Anayeona posho haimtoshi afungashe virago - Nchemba Mwigulu

Anayeona posho haimtoshi afungashe virago - Nchemba Mwigulu

Maboso

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2013
Posts
5,164
Reaction score
5,762
Wizara ya Fedha imepigilia msumari maombi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba ya kutaka waongezewe posho na kusema anayeona ameacha kazi inayomlipa zaidi kwenda bungeni afungashe virago na kuondoka.

Msimamo huo umekuja siku moja tu baada ya gazeti hili kudokeza kuwa madai ya wajumbe wa bunge hilo kutaka waongezewe posho kutoka Sh300,000 za sasa kwa siku, yamegonga mwamba baada ya kamati iliyoteuliwa kuchunguza uhalali wake kusema kiwango hicho kinatosha.

Mwenyekiti wa muda wa bunge hilo, Pandu Kificho alisema jana bila kutaja viwango, kuwa ripoti ya kamati hiyo imewasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete kwa uamuzi. Madai ya wajumbe kutaka waongezewe posho, yamechafua hali ya hewa ndani na nje ya Bunge, huku baadhi ya wananchi wakipaza sauti zao na kumsihi Rais Kikwete alivunje bunge hilo iwapo wajumbe watashikilia msimamo wa kutaka nyongeza ya posho.

Jana, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema wanaoshiriki kutunga Katiba ni Watanzania na siyo wataalamu washauri waliokodiwa kutoka nje. Alisema kwa msingi huo, Serikali ilitarajia kuwaona watu hao wakitanguliza uzalendo zaidi badala ya kudai malipo manono. "Katika kutengeneza Katiba hii, hatujakodi consultants (wataalamu washauri) kutoka Uingereza, Marekani, Kenya, Uganda wala nchi nyingine yoyote… Hawa ni Watanzania na kazi wanayoifanya ni yao," alisema. "Wangekuwa wataalamu wa kukodi wangeweza kudai malipo hayo, lakini hapa ni tofauti... wanafanya kazi yao na kila mtu anafanya kazi yake na anapaswa kujivunia kushiriki katika tendo hili la kihistoria kwa kutanguliza uzalendo," alisema.

Nchemba alisema anazielewa hoja za baadhi ya wajumbe walioibua suala la posho, lakini kwa mtazamo wake, hoja hiyo hata kama ingekuwa na mashiko kiasi gani, imewasilishwa wakati usiokuwa mwafaka. Alisema wapo makandarasi na wazabuni waliotoa huduma kwenye taasisi mbalimbali za umma lakini hawajalipwa. Alisema kwa kawaida, Februari ni mwezi mbaya kwa kuwa baadhi ya wilaya zina historia ya kukumbwa na uhaba wa chakula hivyo kuhitaji fedha nyingi za Serikali ili kuokoa maisha ya watu katika maeneo hayo. Pia alisema si wakati mwafaka wa kudai nyongeza hiyo hasa ikizingatiwa kuwa kuna walimu wapya 30,000 nchini kote ambao hawajapangiwa vituo kutokana na kukosekana kwa fedha za kulipa stahiki zao.

Nchemba alisema mbali na walimu hao wapya kutokupangiwa vituo, walimu wengine wanadai malimbikizo ya fedha zao na kwamba hawajalipwa kutokana na ufinyu wa bajeti serikalini. "Siku zote ukweli unauma. Nasema kama kuna mjumbe ambaye anaona huko alikokuwa kabla ya kuteuliwa alikuwa anapata pesa zaidi kuliko hii, basi kwa heshima afungashe virago na kuondoka," alisema.

Aibu kwa mjumbe

Akizungumzia suala hilo la posho, Mjumbe wa Bunge hilo, David Kafulila (picha ndogo chini) alisema ni aibu kwa wajumbe ambao wameaminiwa na Watanzania na kupewa jukumu zito la kutunga Katiba, kuanza kujadili nyongeza ya posho. "Ninachokiona ni tatizo la standard (viwango) vya posho… hakuna standard kwamba posho ilipweje, kwa nani na kwa kiasi gani. Mtu akidai leo kwamba Sh300,000 ni ndogo tunajiuliza ni kwa standard ipi?" alihoji.

Kamati ya Posho

Kamati iliyoundwa na Mwenyekiti wa Muda wa bunge hilo, Pandu Ameir Kificho kushughulikia madai ya nyongeza hizo, zinasema imeshauri kuwa kiwango kinacholipwa sasa kinatosha. Kamati hiyo inaundwa na William Lukuvi, Mohamed Abood Mohamed, Freeman Mbowe, Paul Kimiti, Jenister Mhagama na Asha Bakari na taarifa yake imekwishakabidhiwa kwa Kificho.

Mmoja wa makatibu wa bunge hilo, Yahya Khamis Hamad alikaririwa juzi akisema suala la posho limetoka mikononi mwa Kificho na mapendekezo yake yameshapelekwa serikalini. Hoja ya kutaka nyongeza ya posho iliibuliwa na wajumbe wawili ambao pia ni wabunge wa CCM, Richard Ndasa (Sumve) na Suleiman Nchambi (Kishapu).


SOURCE: Mwananchi
 
Jamani kumbe Naibu waziri wetu wa Fedha ni Jembe! amepigilia msumari juu ya hoja ya wajumbe wa bunge la katiba ya kutaka kuongezewa posho soma hii..

Jana, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema wanaoshiriki kutunga Katiba ni Watanzania na siyo wataalamu washauri waliokodiwa kutoka nje.


Alisema kwa msingi huo, Serikali ilitarajia kuwaona watu hao wakitanguliza uzalendo zaidi badala ya kudai malipo manono.


"Katika kutengeneza Katiba hii, hatujakodi consultants (wataalamu washauri) kutoka Uingereza, Marekani, Kenya, Uganda wala nchi nyingine yoyote… Hawa ni Watanzania na kazi wanayoifanya ni yao," alisema.

"Wangekuwa wataalamu wa kukodi wangeweza kudai malipo hayo, lakini hapa ni tofauti... wanafanya kazi yao na kila mtu anafanya kazi yake na anapaswa kujivunia kushiriki katika tendo hili la kihistoria kwa kutanguliza uzalendo," alisema.

Nchemba alisema anazielewa hoja za baadhi ya wajumbe walioibua suala la posho, lakini kwa mtazamo wake, hoja hiyo hata kama ingekuwa na mashiko kiasi gani, imewasilishwa wakati usiokuwa mwafaka.

Alisema wapo makandarasi na wazabuni waliotoa huduma kwenye taasisi mbalimbali za umma lakini hawajalipwa. Alisema kwa kawaida, Februari ni mwezi mbaya kwa kuwa baadhi ya wilaya zina historia ya kukumbwa na uhaba wa chakula hivyo kuhitaji fedha nyingi za Serikali ili kuokoa maisha ya watu katika maeneo hayo.

Pia alisema si wakati mwafaka wa kudai nyongeza hiyo hasa ikizingatiwa kuwa kuna walimu wapya 30,000 nchini kote ambao hawajapangiwa vituo kutokana na kukosekana kwa fedha za kulipa stahiki zao.

Nchemba alisema mbali na walimu hao wapya kutokupangiwa vituo, walimu wengine wanadai malimbikizo ya fedha zao na kwamba hawajalipwa kutokana na ufinyu wa bajeti serikalini.

Hongera kumbe wakati mwingine jamaa tunamlaumu bure, kumbe ana point bwana!!

 
kashalimaliza sakata la EFD au bado anahangaika tu na CDM kule Iramba!!
 
Mwigulu ni msomi na mwanasiasa anayejua anachikisema. Wabunge la katiba sio consultants, ni watanzania ambao wakiwa kwenye shughuli za taasisi wanazotoka wanalipwa 80,000 kwa siku kamaposho ya kujikimu nje ya kituo cha kazi. hiyo huwa inatosha na nyingine wanapewa warembo. Iweje 300,000. Ingekuwa mimi ningekodi chumba cha elfu 30 kwa mwezi nibane matimizi lakini nifanye kazi yangu na ya watanzania wenzangu.
 
tatizo lake moja kudhani CDM hawana hoja sometimes angechukua na hoja kidogo ya wapinzani angefika mbali
 
Mtaendelea kujidanganya na kudanganyika. Thinking capacity ya wabongo wengi ni ndogo sana so huwa wepesi wakudanganywa na kudanganyika kwa vitu vyepesi vyepesi sana.
 
FOR THE FIRST TIME MWIGULU ANAPATA CREDIT KWA MTIZAMO NA MSIMAMO! bigup
 
FOR THE FIRST TIME MWIGULU ANAPATA CREDIT KWA MTIZAMO NA MSIMAMO! bigup

Wanaodai nyongeza ya posho ni wana ccm wenzake anaonaje kama wataadhibu ccm kwa kuikubali serikali 3?pia mwigulu hayo maneno kasemea wapi?isije ikawa kama mzee sitta anavyoropoka makanisani lakini kwenye vikao halali vya serikali anakua kondoo.Nchambi ana pesa ya ujangili wa tembo laki 3 kwake ni ndogo
 
Mtu kama Paulo Makonda naye unamchagua Bunge la Katiba unategemea nini? Na kama kawaida yake lazima angekuja na hoja mbovu kama hiyo.
 
Mi nashangaa huyu chambi si ndo aliekua na mabasi ya chambi's leo yanajulikana kama ,mombasaraha,mbona ni tajiri sana,kung'ang'ania posho ya laki tano
 
Mtaendelea kujidanganya na kudanganyika. Thinking capacity ya wabongo wengi ni ndogo sana so huwa wepesi wakudanganywa na kudanganyika kwa vitu vyepesi vyepesi sana.

Ukiwa kama great thinker epuka sana generalization..

Haya wewe nadhani thinking capacity yako vilevile ni ndogo kama ya wabongo wengine..
 
Suala zima la posho kwa watendaji wa serikalini, mashirika ya serikali na makundi mengine yanayowajibika kwa niaba ya serikali inabidi liangaliwe upya kwani hivi sasa Posho ni kikwazo kwa utendaji bora na uwajibikaji. Ni vema taratibu mpya ziwekwe za jinsi ya kuwakimu watendaji ili wasilipwe posho ambazo zinakuwa ni kipato mara mbili pamoja na mishahara yao kwa kufanya kazi ile ile waliyoajiriwa kwayo.

Kwa vile posho zinakuwa ni nyingi kuliko hata mishahara, hivi sasa watendaji wengi hawakai maofisini mwao, bali wanakuwa kila kukicha wanatafuta safari na semina zenye kulipa posho na hivyo
kuzorotesha mchango wao halisi wa majukumu waliyopewa.
 
Hoja ya kutaka nyongeza ya posho iliibuliwa na wajumbe wawili ambao pia ni wabunge wa CCM, Richard Ndasa (Sumve) na Suleiman Nchambi (Kishapu).
Source:Mwananchi
 
Najuta kumpa kura yangu Ndasa 2010!Sitarudia tena aisee....
 
Mwigulu is right. Posho ya shilingi 700,000 kwa siku ni kutengeneza tabaka la kinyonyaji si bunge la katiba. Watanzania wanauza kuku ili walipe kodi, leo kundi dogo lililoaminiwa kutengeneza katiba kwa niaba ya watanzania wote wanataka waishi Dodoma kama machifu wa Nigeria? Hata hivyo, washukuriwe wajumbe wote waliosimama na wananchi kupinga onggezeko la posho bila kujali manufaa yao binafsi.
 
Back
Top Bottom