Andiko latimia, hatimae 93.7 FM yaenda kufanya mapinduzi masikioni mwa Watanzania

shifta

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
474
Reaction score
192
Miezi ikapita, mawiki yakasonga hatimae siku, masaa na dakika zake zikapotea na sasa EFM inayopatikana katika masafa ya 93.7 imesikika hewani kwa majaribio kwa mara ya kwanza.

Redio hii iliobeba watangazaji mahiri, waandaaji wa vipindi wenye umakini, ma DJ wanao sadikiwa kuwa walishushwa kwa ajili ya kazi hii, uongozi thabiti na yenye usikivu mujarab, habari zake zilianza kupenya kwenye masikio ya washashi mwishoni mwa mwaka jana na kupelekea wamiliki na wadau wa redio nyengine kukosa usingizi na hata siku wakiupata basi huweweseka usiku na kupiga mayowe ama kujikuta wakikosa hata nguvu ya kuzuia haja ndogo kutoka.

Redio hii itadili kwa asilimia 85 na burudani...na watakaoongoza balaa hilo ni watu wenye kulijuwa game kwa kipindi kirefu saana na burudani iliolengwa hapa hakika ndio mwiba mchungu utaowatesa weengi waliowanyonya na kuwanyanyasa wasanii kwa miongo kadhaa sasa.

Nanga ndio imeshainuka, Unyonyaji ndio umekwisha, Wanyonge mtafarijika, Game sasa litabadilika, Walio Vilaza wataaibika, makini watasikika, Sina imani nina hakika.

Ndio maana ninaandika.
 
Asante manager wa radio tumekusikia

hah hah hah asante pia ewe msikilizaji mtarajiwa...

All in All goma lipo hewani kwa majaribio.
Waliopo Dar ndio wanahusishwa zaidi...
 
Tufafanulie, wamiliki ni nani, maelezo yako nusu nusu!
 
hah hah hah asante pia ewe msikilizaji mtarajiwa...

All in All goma lipo hewani kwa majaribio.
Waliopo Dar ndio wanahusishwa zaidi...

Jamani hiyo Dar mmezidi kuipendelea kila kitu dar makao makuu dar ...eh embu jaribuni kubalika jaman kha!
 
Daaaah!!!!nimeikubali inanipa vitu Roho inapenda aiseeee!!!mpo vizuri!!!!!!!msije mkaharibu jmn!!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Miezi ikapita, mawiki yakasonga hatimae siku, masaa na dakika zake zikapotea na sasa EFM inayopatikana katika masafa ya 93.7 imesikika hewani kwa majaribio kwa mara ya kwanza.

Redio hii iliobeba watangazaji mahiri, waandaaji wa vipindi wenye umakini, ma DJ wanao sadikiwa kuwa walishushwa kwa ajili ya kazi hii, uongozi thabiti na yenye usikivu mujarab, habari zake zilianza kupenya kwenye masikio ya washashi mwishoni mwa mwaka jana na kupelekea wamiliki na wadau wa redio nyengine kukosa usingizi na hata siku wakiupata basi huweweseka usiku na kupiga mayowe ama kujikuta wakikosa hata nguvu ya kuzuia haja ndogo kutoka.

Redio hii itadili kwa asilimia 85 na burudani...na watakaoongoza balaa hilo ni watu wenye kulijuwa game kwa kipindi kirefu saana na burudani iliolengwa hapa hakika ndio mwiba mchungu utaowatesa weengi waliowanyonya na kuwanyanyasa wasanii kwa miongo kadhaa sasa.

Nanga ndio imeshainuka, Unyonyaji ndio umekwisha, Wanyonge mtafarijika, Game sasa litabadilika, Walio Vilaza wataaibika, makini watasikika, Sina imani nina hakika.

Ndio maana ninaandika.

EFM kirefu chake ni nini? Na pia wamiliki ni akina nani? Hadi sasa mtoa mada hajatoa ufafanuzi. Ukianzisha uzi uwe umekamilika!
 
Mtoa mada unakimbilia wapi toa maelezo yaliyokamilika,nani mmiliki makao makuu yanapatikana wapi na maelezo mengine ya muhimu otherwise we all knw 93.7 itakuwa kiburdani zaidi na itakuwa inashika dar.
 
entertainment FM...
Hilo kingine nakwenda kumjibu mwenzio...
 
Mtoa mada unakimbilia wapi toa maelezo yaliyokamilika,nani mmiliki makao makuu yanapatikana wapi na maelezo mengine ya muhimu otherwise we all knw 93.7 itakuwa kiburdani zaidi na itakuwa inashika dar.

inapatikana pande za Kawe...
Maelezo mengine ni kuwa imeanza kupenya na kuteka masikio ya baadhi ya wakusudiwa...
Ukisikiliza playlst yao wallah hutotamani kusikiliza makorokocho ya hao ulowazoea
 
Back
Top Bottom