Andres Iniesta vs Xavi Hernandez

Kitambi chakufutia tachi

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2019
Posts
1,063
Reaction score
2,566
Amani iwe juu yenu wanajamvi.

Binafsi mimi ni shabiki wa Man United na Real Madrid lakini kiukweli sijawahi kushuhudia pacha bora zaidi katika eneo La katikati kama pacha ya Iniesta na Xavi. Mafundi hawa walishirikiana vema na kufanya mambo makubwa wakiwa ndani ya uzi wa Blaugrana mpaka wakamtetemesha Sir Elexander Chapman Ferguson pale Wembley.

Kutokana na kushirikiana na ubora wao imefikia hatua hauwezi kuyataja mafanikio au Ubora wa mmoja kati yao bila kumtaja mwingine yani ukizungumziwa ubora wa Iniesta lazima Xavi atajwe au yakizungumziwa mafanikio ya Xavi lazima Iniesta atajwe.

Lakini pamoja na yote ushawahi kujiuliza ni nani alikuwa bora zaidi kumzidi mwenzie? Kanakwamba ukipewa fedha umsajili mmoja kati yao ungelimchukua yeye?

Pamoja na kushirikiana vema na kucheza kwa mahaba na kujituma wakiwa pamoja ndani ya uzi wa Barcelona na timu ya taifa Spain unafikiri ni nani alikuwa bora zaidi kati ya Xavi na Iniesta?

Karibuni tujadili

 
Andres Iniesta anaweza kucheza eneo analocheza Xavi Hernandez japokuwa si kwa kiwango cha muhusika (namba 8) lakini bwana xavi hernandez hawezi kucheza nafasi ya andres iniesta (namba 10, 11) hata kwa nusu saa.

Ni rahisi kumpata mrithi wa xavi hata mitaa ya buza kuliko kumpata mrithi wa iniesta kwenye sayari hii ya dunia, hiyo kazi imemshinda isco alcaron, phelippe coutinho na wengineo watashindwa kurithi nafasi ya ball dancer
His silky dribbling, close control and unimaginable vision makes him the embodiment of the modern playmaker.

Udhaifu wa xavi hernandez hawezi dribbling ila ni master wa position (anaweza kuiharibu defence ya timu pinzani bila ya kusogea hatua tano mbele), ndio maana alikuwa ni bingwa wa kugusa mpira mara nyingi ndani ya uwanja

Ni sahihi kumfananisha xavi hernandez na hawa wafuatao

Xavi Hernandez vs Cesc Fabregas
Xavi Hernandez vs Andrea Pirlo
Xavi Hernandez vs Paul Scholes
Xavi Hernandez vs Sneijder
Xavi Hernandez vs Sebastian Veron

Juan Roman Riquelme: "I watch Iniesta and realize that even at my age I could be learning new things.
 
Ngumu kuwafananisha hawa viumbe wawili, ni wachezaji wawili tofauti kwa aina yao ya uchezaji iniesta ni dribbler mmoja hatari, xavi dribbling kwake ni adhabu kubwa, ni kwangu ni rahisi kwa iniesta kuifanya kazi ya xavi ila ngumu Xavi kuifanya kazi ya Iniesta.

Sisemi xavi alikuwa mbovu la hasha

Na kama tukipima kwa umuhimu kila mmoja alikuwa muhimu kwa mwenzie, kukosekana mmoja, timu ilikuwa inakosa balance uwanjani, xavi anamrahisishia kazi iniesta, iniesta analainisha kazi ya xavi.

Moja kati ya combination bora niliyopata kuishuhudia.

Iniesta jamii ya kina seedorf Wakati Xavi ni jamii ya kina Francesco Fabregas.

Nikiambiwa niwa’rate kwangu woote watakula 9/10 kwa 9/10 kwa ubora wao uwanjani.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Xavi macho ya kinyonga ni noma sana alimpigia assist messi ya kisigino sintoishau Yule jamaaa alikuwepo anaujua mpira na Ethics zake.

Iniesta dah! ukisikia ball dancer ndiyo huyu kumpokonya mpira mpaka mkabaji uwe na nidhamu flani ivi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iniesta na Xavi ni best duo of our generation (modern football).

Nisiandike mengi, mpira walioucheza 2008 - 2012 sina uhakika kama nitauona tena katika maisha yajayo.
Hiyo 2008 mzee kuna Busquet, Xavii, niesta, Gaucho na Mess
Formula ni 3-1-2-3-1
Barca hiyo
Unaenda Spain unakutana na
Xavii, Busquet, Iniesta, Alonso na Secs fabrigas
Hadi wapinzani tulihamia aisee
 
Iniesta alikua Mwehu. Ndio Mwehu kama Ronaldinho, carlos Alberto (porto) mwehu kama riquelme na kichaa kama Haruna Moshi...Boban! Xavi alikua wa kawaida hata edu anamkata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja na mimi nichangie, hawa majamaa nimewatazama sana, saana tu.

Ni watu wawili tofauti.

Xavi Hernandez ni mchezaji wa kawaida sana, naweza nikasema hata Ozil akitulia uwanjani anampoteza Xavi, kitu pekee kilichombeba Xavi ni ile falsafa ya Barca (Tiki Taka), so Xavi ni mchezaji mzuri saana endapo timu ikawa na Falsafa hii.

Xavi Timu kama Dortumund, Atletico, Real Madrid, Ajax, Liver n.k hawezi kuchukua namba.

Iniesta hii ni bakora nyingine, wengi mmeshamwelezea, sina la kuongeza wala kupunguza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hamna cha kuongeza Xavi ni fundi lakini iniesta ni habari nyingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kusema ukweli napenda mpira lakini hakuna kipindi nilikua napenda mpira kama 2008- 2015 kwa sababu ya Iniesta,Xavi,Messi n Bosquet.Hakuna mechi niliwahi kukosa za Barca jwa kipindi hiko nilisikia raha kuwaangalia.

Lakini tangu inesta na Xavi walivyoondoka Barca taratibu mapenzi yalianza kupungua ya kuangalia mpira ukweli barcelona imekosa huduma ya hawa watu na wanahangaika sana kwa miaka karibu mitano wameshindwa.

Iniesta alikua anaweza kupenya,kwenye msitu wa mabeki,kucheza na mpira ,kutengeneza kaunta ataki... Hata kufunga katika nyakati muhimu wakati wote wamezidiwa hakika alikua fundi sana.

Xavi alikua hana uwezo wa kukimbia na kudrible ila yule mwamba alikua na pasi zenye macho na kali sana hasa za kupenyeza,pia alikua na uwezo mkubwa wa kutuliza timu katikati wakati wa kushambulia na nidhamu ilikua juu sana katikati kupitia yeye.

Iniesta 9/10 na 9/10 .....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tukianza kuongelea hawa wawili hakuna linalppingika kwamba ile dream team alietaka johan cryuff ilitimia zaidi na vijana hawa wawilii wakiongozwa na Pep
Lakini tukisema iniesta ni bora kuliko Xavi tutadanganyana Xavi alikua ndio mhimili mkuu na roho ya timu ukizingatia tik tak iliwafanya wamiliki mpira zaidi kuliko kukaba Xavi ndio alikua mtu kwenye kile kikosi
Xavi alikua ana jicho kali sana
Xavi alikua anajua muda gani wa kuachia mpira mguuni mwake
Xavi alijua muda gani wa kuenda kuchukua mpira eneo husika
Xavi aliwacontrol kila mmoja kwenye timu iniesta alikuja kuwa bora kwa sababu alikaa na mtu bora na kurithi vingi kutoka kwake lakini the midfield maestro alikua ni Xavi hernandez


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…