Andrew Kisaka, amesema Mamlaka hiyo itawachukulia hatua baadhi ya Watangazaji wanaosoma magazeti kwa mbwembwe

Andrew Kisaka, amesema Mamlaka hiyo itawachukulia hatua baadhi ya Watangazaji wanaosoma magazeti kwa mbwembwe

Meneja wa Huduma za Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Andrew Kisaka, amesema Mamlaka hiyo itawachukulia hatua baadhi ya Watangazaji wanaosoma magazeti kwa mbwembwe huku wakiongezea baadhi ya vitu visivyotakiwa wakati wa usomaji.

Chanzo: millardayo

GENTAMYCINE nawapongeza sana kwa hatua hii japo pia mmechelewa sana kuitoa kutokana na Upuuzi huu mkubwa uliokuwepo.

Hata hivyo kuonyesha kuwa TCRA hamheshimiki na Mliowaonya ( yaani ni Nyoka wa Kibisa ) ni kwamba Asubuhi hii hii katika Kipindi cha Joto la Asubuhi cha EFM Radio Mtangazaji mwenye Upuuzi huu mlioukataza Masanja Mkandamizaji ( Emanuel Mgaya ) kaendelea na Utaratibu huu japo Kiuwoga Uwoga.
Masanja si chawa!
Watakuwa wanamlia mingo Gerald
 
huyo afisa wa tcra kasoma wapi masuala ya habari? Hebu asikwamishe ladha ya usikilizaji wa kusoma magazeti. Mambo ya habari zaidi hutawaliwa na ubunifu na utashi wa mtu katika kufanya presentation ya taarifa. Huyo afisa anakurupuka tu
Hayo muwe mnafanyia chumbani si kwenye vyombo vya habari. Tatizo la nchi hii vilaza ni wengi kuliko sisi. Tupo wachache sana. Sometime mnataka sasa mtuzidi hata kwenye mambo ya maana.
 
Mahubiri yenyewe tu ukileta u serious waumini wanasinzia na kulala usingizi hutasikilizwa lazima ulete mbwembwe waumini wawe active kukusikiliza. Ukiwa mwalimu kama huna mbwembwe somo halitaeleweka utaishia kunong'ona na ubao na kuacha wanafunzi hoi hawaelewi ulichofundisha. Hotuba zenye mbwmbwe ndizo husikilizwa zaidi, wajumbe hawasinzii.
Wachugaji siku izi utaskia "shika jirani zako watano mikono waambie your beautifull ata kama ni wanaume" ilimradi waumini wasiuchape.
 
Mahubiri yenyewe tu ukileta u serious waumini wanasinzia na kulala usingizi hutasikilizwa lazima ulete mbwembwe waumini wawe active kukusikiliza. Ukiwa mwalimu kama huna mbwembwe somo halitaeleweka utaishia kunong'ona na ubao na kuacha wanafunzi hoi hawaelewi ulichofundisha. Hotuba zenye mbwmbwe ndizo husikilizwa zaidi, wajumbe hawasinzii.
Kwa sisi watu smart tunataka content siyo mbwembwe. Hizo mbwembwe wawe wanafanyiwa vilaza. Muda wenyewe upo wapi kuanza kupotezeana muda kwa mambo ya kipuuzi. Watu wapo serious nyie mna wa actia.
 
Huo ni ubunifu wao katika kupeleka taarifa, inawezekana kuna mtu imempata kwenye mfupa.......wanaposoma hayo magazeti nafikri hawazuiliwi kuwa na mjadala wa hizo habari zilizoandikwa kwa hiyo bado wanaweza kuwa na mitazamo tofauti wakaonekana kama wanaongeza maneno.​
 
Mbwembwe, rejea kwa watangazaji wa mpira kama kina baraka mpenja na nazareth upete kama si mbwembwe zao wasingepata umaarufu wa kutangaza mpira. Kuna wasoma taarifa ya habari ile wanaitambulisha taarifa ya habari kupitia media za utapenda, muangalie farhia middle vile anavyotamka itv super brand na kile kidole gumba unapapata hamasa kusikiliza na kutazama, wapo wengi tu akina abdalah tilata wa star tv na usomaji wao wa habari za michezo utapenda kila siku wawe wanasoma kwa mbwembwe
 
Hayo muwe mnafanyia chumbani si kwenye vyombo vya habari. Tatizo la nchi hii vilaza ni wengi kuliko sisi. Tupo wachache sana. Sometime mnataka sasa mtuzidi hata kwenye mambo ya maana.
kesharekebisha kauli yake we bado unang'ang'ana na msimamo wake tuliouponda. Mbwembwe ndio huvuta wasikilizaji wewe. Cheki hotuba za baba wa taifa hutochoka kusikiliza kuliko za marais wengine hawakuwa na ujanja wa kuvuta wasikilizaji. Mkuu mbwembwe ni sanaa tu usikwazike kuzisikia
 
Muhimu chagua chanel ipi usikilize hivyo vichwa vya habari
 
Taarifa ya waziri wa habari
Screenshot_20240215-155057.jpg
 
kesharekebisha kauli yake we bado unang'ang'ana na msimamo wake tuliouponda. Mbwembwe ndio huvuta wasikilizaji wewe. Cheki hotuba za baba wa taifa hutochoka kusikiliza kuliko za marais wengine hawakuwa na ujanja wa kuvuta wasikilizaji. Mkuu mbwembwe ni sanaa tu usikwazike kuzisikia
Nyerere hakuwa na mbwembwe alikuwa smart kichwani alikuwa mwanafasihi. Si hawa vilaza.
 
Huo ni ubunifu wao katika kupeleka taarifa, inawezekana kuna mtu imempata kwenye mfupa.......wanaposoma hayo magazeti nafikri hawazuiliwi kuwa na mjadala wa hizo habari zilizoandikwa kwa hiyo bado wanaweza kuwa na mitazamo tofauti wakaonekana kama wanaongeza maneno.​
Wapumbavu hawatapungua Tazanzania.
 
Back
Top Bottom