Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,982
- 51,157
“MSIBA WA LUKUVI: JE, KILA MWENYE FAIDA NI MWENYE FURAHA?”
Na Emily Mwakilembe
Mwambie Mwenezi wa CCM Kihongosi kuna msemo unaoitwa “kufaa kufaana.” Ukielewa falsafa hii, utaona kuwa katika kila tukio hata la huzuni kuna upande mwingine unaonufaika kimyakimya.
Nenda kituo cha polisi kilicho karibu nawe, kawaripoti hawa “wanaofurahia” msiba wa William Lukuvi, kwa sababu kwa mantiki hiyo, hawa ndio wamepata fursa kupitia kifo chake:
1: Aliyeuza jeneza ameongeza kipato, ada za watoto zinalipika.
2: Aliyekodisha hema (tenti) familia yake imepata mkate wa siku hiyo.
3: Aliyefunga mfumo wa sauti kazi imepatikana, kipato kimeingia.
4: Kampuni za catering & service – vijana wamepata ajira, kodi imelipwa.
5: Wabebaji wa viti, hema, na vifaa madereva na wasaidizi wamepata kazi.
6: Mafundi wa kaburi jasho lao limezalisha kipato.
7: Maduka ya vifaa vya ujenzi (hardware) mauzo yameongezeka.
8: Mabasi ya kusafirisha waombolezaji kampuni zimepata mapato.
9: Wauzaji wa vyakula na vinywaji biashara imechangamka.
10: Waliokuwa na migogoro na marehemu mioyoni mwao kuna afueni ya kimya kimya.
11: Washindani wa kisiasa Jimboni wanaona mlango umefunguka, japo hawatasema hadharani.
12: Wanaotamani nafasi za uwaziri wanaiona kama fursa ya kupanda ngazi.
13: MC wa shughuli amelipwa, familia yake imenufaika.
14: Wamiliki wa Nyumba za wageni
15: Walioumia katika matukio ya nyuma Mo29 bila kufarijiwa wanaona tofauti ya namna huruma inavyotolewa.
Hii ndiyo maana halisi ya “kufaa kufaana.”
Sio kila anayenufaika na tukio la msiba anafurahia kifo wengine wanapambana kuishi kupitia mazingira hayo hayo ya majonzi.
Tusikimbilie kuhukumu mioyo ya watu kwa juu juu. Maisha yana mizunguko yake leo ni majonzi kwa mmoja, kesho ni tegemeo kwa mwingine. Huu ndio ukweli mchungu wa jamii yetu.
Badala ya kulaumu nani anafaidika au Kufurahia kifo cha Kiongozi, tujiulize je, tunaijenga jamii inayojali wote wakati wa furaha na wakati wa huzuni? Maana mwisho wa yote, sio nani amepata, bali nani amebaki na utu wake. Uhuru, Haki, Upendo na Wema ni Jumba bovu la Amani linalobomoka taratibu likiwa limebaki upande wa Magharibi tu!! Liue jamii inayo lizunguka.