Abel Ndundulu
JF-Expert Member
- Sep 17, 2015
- 846
- 388
Huyu mke anaweza kuwa hajui kuwa kwenye ulevi ndio kuna michongo!! Ona sasa amejisababishia ujane!!Jaman wale mnaopenda kulewa au kuchelewa kurudi majumbani mwenu kwa sababu za starehe kama hizi muwe mnakuwa na funguo za ziada ili ukirudi unajifungulia mwenyewe kuepusha vifo visivyo vya lazima.
Inachosha sana kuamshwa na mtu aliyetoka kwenye starehe zake ukatishe usingizi wako ili umfungulie
Usingelisema mpare ningekuibukia kama mwewe!!Bora na ww umejionea.
Na akirudi vurugu. Lipo lipare limoja la makanya linafanya bandari nalo lina tabia za kula starehe huko na madanga halafu likirudi limelewa chakarii linampiga maza angu mdogo.... linanikera natamani hata lipate majanga Leo kesho.
We libaba kama unasoma hapa jua tu kwa matendo yako sikupendi kama m****avi
Na wewe una tabia hizo eeh ?Usingelisema mpare ningekuibukia kama mwewe!!
Michongo gan bwana zaidi ya kuspend?Huyu mke anaweza kuwa hajui kuwa kwenye ulevi ndio kuna michongo!! Ona sasa amejisababishia ujane!!
Riki nauchukia ulevi pia hata hao wanawake huvumilia mengi....pia nao ni binadamu wana nyongo.....Yani kama ukilewa ukirudi kwako lazima uruke ukutaa achana na pombe tuu maana nyumba yako tu imekushinda kuicontrol...!! Mwanamke anapaswa kumfungulia mumewe mlango muda wowote...saa yoyotee
Kweli mkuu me hapa naongelea mtu anarudi saa 4 saa 5 usiku yani kweli aruke ukutaa...??? Ndo kuvumiliana kwenye raha na shidaa mkuu[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Riki nauchukia ulevi pia hata hao wanawake huvumilia mengi....pia nao ni binadamu wana nyongo.....
Huwa na kunywa sizidishi kiwango pia kuepuka kampan za ajab ajab.....pombe sio shetani shetani ni mtu mwenyewe....
ThanksHawezi
Mtoto ukimuonesha upendo toka mtoto akiwa mchanga hawezi kukusahau kamwe...anaona the sacrifice u make and the like
Ila for sure Kuna wanaume wanaboa sana wakilewa....Kweli mkuu me hapa naongelea mtu anarudi saa 4 saa 5 usiku yani kweli aruke ukutaa...??? Ndo kuvumiliana kwenye raha na shidaa mkuu[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Wanawake HAMUELEWEKi mnachongea sio kitu ambacho kipo kwenye HISIA zenu unaweza unaweza ukasema ahh siolewi na mnywa POMBE ukaolewa na ukaishi vizuri tu vitu mnavyoongea mara nyingi hammaanishi nyie ni HISIA ndio zinawafanya mtende mtendayo I'm out
Ameeeeen...Dah almost umenitoa machozi , haka kabinti kangu nakaombea kawe kama wewe .
Itikia Amen kwa afya ya furaha yangu
Amin tena kwenye vikao kuna michongo sana.Michongo gan bwana zaidi ya kuspend?
Ningefrahi ingelikuwa ni mimi, hakuna hasara yoyote anayopata mtu aliyekufaSiyo mpwayungu kweli
Huyo mkewe tumwite nani?Memba mwenzetu ametangulia mbele ya haki. Pengine nisingejisumbua kuripoti huu msiba lakini mazingira ya kifo chake ni ya kuhuzunisha na yenye mafunzo. Sijui username yake ya JF kwani tulikutana ''casually'' kwenye kilevi mwezi wa tatu mwaka huu tena siku moja tu. Katika maongezi alinijulisha kuwa yeye ni ''active member'' wa JF na anapenda sana kuchangia. Baada ya kilevi (maeneo ya Boko) tulipokuwa tunaondoka akanionyesha nyumbani kwake na mimi nikaondoka kurudi kwetu Msasani ninakoishi.
Fast forward, wiki kama mbili zilizopita nilirudi tena maeneo tuliyokutana kwenye mishe zangu. Nikaona msiba kwenye boma aliloniambia ni nyumba yake. Kuulizia kulikoni nikaambiwa ni yeye, mwenye nyumba amefariki. ''Eti'' alitoka kwenye kilevi usiku, akagonga geti, mke akagoma katukatu kumfungulia. Akachukua uamuzi wa kuruka ukuta. Kwa bahati mbaya akachomwa na moja ya nondo zilizoko kwenye geti la nyumba (nadhani wengi mnafahamu nondo zinazochongwa kama mkuki na kuwekwa juu ya kuta au geti ili kuzuia vibaka). Kwa bahati mbaya akavuja damu nyingi mpaka akapoteza maisha. RIP member.
Ulevini tunakuwa na funguo za gari tu hayo mafunguo mengine sie tusiokaa nyumbani hatuyaweziAmetoa ushauri muwe na funguo zenu, hujaona? Umeona tu roho mbaya ya huyo alogoma kufungua mlango?
Yan mtu umejizoelea kulala saa 4, mumeo mlevi anakaa bar mpaka saa7/8/9, kuamshwa kila wakati hivyo inaboa sana.
Pombe ni mbaya sanaPole kwa wafiwa..
Mi nilikuwa na mazoea hayo ya kulewa na kurudi usiku naruka hizo nondo asubuhi najikuta nimekwaruzika mwili mzima kisa cha kuacha mchezo huo sitasahau.
Nilirudi siku hiyo kilevi kimezidi kuliko kawaida nikapiga simu na kugonga sikufunguliwa nikachukua maamuzi ya kuruka. Niliacha kila kitu juu ya nondo surwali shati hadi boksa. Nikaingia ndani nikalala na viatu tuu. Asubuhi kidogo mama angu afe kwa presha akajua nimeuliwa nikatupwa juu ya nondo kumbe nguo. Akaingia ndani nimelala uchi akanikagua mzima zaidi ya michubuko tuu. Sitasahau