Anayopitia mdogo wangu wa kike siyo sawa na umri wake, inaniumiza sana...

mpe support kulea! We ndio mjomba na ndie baba wa hiari wa watoto wa dada yako
 
Nani unampa lawama? Au hujasoma na kuelewa mada
 
Umenikumbusha mbali sana
Mimi mshua wangu hajafa yupo ila amejua kunihenyesha,wakati nimeanza chuo mwaka wa kwanza akalipa ada semester ya kwanza,ya 2 akanipigia simu akasema nisimtafute kwa simu manake atakua hana ela miaka yote wakati ni mtu mwenye uwezo wake,kama utani nikaacha chuo nikabaki home napalilia mihogo!
Badae nakuja kujua kumbe ameoa bi mdogo ambae mi nimemzidi umri yan mdogo wangu anampa full bata na yule bi mdogo yuko busy kunipa pole vile mshua wangu hanithamini,ananiambia anamshangaa sana mshua wangu tena anasema ye mwenyewe anamchuna tu ila akishamfanikishia mishe zake anamwacha anasepa na kweli yule binti aliishia kuchuna na kusepa huku mie sent 5 ya mshua siioni!mengine ngoja nisiandike, ila
Duniani huku sometimes maisha ni machungu sana japo sio kwa wote!
 
Kwanza nianze na kukupa makavu katika ID zenye tabia mbaya Ni yako hii unapenda sana kutoa dislike hata kwa comment isiyokirihisha mi nilikuwa sikajui hako kakitufe mpk siku moja uliponipa,na Mimi nimekupa hatimaye,,
Inaonekana mapito yako yanakufanya utupe dislike ovyoovyo tu,,( kananiboa hako kaemoji kananiogopesha sikapendi kabisaa kapo kama kashetani, jf wakatoe jamani wengine sie Ni waoga balaa)

Tukirudi kwenye mada yako, nakupa pole na pongezi ya kumlea ndugu yako, mtafute mtu aliye kwenye dawati la ustawi wa jamii, akusaidie kuwabana baba wa hao watoto wawajibike katika malezi ili kukupunguzia mzigo,, vilevile mtafutia mdogo wako biashara ya kufanya walaua aingize chochote kitu wakati huohuo umpeleke hospital aanze uzazi wa mpango kama mbishi mzunguke aanze kutumia uzazi wa mpango tafuta nesi amzuge kaugonjwa ili amchome sindano ya uzazi mchezo unaishia hapo
 
Mshauri Dada yako asipate Mimba tens afanye vibiashara vidogo make pamoja ili umsaidie kulea watoto. Asizae kwanza atulie. Na wewe kaka Dada yako anapataje mimba nyingine na wewe upon? Ongea nae mshauri mtahadhalishe awe na msimamo vinginevyo mtaumbuka
 
Pole. Forgive him.

Hata wazee wetu ni binaadamu na hufanya makosa vile vile.
 
Wanawake muda mwingine n wajinga sana.
Anapgwa mimba anatelekezwa,anahangaika nayo baada ya muda kidogo unaona kapgwa nyingine tena,huu ni upumbavu.

Kama umeamua kutumia uchi kutatua changamoto,basi tumia njia ztakazo zuia mimba.

Mimi wanawake wa hiv hata huwa siwahurumii hata kidogo
 
Ulitaka wazazi wafanyeje? Wakamchukue binti yao kinguvu kwa mwanaume wake aliyeridhia kuwa nae bila kulazimishwa?
 
unaogopaje aka kadude 😡😡 🤣 lbd pengine ni staili yake ya kujitambulisha humu
 
Maisha yana changamoto nyingi sana. Kifua chako kina mengi sana lakini usichoke kumshika mkono dada yako maana anakuhitaji sana kuliko unavyodhania mkuu
Bado anaamini hushindwi kitu na anakuombea sana too early to give up bro keep stron and maintain ukiamini kuna siku mungu atarudisha tabasamu lililopotea usoni mwenu either kupitia wewe au sister yako
Allah Kareem ya shabaab!!
 
Niritaka kusema hivyo! Kumbe kiko na stress za maisha kinajifanya kiccm zaidi ya ccm yenyewe!
 
Simameni na dini muwe na ushirika ni rahisi kupata msaada wa kimawazo au mali maana panapowengi waliosimama na Mungu hamtobaki wakiwa.Hio ni mitihani haina budi kuishinda watoto ni baraka bila kujali wamepatikanaje.
Usikate tamaa Hakuna matatizo mapya duniani ambayo wengine awakuwahi pitia wapo waliokuwa wakilala nje kariakoo leo wanamiliki maghorofa na majumba ya kulala wengine miaka 15 iliyopita tulikuwa ni walinzi tukilinda watu waliolala ndani leo tunalala ndani tukilindwa,atukuwahi kata tamaa Hakuna giza lidumulo milele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…