Jamiitrailer
Senior Member
- Oct 20, 2019
- 190
- 452
Kuna mtu kasema eti PEOPLE'S POWER haina nguvu mbele ya silaha. Sijui anamaanisha nini..,lakini ni wazi anafanya upotoshaji wa wazi na wa makusudi. Sayansi ya siasa na historia vinathibitisha kwamba NGUVU YA UMMA siku zote imeonesha kuwa matokeo chanya katika jamii.
Soma pia Kauli ya people power IPO kisiasa. Hakunaga nguvu ya umma mbele ya wenye silaha hata wawe Mia moja tu
1. Watu wa iliyokuwa jamhuri ya Cźchoslakia walipochoka kuburuzwa na utawala wa dikteta mkomunisti Nicolae Ceausescu waliingia mtaani na kuandamana kwa maelefu kuelekea iikulu na kumng'oa madarakani. Kabla ya hapo jeshi na vyombo vya usalama vilikuwa vikiwapiga jela na kuwapoteza watu kila leo ili kuzima ukosoaji. Uwingi mkubwa wa watu ulifanya jeshi lisite kutumia nguvu.....walijiuliza waue watu laki kadhaa kwa maslahi ya nani?
2. Utawala wa Joseph Estrada wa Philipines uliogubikwa kwa rushwa na uzembe na uliondeshwa kwa hila uling'olewa baada ya maandamano makubwa ya wananchi nchi nzima...hiyo ikiwa pamoja na wafanyakazi wa serikali. Umma ukiitikia kwa mfano huo jeshi lenye silaha litasaidia nini kuwafanya watu waende maeneo ya kazi? Kukishakuwa na standstill kila kitu,kila shughuli inasimama. Uongozi unaongozaje?
3. Robert Guei mtawala wa kijeshi wa Liberia ilibidi akimbie ikulu baada ya wananachi kuandama kwa uwingi na nguvu.
Ingawa mwanzo wa maandamano jeshi lilishambulia wananchi na kuua watu zaidi ya 500,lakini uwingi wa watu ulipozidii jeshi likaamua kuwa upande wa watu na kumtosa mwanajeshi mwenzao Guei.
Hata maandamano ya Tz ya Oct 29 yangefikia uwingi unaohitajika, leo hii Samia na ccm yake wasingekuwa madarakani.