Anayeoa hajui ndoa na anayeolewa hajui ndoa. Usela endelevu hauna tiba

Anayeoa hajui ndoa na anayeolewa hajui ndoa. Usela endelevu hauna tiba

Kichwamoto

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2019
Posts
3,403
Reaction score
4,692
Hello,

Je waoaji na waolewaji wanafahamu na kupata maarifa ya kutosha kuhusu ndoa, why ndoa? Uishije ndoa? Road map ya ndoa inarejea msingi ngapi na ni zipi.

Usipojua haya huna tofauti na masela wenye jinsia tofauti ila wako ghetto na wana mishe mishe fulani.

Hitimisho kama walioa na kuolewa ndio hawa acha tule na wa kwao.
 
Hakuna asiyeelewa isipokuwa zile mbegu za wabishi za Wana wa Israel zilizombishia Musa kurudi Misri badala ya kwenda Kanani hadi ziliposhushiwa kipondo kizito kwa kung'atwa na nyoka ndizo bado zinaendelea kizazi hadi kizazi.

Kwani wangapi wanabaka, wanaua nakati wanaelewa fika si sheria tu za kidini zinakataza huo ushetani bali hata sheria za kidunia?
 
Unakuta mtu kaoa au kuolewa lakini bado anaishi utadhani yupo kwa baba na mama yake!Hapo tegemea vibweka tu na si maisha ya wanandoa.Ndoa ni mchakato.Hauamki tu na kusema..."wee Selina,njoo nikuoe"...!
 
Vijana wa sasa wakishapeana mimba kuhofia aibu wanafunga ndoa mtoto akizaliwa basi mke anakuwa na jeuri na mume anakuwa mchepukaji basi wanaachana
 
Siku hizi ukisikia neno ndoa ujue badae kuna neno ndoano yote yanaenda sambamba ni suala la muda tu.
Na baadaye neno linaanza kupungua kidogokidogo
Ndoa - a = ndo ...kumbe ndo hivi!!!!
Ndoa - N = doa ...ndoa imeingia doa
Doa - D = oa ... unajitoa kwenye ndoa unaoa upya
Oa - O = a ...mtu unajishika kichwa a!!!! Yaani ni yaleyale sioni tofauti
A - A = 0 ... unarudi kwenye usela nondo unatazama haja ya siku hiyo unakimbilia facebook
 
Ila ndoa za siku hizi ni kizungumkuti, cha ajabu zinafungwa kwa mbwembwe na gharama kubwa zikizaa mtoto mmoja au wawili zinavunjika na wanandoa wanarudi kwenye maisha ya usela
 
Hello,

Je waoaji na waolewaji wanafahamu na kupata maarifa ya kutosha kuhusu ndoa, why ndoa? Uishije ndoa? Road map ya ndoa inarejea msingi ngapi na ni zipi.

Usipojua haya huna tofauti na masela wenye jinsia tofauti ila wako ghetto na wana mishe mishe fulani.

Hitimisho kama walioa na kuolewa ndio hawa acha tule na wa kwao.
Finland wanafanya tofauti na tamaduni zingine duniani, wao wanaruhusu watu wanaotaka kuoana waishi pamoja kwa muda fulani ili waone kama tabia na interests zao zina match, wakishajiridhisha kuwa wanaendana na kuelewana wanaoana, wakiona wamelamba galasa wanatawanyika emmediately
 
Shilingi imekuwa ngumu na kuna baadhi hawajui pia kuna kukosa Kwa hiyo matarajio yakienda kinyume mtiti unaanza kwenye ndoa na hatimaye ndoa inaparanganyika
 
Kwani imekuwaje tena? Mbona kama lawama lukuki?
Vuruvuru mikadi ya michango kibao halafu ukiwahoji zero brain kuhusu ndoa zenyewe, nawambia ukishindwa jibu ntakupa elfu25 tu ya usumbufu. Lengo la wapate michango pesa ili wapate kununua vitu na badae vinawagombanisha wanaachana
 
Back
Top Bottom