BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Mshtakiwa katika Kesi Namba CC.5866, Baraka Benedicto ambaye anashtakiwa kwa kosa la ulawiti, licha ya kufika Mahakamani, Februari 26, 2025 ameshindwa kutoa ushahidi wake kama ilivyopangwa kwa maelezo kuwa anaumwa.
Kesi hiyo ambayo ina kipindi cha mwaka mzima tangu ilipoanza kusikilizwa ilitajwa kwa ajili ya mshtakiwa kutoa ushahidi wake ikiwa ni baada ya mashahidi wa Jamhuri kutoa ushahidi wao.
Hivyo, kufuatia hoja ya mshtakiwa kuhusu afya yake, Mahakama kupitia Hakimu Nabwike Mbaba imeahirisha shauri hilo mpaka Machi 3, 2025, ambapo mshtakiwa atakuja kutoa ushihidi wake.
Baraka Benedicto ambaye kabla ya kutiwa mbaroni alikuwa mlinzi katika Parokia ya Bikira Maria Mama Mwokozi-Sinza, ambapo alipandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni na kusomewa shtaka moja la kuingilia mtoto kinyume na maumbile.
Mshtakiwa huyo inadaiwa alimuingilia mtoto wa kiume kinyume na maumbile 'ulawiti' katika vyoo vya Parokia hiyo.
Ikumbukwe kuwa, hatua ya kufikishwa mahakamani ilikuja baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kuripoti madai hayo na kutaka hatua stahiki za Kisheria zichukuliwe.
Kilichotokea kuhusu kesi hiyo, soma hapa:
~ Serikali imsaidie Mtoto huyu anayedaiwa kulawitiwa na Mlinzi wa Kanisa Katoliki Sinza
~ Dar: Mlinzi wa Kanisa anayetuhumiwa kumlawiti Mtoto Muimba kwaya kwenye vyoo vya Parokia apandishwa kizimbani
~ Madai ya Mlinzi wa Kanisa Katoliki Sinza kumlawiti Mwanafunzi, mama wa Mtoto aomba Serikali imsaidie
~ Tukio la Mlinzi wa Kanisa Katoliki Sinza kudaiwa kumlawiti Mwanafunzi, Padri asimulia kilichotokea
~ Anayetuhumiwa kumlawiti mtoto katika Vyoo vya Kanisa la Roma Sinza, asema “Sina lolote, naiachia Mahakama”
- Mlinzi wa Kanisa (Sinza, Dar) aliyeshtakiwa kwa kumlawiti mtoto kwenye vyoo vya Kanisa, atupwa jela Miaka 30