Imagine: Najitoa kila unapohitaji msaada wangu, sisiti kutumia chochote ili kukufurahisha, najitahidi kwa kila njia nisikuudhi, nakuletea zawadi kila mara, usipoonekana nalalamika kuona wivu, nakusifu kupendeza kila wakati, nakuomba mara kwa mara usiniache kwa kuwa nakupenda sana, nawajali wazazi wako na ndugu zako wote wananipenda na muda wote nawafaa ninapohitajika. Ninafanya yale unayosema wewe na si mwingine. Unaposema tusubiri nakubali na unaposema ok basi nahakikisha hujutii kuwa na mimi, bado unapougua nahangaika na kupozi kwa majonzi na unapopona nakufanyia pati na mazuri mengine yote yanayoweza kufanywa na mtu anayekupenda. Je hii inamaanisha ninakupenda kweli? Hakuna uwezekano wa mtu mwenye agenda yake kufanya vitu hivi tena kwa umakini mkubwa kiasi cha kuwaaminisha watu kuwa ni chaguo bora na la pekee?
[/QUOTE=Gaga;2080410]Anayependa kweli anajitoa kwa moyo wake wote, ila yule anayeigiza utamjua tu, hata kwa kuwangalia, na hata siku moja hawezi kusucrifice kitu chochote juu yako, na wala hajali akikuumiza kwa lolote[/QUOTE]