Andaa Business Plan inayolenga soko zaidi, mengine baadaye

Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
1,414
Reaction score
2,181
Chuo tukisoma business administration , unapewa format ya kuandaa business plan ambayo robo ya muongozo unajikuta unashindwa kundana nao.
Lakini ukiingia sasa elimu ya kimtaani taani (iite kitaalogy) unagundua lngo kuu la Businss Plan ni marketing.
Wiki hii kuna familia walinitafuta wanataka wafanye biashara ya kuuza mbuzi kwa viwanda vya nyama. Niwaandalie Business Plan.
Bada ya kufanya makubaliano , mipango yangu yoote nikaelekza kwenye soko.
Kwa kuanzia nikasign in app yangu maalum ya kujua ukubwa wa soko kwa kila bidhaa.Nyama ya mbuzi Tanzania tunauza zaidi nchi zifuatazo:
1730052186225.png

Nikaenda kuzihakiki wazara husika ,nikakuta ongzko la Comoro. tukaongeza.

2. Tukaangalia ukubwa soko (kiwango cha bidhaa na mapato)

1730056419158.png

Tukahakiki na wizara husika, tukakuta ni kweli soko kubwa mnoo
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema nyama ya mbuzi inaongoza katika mauzo nje ya nchi na inachangia asilimia 70.1 ya mauzo yote.

Amebainisha hayo kwenye makabidhiano ya Kituo Atamizi cha Vijana cha ufugaji mbuzi kibiashara kilichojengwa na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), kwa ufadhili wa Serikali ya Denmark kupitia Mfuko Binafsi wa Kusaidia Wakulima (PASS TRUST).

Amesema mauzo ya nyama nje ya nchi yameendelea kuongezeka hadi kufikia Aprili, 2024 tani 11,682.3 (zikiwamo tani 870.7 za nyama ya ngómbe, tani 8,059.38 za nyama ya mbuzi, tani 2,715.5 za nyama ya kondoo, tani 27.5 za nyama ya kuku na tani 9.3 za nyama ya nguruwe) zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 50.3 zilikuwa zimeuzwa nje ya nchi.

3.Nani partner wanaotambulika na serikali ili tufanye nao kazi?

Tukawa tumepata viwanda 10.Hapo tukachagua vya jirani zaidi viwanda viwili.Baada ya muda tukawa tumpata taarifa za uzito wanaohitaji wa mbuzi kuanzia kilo zipi, bei kwa kilo na idadi ya chini ya mbuzi wanaonunua kwa muuzaji mmoja. Kapokea Business Plan, ndani ya wiki kaingiza shilingi ya kwanza ya Mauzo.

MUHIMU: Habari za idadi ya wafanyakazi, uanze na mtaji gani, uwe na eno la ukubwa gani ,n.k Ni mambo yanayokuja baada ya kujua taarifa za soko ,kisha unajiwekea malengo kulingana na misuli ya mtaji uloandaa.Soko kubwa ,unaandaa taarifa za washindani wako za nini?.
 
Chuo tukisoma business administration , unapewa format ya kuandaa business plan ambayo robo ya muongozo unajikuta unashindwa kundana nao.
Lakini ukiingia sasa elimu ya kimtaani taani (iite kitaalogy) unagundua lngo kuu la Businss Plan ni marketing.
Wiki hii kuna familia walinitafuta wanataka wafanye biashara ya kuuza mbuzi kwa viwanda vya nyama. Niwaandalie Business Plan.
Bada ya kufanya makubaliano , mipango yangu yoote nikaelekza kwenye soko.
Kwa kuanzia nikasign in app yangu maalum ya kujua ukubwa wa soko kwa kila bidhaa.Nyama ya mbuzi Tanzania tunauza zaidi nchi zifuatazo:
View attachment 3136674

Nikaenda kuzihakiki wazara husika ,nikakuta ongzko la Comoro. tukaongeza.

2. Tukaangalia ukubwa soko (kiwango cha bidhaa na mapato)

View attachment 3136746

Tukahakiki na wizara husika, tukakuta ni kweli soko kubwa mnoo
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema nyama ya mbuzi inaongoza katika mauzo nje ya nchi na inachangia asilimia 70.1 ya mauzo yote.

Amebainisha hayo kwenye makabidhiano ya Kituo Atamizi cha Vijana cha ufugaji mbuzi kibiashara kilichojengwa na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), kwa ufadhili wa Serikali ya Denmark kupitia Mfuko Binafsi wa Kusaidia Wakulima (PASS TRUST).

Amesema mauzo ya nyama nje ya nchi yameendelea kuongezeka hadi kufikia Aprili, 2024 tani 11,682.3 (zikiwamo tani 870.7 za nyama ya ngómbe, tani 8,059.38 za nyama ya mbuzi, tani 2,715.5 za nyama ya kondoo, tani 27.5 za nyama ya kuku na tani 9.3 za nyama ya nguruwe) zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 50.3 zilikuwa zimeuzwa nje ya nchi.

3.Nani partner wanaotambulika na serikali ili tufanye nao kazi?

Tukawa tumepata viwanda 10.Hapo tukachagua vya jirani zaidi viwanda viwili.Na kukamilisha biashara.

MUHIMU: Habari za idadi ya wafanyakazi, uanze na mtaji gani, uwe na eno la ukubwa gani ,n.k Ni mambo yanayokuja baada ya kujua taarifa za soko ,kisha unajiwekea malengo kulingana na misuli ya mtaji uloandaa.
Hili tangazo limekaa kitaalam sana
 
Back
Top Bottom