Anayopitia mdogo wangu wa kike siyo sawa na umri wake, inaniumiza sana...

Thank you my dear
Nimejifunza sana
Mungu anisaidie nisipite njia hiyo watoto ntawaumiza wakati hawana hatia
It,s more like psychological torture and trauma
Amen Amen Dear
 
Maisha haya una watoto wawili na baba zao kawakupi hata 100 ya kununua japo chakula na wewe mwanamke huna chochote hata mtaji bhasi usipochukua uamuzi mgumu wa kwenda kuwapeleka kwa baba zao kwa heri ama kwa shari kuna siku unaweza wapa sumu na wew ukajiua ukidhani ndio njia pekee na jibu.
 
Kama huwezi kumsaidia mdogo wako pole sana lakni msaidie awapate wanaume aliozaa nao yani japo atakuja onekana mama katili watoto wakikua ila hana jinsi.. Akishdwa kuwapata bhasi msaidie japo mtaji kama huna mwambie aweke njia ya uzazi wa mpango ajiongeze. Pole sana!
 
ndio shida za vijana siku hizi, wakati mwingine labda hawahitaji misaada halisi wanataka michango labda[emoji2960]
 
Pole sana jamaa yetu,, mnapitia magumu kwakweli, ila nnacho kuomba ujaribu tu kubariki haya maisha kwamaneno yako mwenyewe... Ukiwa unalaumu maisha nakusema maisha ni ovyo yanakua ovyo hivohivo... Lakini ukisemea mazuri mazuri yatakuja hata Kama sio leo...
Mungu akutie nguvu akupe furaha na maisha bora ili usaidie na ndugu zako na wote wenye shida maana unajua shida ninini naamini ukitoboa hutosahau kusaidia waitaji... Mungu atulinde..
 
Pole sana Kaka binafsi nimeguswa mno maana nayajua maisha ya kuishi Kama chokoraa huna wazaz Wala walezi ukiwa binti mdogo kwakweli simlaumu kupata mimba hizo ni matatizo mazito mno

Nilianza maisha ya kujitegemea kila kitu nikiwa na miaka 18 Ila msoto wake sitamani kukumbuka kuishi bila kula hata siku tatu ilikua kawaida kwangu, kufukuzwa Kodi etc all in all bado napumua[emoji120]

Pambana Kaka msaidie mdogo wako kwa namna yoyote
 
Mkuu emb mcheki MalisaGJ huko Facebook au Insta
 
Wengi tumepitia maisha hayo machozi yamejaa kwenye vifua vyetu na hatukua na pa kuegemea dah nakumbuka mbali Sana nilipoanza kujitegemea nikiwa na miaka 12 ndani ya jiji la dar lakini mpka sasa nimesonga ni maisha ambayo watoto wengi wa kimasikini tunapitia kwa sababu unabeba majukumu ukiwa na umri mdogo kikubwa ni kupambana tu Mungu atakusimamia
 
12?oh no!...dah...aise
 
Siku njema zijapopita usihuzunike bali ufurahi kwa kuwa zilikuwako.
 
Maisha ni safari. Tutafika tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…