kupigana ila nje ya uwanja hawezi hata akiuziwa kwa kiwango kile kile maana hakuna pressure yeyote alijitahidi kuchezesha mpira ila kadi zilikua nyingi alitoa akiamini wahuni watapunguza fujo kumbe wapi yeye angepeta tuu zingine kupunguza kadi na mpira uchezwe...
 
Back
Top Bottom