Anayeweza kuitafsiri hii ndoto anisaidie

Anayeweza kuitafsiri hii ndoto anisaidie

Hauchezewi mimi nimtafsiri tena nibure kabisa si uongo wa mitandao, anayekuchezea ni mama yako sali sana kwasababu mama yako yupo kwenye makundi ambayo amejiunga nayo na sasa yanakuhitaji, kwa lolote wanachotaka kufanya , ukiona mama yako anaumwa mguu ujue wameshindwa ukiona amepona ujue unatumika mwombe mungu sana ukiwa kwenye taja hata jina la BWANA YESU KRISTO MWOMBE MUNGU ALIYE HAI AKUTOE MAZINGIRA hayo kwani unapocheka inamaanisha hauwaogopi wanapokufuata inamaanisha wanakuhitaji kwa kazi yao unapoingia kwenye banda ni umejificha alipokubeba inamaanisha walifanikiwa kukupata kisha ukapotea ndiyo maana unasikia sauti ikikuita kwasababu huonekani kwenye ndumba zao sali sana mpendwa hiyo ni hatari, akiumwa tena zidi kusali uko kwenye mazingira mabaya kiimani , unapoambiwa na watafsiri kwamba unachezewa na mtu wakaribu inamaanisha huyo unayoongea naye, uswambie mama yako ndoto zako tena jaribu kuwaambia watu wengine Mungu akubariki sana na akulinde kila baya linaloendea kuharibu maisha yako ninakemea kwajina la YESU KRISTO Aliye hai.
Mama mwenyewe baadae aliniambia vile alivyoota na kunisisitizia niwe nasali, nisiwe naacha.
Au na yeye hajui chochote labda wanamtumia?

na hapo vipi uliposema nisimwambie ndoto zangu, hapa sijakuelewa, ndoto za kimafanikio ya kiuchumi au ndoto gan?
 
Samahani, mimi leo nimeamka nikapigiwa simu na mdogo angu akanambia kuwa mama yetu aliota usiku wa kuamkia leo kuhusu mimi, kuwa nilikuwa niko porini, alafu watu wananisemesha ila mimi siwasikii. NDOTO HIYO.

Baadae saa 11 jioni, nilikuwa chumbani peke angu alafu mlango nilikuwa nimeuegesha ila gafla nikasikia sauti inaniita kama mara mbili ivi, kupitia pale mlangoni wa chumba changu, nikatoka kwa woga kufata sauti inapotoka sioni kitu, kisha nikatoka kwenda kuongea na mama kwenye simu kumuuliza ile ndoto, akanielezea kuwa , jana mida ya saa tano usiku alijihisi mguu unamuuma, akachukua dawa akajichua ,kidogo akapitiwa usingizi gafla akaanza kuota ndoto, kuwa akiniona niko porini alafu, yeye akiwa na baadhi ya watu wananiita ila mimi nikageuka nikacheka kisha sikuwajibu kitu nikaenda zangu, pembeni katika kakibanda kadogo nikaingia , ila wenyewe wakanifata na kuniita nitoke nikakaa kimya.

Mama mwenyewe akanijia mule bandani akanibeba na kunikalisha, hapo mama akashituka ndoto ikaishia hapo, ila pia palipo kucha mguu ulimuuma tena akauchua mpka sasa hasikii maumivu tena. Sasa mtumishi nahisi nimeingia katika vita ya kiroho mimi na mama yangu , nahisi tunachezewa, ila sijajua na watu wapi wanaofanya ivyo, nimeenda kwa watafusiri mbali mbali , mmoja kaniambia ni masuala ya mizimu, mwingine kanambia kuna namna nafanyiwa na watu wa karibu, naombeni wajuzi wa mambo mnipe ushauri🙏.
Wee jamaa acha kuchosha watu na mandoto yako ya nguvu za giza! Kuna Member mmoja hapa mwenye avatar ya mzee hivi (I guess) alikutafsiria vizuri tu! Wee endekeza kushobokea mandoto ya kichawi utadata!
 
Mama mwenyewe baadae aliniambia vile alivyoota na kunisisitizia niwe nasali, nisiwe naacha.
Au na yeye hajui chochote labda wanamtumia?

na hapo vipi uliposema nisimwambie ndoto zangu, hapa sijakuelewa, ndoto za kimafanikio ya kiuchumi au ndoto gan?
Kwasababu hujui ni nani ni adui, wewe unahisi huna adui lakini huwezi kupendwa na kila mtu, ukiwaambia watajuwa kuwa wewe unafahamu wanachofanya kila watatumia njia nyingine,yatakusanywa majeshi unaweza kupambana nayo??
 
Back
Top Bottom