Anayepanga mechi za Ligi Kuu Tanzania hana maana

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Leo saa 18:30 kuna mechi ya Chelsea na Liverpool halafu saa moja mechi ya Simba na biashara.

Nina hamu kuona Simba anafanyaje leo lakini itabidi tu nilazimike kuangalia mechi ya Liverpool.

Huu upangaji ni kama hujuma tu kwani hamtaki hata hao wachezaji waangalie mechi kubwa za PL?

Kibaya zaidi mnatugawa sisi washabiki.
Ni vizuri mkipanga mechi muwe mnaangalia ligi hii pendwa ya uingereza ina mechi gani.Vinginevyo mtaathiri hata mapato ya Azam TV msipotumia akili na mkabaki na akili za kulimia mikorosho
 
Na wewe inapoteza muda wako kuangalia game za Mikia F.c wazee wa bukutatu
 
Ratiba za ligi za Afrika matatizo makubwa.

Kuna mwaka World Cup inachezwa lakini baadhi ya ligi za Afrika zilikuwa zinaendelea. Mpaka Unajiuliza kwani tumelogwa na nani?!
Kombe la Mataifa Afrika huwa linafanyika huku ligi nyingi zikiwa zinaendelea barani Afrika.

Kwa influence ya ligi ya Uingereza ni vyema TFF ingekuwa inazingatia hilo.
 
Dah tunatofautina sana kama alama za vidole vyetu inavyotofautina. Kwangu miye haijalishi anacheza nani iwe mashujaa na simba ama yanga na jang'ombe sijui mtwivila fc na mundu fc(washamba wa ng'ambo), au tukuyu star vs 82 rangers. Nitaangalia kwanza hyo huko kwingine labda nichungulie tu kwenye livescore. Infact napenda sana ligi ya bongo tangu enzi hzo nikisikilza kwenye RTD akna uncle father Ahmed Jongo, Swedi Mwinyi, Ezekiel Malongo, halima mchuka wakirindima kwenye receiver zetu za mkulima
 
Yaaani wapange ligi kwa kukwepesha mechi za ligi ya uingereza?

Lawama zingine hata ukiambiwa mwenyewe upange ratiba inayowezesha ligi kuisha kwa mda muafaka huwezi. Acha lawama.
 
Haya ni mawazo muflis kabisa. Ligi ya Uingereza ndio kitu gani? Kwa akili zako Watanzania wanapenda Ligi ya Uingereza zaidi ya timu zao za nyumbani? Nina DSTV na Azam TV lakini mechi ya Simba ilipoanza niliachana na Liverpool. Kila mtu ana mapenzi yake na furaha unaichagua hupangiwi.
 
Tumesikia kilio chako. Tunakifanyia kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…