Kitambi chakufutia tachi
JF-Expert Member
- Jun 16, 2019
- 1,063
- 2,566
Amani iwe juu yenu wanajamvi.
Binafsi mimi ni shabiki wa Man United na Real Madrid lakini kiukweli sijawahi kushuhudia pacha bora zaidi katika eneo La katikati kama pacha ya Iniesta na Xavi. Mafundi hawa walishirikiana vema na kufanya mambo makubwa wakiwa ndani ya uzi wa Blaugrana mpaka wakamtetemesha Sir Elexander Chapman Ferguson pale Wembley.
Kutokana na kushirikiana na ubora wao imefikia hatua hauwezi kuyataja mafanikio au Ubora wa mmoja kati yao bila kumtaja mwingine yani ukizungumziwa ubora wa Iniesta lazima Xavi atajwe au yakizungumziwa mafanikio ya Xavi lazima Iniesta atajwe.
Lakini pamoja na yote ushawahi kujiuliza ni nani alikuwa bora zaidi kumzidi mwenzie? Kanakwamba ukipewa fedha umsajili mmoja kati yao ungelimchukua yeye?
Pamoja na kushirikiana vema na kucheza kwa mahaba na kujituma wakiwa pamoja ndani ya uzi wa Barcelona na timu ya taifa Spain unafikiri ni nani alikuwa bora zaidi kati ya Xavi na Iniesta?
Karibuni tujadili