Messi ni mchezaji bora hilo halipingiki.Lakini MVP wa World Cup hii iliyoisha juzi alipaswa kuwa Mbape...
Hayo mambo ya GOAT mimi huwa sioni mantiki yake kwa sababu every player plays in his time and football rules,styles,techniques,tactics keeps on changing everyday..Ukinambia mchezahi bora kuanzia 2010 hadi sasa nitaona sawa....
Lakini kumuita yeyote ni greatest of ALL TIME kwangu haikubaliki kwakuwa vipimo tunavyotumia kupima vinabadilika kila era.Kuna magoli yalifungwa zamani ambayo kwa sheria za sasa ni Off side!Kuna penati hazikutolewa ambazo kwa sasa ni penati.Kuna VAR sasa na zamani haikuwepo.Kuna kulimit uwezo au uchezaji wa mchezaji kusuit style ya timu inavyocheza.
Mpira sasa ni wa maelekezo zaidi kuliko zamani ambapo wachezaji walikuwa wakicheza kwa uwezo wao na kujiachia kwa uhuru.Mtu kama Okocha labda asingepata namba kwenye mpira wa sasa (robotic era)na ni bonge la mchezaji kwa kipindi chake.
Kwahiyo kujumlisha era zote za football na kumpata mmoja ambaye ni outstanding kwa mtazamo wangu sio idea sahihi.