Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,183
- 2,100
Wakuu,
Hapa Majuzi Mbunge Musukuma alisema Bungeni kuwa wenza wa Wabunge wawe wanaruhusiwa kukaa VIP kama wenza wao.
Nimependa hoja ya Mzee wa Kaliua (Oscar oscar) kwamba kila anayetaka ViP basi alipie, kwasababu tukiruhusu tu wenza kupata huduma hiyo, basi ipo Siku watoto wao na wajukuu wao watataka pia
Nakubaliana naye 100% kwasababu katika jamii ya kidemokrasia na usawa, VIP treatment zinapaswa kutolewa kwa misingi ya haki, si kwa misingi ya uhusiano wa kifamilia au ukaribu na viongozi wa serikali.
Wazo la kuwaruhusu wake/waume wa wabunge (MPs) kupata huduma za VIP bila malipo linaweza kuwa na athari kubwa katika mfumo wa utawala bora, matumizi ya rasilimali za umma na kuendeleza tabaka la upriviliged.
Halafu ni Matumizi Mabaya ya Kodi ya Umma. Huduma za VIP aghalabu hutumia rasilimali nyingi: magari maalum, walinzi, maeneo ya kifahari, Hizi gharama zinalipwa kwa kodi ya wananchi, na si haki kodi ya mtu wa kawaida itumike kumpa starehe mtu kwa sababu tu ameolewa na mbunge.
Huduma za VIP Zipo Kwa Mlipaji, Kama mtu anahitaji huduma ya VIP iwe uwanja wa ndege, hospitali, au sehemu nyingine yoyote zipo kwa gharama inayojulikana. Mtu yoyote anayehitaji starehe au upendeleo wa hali ya juu anaweza kulipia. Huu ndio usawa wa kweli.
Kama mtu anataka starehe au heshima ya ziada, ni vyema alipe kama walipavyo wengine. Mfumo wa VIP usitumike kuendeleza tabaka la kifamilia bali kwa wale wanaohitaji na wako tayari kugharamia.