Andika haya maneno kwa Kiswahili

sio ndege ulaya, ni ndege pori.
 
mwanga lutila, hili swali limekuwa likijitokeza mara kwa mara humu ndani na nimekuwa nikilitolea majibu...najibu kwa mara ya mwisho:

NI NDEGE, SIYO NYUNI...

Nimecheka sana na majibu ya waswahili wasiopenda kiswahili na wasio tayari kujifunza. Kwa kweli ni changamoto sana kuona mtu anakuwa mwepesi sana kutafuta kujua lugha ya kigeni ilhali yake inamsumbua.
Jibu sahihi ni "siyo ndege ni nyuni"

Nyuni ni nini mmeniacha hpo
. yahoo

nyuni nm [a-/wa-] bird.

ndege1 nm [a-/wa-] bird.

ndege2 nm [i-/zi-] aeroplane.
.

 
Kwa hiyo nikisema ndege wanakula mtama nakua nimekosea

Ndege mwenye uhai pia huitwa NYUNI....NYUNI huyo huyo kwa lugha nyingine huitwa NDEGE....
Ili kuiweka sawa sentensi hiyo isiwe na utata tunatumi neno lingine...Mfano:
Chombo chenye magurudumu kinachokokotwa na ng'ombe huitwa gari sawa na chombo kinachotembeshwa na injini...
 
Sio denge chombo cha usafiri,ni denge mnyama!!
 
kiswahili kinajitosheleza sawa na mazingira yetu kuna baadhi ya maneno yanakua hayana kiswahili chake kwasababu ya uvumbuzi huo haukutokea katika mazingira yetu na sio kweli kwamba kiswahili hakijitoshelezi....mazingira ndiyo huathiri kuwepo au kutokuwepo kwa tafsiri ya msamiati kutoka lugha chanzi kwenda lugha lengwa mfano mlenda kwa kingereza ni nini, mkunungu je......je kwa kukosa maneno haya kwa kingereza tunaweza tuka sema kingereza hakijitoshelezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…