Black listed
Senior Member
- Apr 6, 2023
- 181
- 260
Kibiolojia, kuna makundi makuu mawili ya viumbe hai hapa duniani. Kundi la kwanza linaitwa mamalia (animalia), na la pili ni mimea (plantae).
Kwenye kila kundi bado kuna mgawanyiko (classification). Kundi la mamalia tupo sisi binadamu na wanyama (hayawani).
Kuna sifa zinazotofautisha kati ya viumbe hawa wawili (binadamu na wanyama). Sifa hizo ni namna ya kutembea, aina ya vyakula tulavyo, nk. Lakini sifa kuu inayotufautisha wanadamu na wanyama ni akili na utashi (ustaarabu).
Ni kutokana na akili na utashi, maisha ya wanadamu yamejengwa katika misingi itakayomtofautisha na wanyama. Misingi hii ni sheria, mila, tamaduni, nk.
Misingi hii ipo katika ngazi ya taifa, mikoa, wilaya, tarafa, kata, vijiji, ukoo, hadi ngazi ya familia. Na ndio maana mtu akikiuka misingi katika ngazi yoyote huhukumiwa kulingana na ngazi husika.
Watu wengi hutii sheria za ngazi za juu tu, lakini hawatii sheria za ngazi za chini. Labda hii inatokana na uwajibikaji wa mamlaka ya ngazi hizo kuwawajibisha (kuwaadhibu) wale wote wanaoenda kinyume na sheria.
Katika ngazi za familia, na hata ukoo, watu wamekuwa wakikiuka mila, desturi, na utamaduni ambavyo ndio sheria zinazowalinda na kuwatambulisha.
Watu wanaharibu sifa ya familia au ukoo kwa kufanya mambo ambayo wanahisi kwao yana masilahi. Watu wa aina hii, wengi wao ni wabinafsi, na anafanya hivyo ili kuwaonyesha watu kwamba yeye ni wa kipekee, tofauti na familia au ukoo anaokotoka.
Kama kuna jambo jema limetokea ndani ya familia au ukoo wenu, kulitoa jambo hilo nje sio vibaya. Lakini likitokea, kwa bahati mbaya, jambo lisilo jema (labda la kutia aibu familia au ukoo), usilitangaze nje, maana utaharibu sifa ya familia au ukoo, ambako na wewe mwenyewe unatoka.
Utakuta mtu mmoja kutoka katika familia au ukoo fulani ana tatizo na anahitaji msaada kutoka kwa wanandugu. Wewe badala ya kumsaidia unatoka na kwenda kumtangaza vibaya kwa watu wa mbali, kwamba yule jamaa masikini sana, amekuja ameniomba kitu fulani. Unafanya hivyo ili kumharibia sifa yake.
Kuna mambo mengine yanatakiwa kuwa siri ndani ya familia au ukoo; hayatakiwi kutoka nje. Hapo ndipo linakuja suala la mila na desturi. Kila familia na ukoo vina mila tofauti na familia nyingine, japo baadhi zinaingiliana, lakini maadili yatabaki kuwa ndani ya familia na ukoo husika.
Kuna baadhi ya makabila yako makini sana katika suala la kutunza maadili ili kulinda mila, desturi, na tamaduni zao. Baadhi ya mabila haya ni yale ya kaskazini. Makabila haya, mtu akikengeuka, akatoa nje siri za familia au ukoo, atashikwa na kuletwa mbele ya familia au ukoo, atatandikwa fimbo hadhrani, bila kujali umri wake. Akitoka hapo, adabu tele!
Nadhani kila familia au ukoo, vingejiwekea taratibu na sheria za kufuatwa (kuchukuliwa) pindi ikitokea kuna watu wanaharibu mila na desturi, ili kuziepusha na aibu familia na koo husika.