Mkuu GM7 Kamwene mambo yamebadilika mkuu kila wakati mambo yanazidi kubadilika mkuu usifananishe Mjini iringa kasoro bahari na Jiji la Dares-Salaam mkuu umesoma mpaka Darasa la ngapi? jiji la Dar lina kila kitu cha Historia ya Nchi yetu tofauti na mjini iringa kwa Wahehe na Wabena Upo na mimi mkuu GM7?
mzizi mkavu, uwe unaelewa kinachoongelewa, tunachoongea hapa ni mpangilio wa mji, kwa mfano, ukiangalia hiyo picha ya mji wa iringa, jiji la Tanga na mji wa sumbawanga (just type hapo kwenye ramani yenyewe itakupeleka), utaona kuwa, miji ya iringa, Tanga na sumbawanga imepangwa vizuri sana sana, kiasi kwamba unaweza hata kuletewa barua home badala ya kupelekewa kwenye box yako posta....just angalia barabara zilivyopangwa vizuri kwenye jiji la Tanga, na hata hapo iringa...inaonyesha kabisa kuwa viongozi wa manispa wako makini kucontrol ujenzi usiwe holela....
ukija Dar, rafiki yangu, Dar hamna kitu, ukiwa na rafiki yako toka hata nchi ya jirani tu hapo, utaweza kumpeleka temeke, yombo, mbagala, buruguni, manzese etc....hata maeneo mazuri kama oysterbay, msasani, mbezi beach, masaki, mikocheni etc utakuta bado tu hawajapanga vizuri kabisa. sasa hii ni aibu, kwasababu tukitembelea nchi za wenzetu, tunaona kuwa wamepanga miji yao vizuri...miji yao misafi nk. sisi sote hata kama tunatoka mkoani, wote tunaishi apo apo Dar, LAKINI KUSEMA UKWELI, kila wakati nikishuka hapo Dar, uchafu huwa unaanza kunuka kuanzia airport hadi jiji zima na watu nchi zingine wamesema hadi wamechoka..ni PACHAFU, HALAFU NYUMBA KILA MTU ANAJENGA APENDAVYO.