Angalia Bunge la Katiba TBC na Star Tv

Angalia Bunge la Katiba TBC na Star Tv

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Fuatilia Bunge la katiba live TBC na Star Tv.

Leo ni semina ya kanuni kwa wajumbe wa Bunge maalumu la katiba na kwa hivi sasa kinachosubiriwa ni ugawaji wa rasimu za kanuni kwa wajumbe ingawa rasimu zenye hazitoshelezi ila nyingine zitaongezwa baadae.

Update:
Bunge limehairishwa mpaka saa 11 jioni ya leo.

Hata hivyo,kabla ya uamuzi huo,uliibuka mvutano huku wabunge wengine wakitaka semin hiyo iairishwe mpaka kesho na wachache akiwemo mh.Mdee na ma Makinda wakipendekeza semina hiyo iendelee jioni ya leo.

Baada ya kusikiliza hoja zote hizo,hatimae mwenyekiti wa muda akakubaliana na hoja ya kukutana jioni ya leo badala ya kuairisha semina hiyo hadi kesho kwa hoja kuwa muda uliopo ni mfupi.
 
Kama kawa vituko havikosi nakala hazijasambazwa wanazisubiri walikuwa wapi kuandaa mapema
 
Tbc wamekata matangazo ya bunge wameleta matangazo mbalimbali
 
hivi nyie kushinda kwenye tv kuangalia bunge hamna kazi zingine za kufanya?

makaka fanyeni kazi wenzenu wanafanya utani hapo lakini posho 300000 inaingia.
 
Kwa mwenye kufahamu link ya TV ama Radio inayotangaza haya, tunaomba aturushie.
 
hivi nyie kushinda kwenye tv kuangalia bunge hamna kazi zingine za kufanya?

makaka fanyeni kazi wenzenu wanafanya utani hapo lakini posho 300000 inaingia.

Nipo dukani kwangu naangalia bunge,kuna tatizo kwani??
 
hivi nyie kushinda kwenye tv kuangalia bunge hamna kazi zingine za kufanya?

makaka fanyeni kazi wenzenu wanafanya utani hapo lakini posho 300000 inaingia.

Unajua nature ya kazi yangu?

Kwa kifupi,niko off.
 
Hawa jamaa mbona wanatuchanganya,?mara ijumaa mara nini sijui,bora tu kuangalia ITV -uzinduzi wa kampeni ya uelewa wa rasimu ya katiba. Live on ITV!
 
hivi nyie kushinda kwenye tv kuangalia bunge hamna kazi zingine za kufanya?

makaka fanyeni kazi wenzenu wanafanya utani hapo lakini posho 300000 inaingia.

Siku hizi mambo si kama zamani Maofisini kuna tv.kivukuni kuna tv,mahospitali ndo usiseme Bajaji kuna tv simu mchina kalaisisha zina tv watu wanaangalia na huku kazi zinaendelea....
 
hivi nyie kushinda kwenye tv kuangalia bunge hamna kazi zingine za kufanya?

makaka fanyeni kazi wenzenu wanafanya utani hapo lakini posho 300000 inaingia.

Utakuwa huna TV wewe na yule jirani yako ambako huwa unaenda kupiga chabo kwa TV yake kasafiri....
 
hivi nyie kushinda kwenye tv kuangalia bunge hamna kazi zingine za kufanya?

makaka fanyeni kazi wenzenu wanafanya utani hapo lakini posho 300000 inaingia.
hivi wewe unafikiri kazi ni kwenda ofisini tu, au kwenda kulima au kitu gani, hata kusikiliza bunge na kuwahabarisha wenzio nayo ni kazi. waache watuhabarishe sisi wengine tupo mbali na tv. ila nimefurahi sana kusikia na star tv sasa wameruhusiwa kuonyesha live maana tbc1 ni wasanii, ila naomba serikali iwape star tv mgao wa kodi zetu badala ya kuwapa zote tbc1.
 
hivi nyie kushinda kwenye tv kuangalia bunge hamna kazi zingine za kufanya?

makaka fanyeni kazi wenzenu wanafanya utani hapo lakini posho 300000 inaingia.

kwani unapoangalia Bunge ndio ina maana kuwa haufanyi kazi??? hayo ni mawazo ya kivivu
 
Back
Top Bottom