Sababu kubwa ya kutolewa basilo matei ni kwamba alikuwa kamanda muelewa sana.. Na pia alikuwa hatoi amri za kutishia wala kuonea... Wakati wa uchaguzi aliambiwa awatawanye watu pale manispaa yeye akasema kuwa walioko pale ni wanachama wa chadema na siyo ccm hivyo wapewe matokeo yao ili watawanyike.. Na walipofanya hivyo tu.. Wanachadema walitawanyika kwa amani sana.
Sasa basilo akaonekana kuwa ni kibaraka ya chadema wamamhamisha bila sababu ya msingi na kumleta huyu andengenya.. Sasa jamaa amekuja kuungana na zuberi basi ni balaa tu.. Asubuhi walileta magari kama kumi ya polisi kutoka moshi hayakutosha wakaleta mengine mchana kuongeza nguvu.
Wametumia mabomu kupiga hata sehemu zisizofaa mfano pale mnara wa mwenge karibu na hospitali ya kaloleni, pale kwenye jengo la salimu ally karibu na hospotali ya st. Thomas. Haya mabomu yalileta shida sana kwenye hizi hospitali kwa wagonjwa ambao wengine walipata mishtuko hata kuzimia.
Walikuwa wanapiga watu na mipini ya majembe, mateke na risasi za moto.. Kwa nini yote hii?? Ccm hawawezi kufanya mikutano tena arusha kwani umeona watu walichofanya walienda kuvunja vioo vya jengo la ccm mkoa.. Hii yote inaongeza chuki kwenye jamii.
Sasa hii inamaanisha nini? Andengenye lazima ashtakiwe na igp.. Waziri nahodha awajibishwe.