Android Application Development.

Android Application Development.

Life starts at 45

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2015
Posts
998
Reaction score
987
Wakuu natumaini mu wazima wa afya, karibu hapa tujadiliane kidogo kuhusiana na maswala ya Android application development.
Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakihitaji kuingia kuna Android Development lakini wanakosa pa kuanzia sasa hapa nazani patawafaa sana.

Natambua kuna nyuzi kadhaa zimewahi anzishwa hapa kuhusiana na android development lakini huu ni tofauti na hizo. Hapa hatujalenga kuwa tunaandika code za kudevelop app badala yake tutakuwa tukiangalia jee kuna teknologia gani zipo na utumie ipi na kwa nini. Tutaangalia vitu kama what are good practice that are recommended by google. Leo kwa kiasi kikubwa tutaenda kutazama ni kwa nini kwenye development zetu tutumie Kotlin instead of java.

kotlin.
Kotlin imeanzisha mwaka 2011 ikiwa kama official programming language kutoka google. Na kutangazwa rasmi mwaka 2017 kama official programming language kwa ajili ya android development. Toka kotlini kutangazwa kwake imekuwa ikijichukulia umaarufu na hivyo watu wengi kuamia huko. Sasa kama wewe ndio kama unaanza kujifunza Android basi nakushauri tumia kotlin kwa ajili ya development zako.



KWA NINI KOTLIN.
  • Kotlin inakuwezesha kuandika code chache.
Ukiwa na code nyingi basi zinaongeza na muda pindi ukiwa unataka hata kufanya maintenance ya system yako mfano hebu jaribu kuangalia tofauti ya hizi code mbili kati ya java na kotlin.
Java

1650628607614.png


Kotlin
1650628634473.png



nazani wewe wenyewe umejionea utafauti kati ya hizo code mbili japo zote zinafanya jambo moja sasa kwa nini utake maisha magumu ilihali rahisi yapo?
Code chache unachukua muda mchache kuandika, mda mchache kusoma na inapunguza hatari za bugs zisizokuwa za msingi.

  • Boilerplate code.
Boilerplate code hizi huwa ni zile code ambazo mara nyingi zinajirudia hivyo ukiwa unatumia kotlin basi wao wamejitahidi kwa kiasi kikubwa kuondoa boilerplate code.
Mfano mzuri huwa ni data class it's likely any prgram lazima itakuwa na data class so sasa kwa nini watu wajichoshe kuadika kitu kile kile ilihali kuna uwezeakano wa compiler kufanya hiyo kazi.

  • Null pointer exceptions.
Kwa kiasi kikubwa kotlin imepunguza maswala ya app ku clash ikiwa ina run kutokana na sababu za null pointer exception sababu inakupa uwezo wa kutengeneza variable ambayo inapokea null varible.
1650629788691.png



  • Faida zingine ni kama kuwa na default value kwenye function parameter.
  • ku achive multithread kwenye kotlin ni rahisi ukilinganisha na java.

kwa aliye na cha kuongeza au kulekebisha palipo na mapungufu basi anakalibishwa. Next time tutaangalia kwa nini ni muhimu kutenganisha back-end na front end.

Source.


@coutinhotz

 
Mkuu,hivi inawezekana kuanza apps development kama hauna background ya programming?kama hapana inatakiwa ujue nini kwanza kabla ya kuingia kwenye apps development? Life starts at 45
 
Mkuu,hivi inawezekana kuanza apps development kama hauna background ya programming?kama hapana inatakiwa ujue nini kwanza kabla ya kuingia kwenye apps development? Life starts at 45
Inakubidi kwanza kujua basics za programming kabla ya kuanza application development. Kama unahitaji kuanza kujifunza Android development basi anza moja kwa moja na lugha ya "Kotlin".
Kisha baada ya hapo waweza sasa kuanza kujifunza android app development.

Ila kama target yako ni iOS basi anza na "swift" kisha baada ya hapo ndipo uanze kujifunza development ya iOS Sasa.
 
Java ni sawa na ilivyo C au C++! Mtaiponda sana mara boiler plate mara google mara sijui nini! Lakini ipo na itaendelea kudunda na wenda mkafa mkaiacha.

NB: Android ni java na java ni android.
 
NB: Android ni java na java ni android.
Kwa legacy Android development language sio issue. Ila future ya Android ni Kotlin. Declarative programming ndio future na kwa Android ni Jetpack Compose.

Ninavyofahamu so far Compose ni Kotlin pekee. Hii ina maana Google watakapodondosha support ya Legacy Android development ndio itakuwa mwisho wa Java kwenye Android.
 
Kwa legacy Android development language sio issue. Ila future ya Android ni Kotlin. Declarative programming ndio future na kwa Android ni Jetpack Compose.

Ninavyofahamu so far Compose ni Kotlin pekee. Hii ina maana Google watakapodondosha support ya Legacy Android development ndio itakuwa mwisho wa Java kwenye Android.
Jetpack Compose ni Kotlin peke ake, java haifanyi.
 
Back
Top Bottom