Anayetumia passo ya piston 3(au fundi/mjuzi yeyote) tafadhali nisaidia ubora wake na udhaifu wake

The golden amejibu vema... Epuka gari yenye cc ndogo maranyingi sio imara... Kama unataka gari yenye cc ndogo basi opt Suzuki Gypsy, Jimmy au Samurai na kwenye Toyota opt Duet

Jr[emoji769]
Mkuu Duet ni imara kuliko Vitz?
 
mi ninayo Passo toka 2015,nipo nako hadi leo,ila kangu kana gonga sana miguu ya mbele,niliacha kitengenenza maana nakaa makorongoni nakaumiza we acha tu,...vigari vidogo shida sana,nikimaliza mkopo tu nakauza
Maana nilichukua mkopo sehemu nikaweka kwenyewe ndio dhamana
 
Lakini naona vinasoko sana sijui watu wamegundua nini tofauti na mafuta ulaji wake
mi ninayo Passo toka 2015,nipo nako hadi leo,ila kangu kana gonga sana miguu ya mbele,niliacha kitengenenza maana nakaa makorongoni nakaumiza we acha tu,...vigari vidogo shida sana,nikimaliza mkopo tu nakauza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni bora ununue starlet kuliko paso, by the way usihadaike na bei ya io paso itakutesa ukajuta tafuta gari standard usiwe na haraka sana angalau cc 1990 kama hizi premio au allion... Otherwise chukua subaru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usirogwe kununua vigari vyenye piston tatu vina shida sana, me nilikuwaga na Suzuki Kei ilikuwa ni kila leo niko garage mara kamekata fan belt, mara kameunguza solenoid kwenye gearbox ikabidi nikauze tu. Kama ni gari ndogo chukua Vitz old model, ni vigari imara sana
 
Chukua toyota carina.gar nzur na inanusa mafuta.elf5 unafika mjin

Sent using Jamii Forums mobile app
Ki-ukweli Carina ni gari ngumu .Ni gari inayovumilia shida .Ni gari ya watu wenye kipato cha chini. Gharama za kuitunza ni za chini kabisa.

Labda changamoto ni kuwa gari hii imekuwa ya kizamani sasa. Na nyie vijana mnapenda kwenda na wakati.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…