Kuna shule moja ya KKT walishindwa kuiendesha kutokana na ukosefu wa wanafunzi, wakaamua wampatie mwamba mmoja mwalimu mstaafu aisimamishe hiyo shule kwa makubaliano ya mkataba.
Alichofanya yule mzee ni kutafuta vijana wa kazi, aliofanya nao kazi zamani; akaanza kutoa matangazo mkoa kwa mkoa, wilaya kwa wilaya n.k, watu wakakabiziwa fomu iwe kwa mwalimu, mwanakijiji, vijana n.k, na ela ya fomu ilikuwa inabaki kwa mwenye fomu.
Watu wakawa wanakimbilia fomu na kuuza ili wapate hela, baada ya muda mfupi shule ilisimama, wanafunzi wakawepo wa kutosha.
KKT baada ya kuona hivyo, wakaanzisha mizwenge ya kutaka shule yao, baada ya mgogoro kuwa mrefu, wakaachiwa shule, na kwa sasa shule ilishakufa.