SoC02 Andiko la mabadiliko chanya katika jamii kwenye nyanja mbalimbali zikiwemo za elimu, uchumi, kilimo,utawala, afya, sayansi na teknolojia

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Aug 4, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Mabadiliko chanya katika Elimu; Kumekuwa na fikra hasi katika jamii zetu kwenye swala la elimu vijana wengi fikra zao kwa sasa katika elimu zinatokana na ukosefu wa ajira ama ajira zisizotosheleza idadi ya watu waliopo, Hivyo basi vijana wengi wanaona hakuna umuhimu wa kupata elimu ikiwa ajira hamna na hiyo imetokana na mfumo wetu wa elimu Hivyo basi tunahitaji mabadiliko katika nyanja tofauti kwenye elimu katika jamii zetu Kwa ujumla.

Hivyo basi kuna umuhimu wa kuanzisha masomo ya Ujasiriamali Katika ngazi tofauti kwenye elimu yetu katika jamii ambayo itamsaidia kijana ambaye akimaliza masomo yake ya elimu ya juu ajihusishe na maswala ya Ujasiriamali ambayo yatamsaidia kufanya Biashara mbalimbali zitakazo muingizia kipato ambacho kitamsaidia kujikimu katika maisha yake.

Pia kuna uhitaji wa elimu yetu kubadili mifumo yake yaani iweze kumuandaa mwanafunzi pale anapo hitimu elimu yake ya juu awe ana uzoefu wa kutosha wa kuifanyia kaZi elimu aliopata mfano mzuri ni kama serikali kuingia mikataba na makampuni tofauti tofauti Ili waweze kuwapa hawa wanafunzi uzoefu kipindi wanasoma elimu yao ya juu Ili wakija kuhitimu waweze kuwa na uzoefu wa kutosha ambao itamsaidia kufanya kazi kwa ufanisi.

Hata hivyo serikali yetu hivi karibu imeweza kuleta mabadiliko kwenye swala zima la elimu ambapo imeweza kutoa elimu bure mpaka kidato cha sita na hii itawezesha watu katika jamii kupata haki ya ya msingi ambayo ni elimu kwa ujumla.

Mabadiliko chanya kwenye nyanja ya Uchumi ; Tunahitaji mabadiliko makubwa katika jamii zetu kwenye swala zima la kiuchumi Hivyo basi inabidi uchumi uanzie kwa raia na pia uje kufika mpaka katika ngazi ya Taifa yaani inabidi tukuze uchumi wa mtu mmoja mmoja hiyo itasaidia hata kufanya pato la taifa kuongezeka na hatimaye kufikia uchumii wa juu.

Kuna vitu ambavyo vinaweza kusaidia jamii zetu katika swala zima la kukuza uchumi kwa mtu mmoja mmoja kama tunavyojua swala zima la ajira limekua ni tatizo kwa taifa letu na Hivyo kuwaweka vijana , wengi kwenye jamii zetu kwenye sintofahamu ya kukosa ajira licha ya kwamba wana kila sifa ya kupata ajira sehemu yeyote ile.

Hivyo basi kuna haja ya kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja katika jamii zetu Kwa namna mbalimbali kama vile kuwahimiza vijana kujihusisha na Ujasiriamali na kuanzisha Biashara mbalimbali ambazo zitawasaidia kupata kipato ambacho kitamsaidia kijana huyo kujikimu kimaisha, pia kuwawezesha vijana Kwa kuwapa mikopo ambayo itawasaidia kujihusisha na maswala ya Ujasiriamali hata hivyo kuondoa ugumu ambao wanaupata katika Biashara ambazo watajihusisha nazo vijana hawa katika jamii zetu.

Ili kuweza kuleta mabadiliko chanaya kwenye uchumi wetu pia tunahitaji kuboresha miundombinu yetu maeneo tofauti katika Nchi yetu haswa maeneo ya vijijini hii itawezesha sehemu hizo kufikika kwa urahisi pia itasaidia katika usafirishaji wa bidhaa mbalimbali kutoka mjini kwenda vijijini na hata hivyo kiwezesha Biashara nyingi kufanyika kwa haraka na kwa wakati.

Mabadiliko chanya kwenye nyanja ya Kilimo; imewahi kuelezwa kuwa Kilimo ni uti wa mgongo katika uchumi wa Nchi yetu ya Tanzania. Hivyo basi kuna haja ya kuleta mabadiliko chanaya katika Kilimo chetu cha Tanzania ikiwemo kutoa msaada Kwa wakulima wa vifaa vya kisasa ambavyo vitasaidia kufanya uzalishaji kwa wingi ndani ya mwaka mfano matrekta,mbolea za kisasa,mashine za kuvunia japo ni gharama lakini kuna haja kubwa ya kuleta mabadiliko hayo katika jamii zetu Ili tuweze kukuza uchumi wetu. Wakulima wengi wanakosa mtaji ambao itawasaidia kufanya uzalishaji mkubwa wa chakula na malighafi Hivyo kuna haja kubwa ya kuwapa mikopo ambayo itakuwa ina riba nafuu kwao hii itaweza kuwawezesha kwenye shughuli zao za kilimo.

Kama tunavyojua Kilimo kina umuhimu mkubwa kwa taifa letu ambapo husaidia kupata chakula mfano mshindi husaidia Kwa upatikanaji wa chakula kama ugali Hivyo basi kuna haja ya kuleta mabadiliko ambayo nimekwisha yataja hapo juu Ili tuweze kusonga mbele na kupiga hatua kubwa sana katika Kilimo.

Mabadiliko mengine yanayohitajika ni kama kuwapa elimu wakulima namna gani ya kujihusisha na Kilimo cha umwagiliaji ambacho kitamsaidia mkulima kuzalisha kipindi ambacho upatikanaji wa mvua ni mchache haswa kipindi cha kiangazi mvua huwa ni chache Hivyo basi tukitoa elimu pamoja na kuwapa vifaa wakulima itaweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye Kilimo.

Mabadiliko chanya kwenye nyanja ya Afya; Kwanza kabisa kuna haja ya serikali kuleta mpango mkakati ambao utamuwezesha kila mtanzania awe kupata bima ya Afya kwa gharama rafiki. waTanzania wengi huwa wanashindwa kumudu gharama za matibabu haswa Kwa wale wenye magonjwa sugu kama magonjwa ya moyo ,saratani n.k hivyo basi kama kukiwa na haja ya kila mtanzania kupata bima ya Afya ambayo itakuwa ya gharama rafiki kwa jamii zetu hii itawezesha watu wenye kipato cha chini kutibiwa kwa gharama nafuu. Pia kuna umuhimu wa ujenzi wa vituo vya Afya vingi haswa maeneo ya vijijini ambapo watu huenda wakawa wanasafiri umbali mrefu Ili kusaka matibabu. Hata hivyo kuangalia kwa ukaribu yale makundi maalum haswa wazee kama kuna uwezekano wawe wanapewa matibabu bila malipo Ili kuweza kuwapa uangalizi wazee katika jamii zetu.

Mabadiliko chanya kwenye nyanja ya Utawala; Katika nyanja hii ya utawala tunahitaji kupata viongozi bora na sio bora viongozi yaani viongozi ambao watakuwa tayari kutetea haki za watu wa jamii husika na maslai mapama ya Taifa letu. Katika jamii zetu zimekuwa nyuma kimaendeleo kwa sababu tumekosa viongozi mbao wana uchungu na taifa letu Hivyo basi ni jukumu la wananchi kipindi cha uchaguzi kufanya chaguzi sahihi ambazo zitaleta maendeleo katika taifa letu kwenye maswala ya utawala.Hata Hivyo Ili kuleta mabadiliko chanaya kwenye utawala inabidi kutokomeza janga la rushwa kama sio kupunguza Ili kuweza kuleta maendeleo katika jamii zetu kumekuwa na viongozi wengi katika jamii zetu ambao wanajihusisha na rushwa na kufanya ubadhilifu wa mali za umma vitendo hivi kama ndo vinaleta nyuma maendeleo hivyo tukivikomesha tutaweza kuongeza ufanisi katika nyanja hii ya utawala.

Mabadiliko chanya kwenye nyanja ya sayansi na teknolojia; Ili tuweze kuleta mabadiliko katika maswala ya sayansi na teknolojia inabidi tuwape ushirikiano wale watu ambao wanakuja na uvumbuzi wa vitu mbalimbali ambavyo vitaweza kukuza sayansi na teknolojia kwa sababu hawa watu kama wakipewa elimu zaidi na kuwaendeleza Ili waweze kuja na vitu vipya zaidi. Mfano mzuri ni Ndugu Masoud kipanya ambaye aliweza kugundua gari lake lakini mpaka leo hajaweza kupewa ushirikiano Hivyo basi Ili tuweze kukuza kiwango cha sayansi na teknolojia atika jamii na Nchi kwa ujumla inabidi tuweze uwapa ushirikiano watu kama hawa.
 
Upvote 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…