CCM NI MAJAMBAZI
Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa imemuhukumu kifungo cha miaka 22 Jela Maria Ngoda mkazi wa mtaa wa zizi la ng'ombe uliopo manispaa na mkoa wa Iringa baada ya kumkuta na hatia ya kukutwa na ndoo yenye vipande 12 vya nyama ya swala kinyume na sheria.
Hukumu hii imetolewa na hakimu mkazi mkuu mkoa wa Iringa Said Mkasiwa baada ya kujiridhisha pasi na shaka kuwa ni kweli mtuhumiwa alikutwa na ndoo iliyokuwa na nyama hiyo ya swala yenye vipande 12 ndani yake vyenye thamani ya Tsh. laki Tisa (900,000)
Mkasiwa amesema kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 86 (1) (2) (c) cha sheria ya uhifadhi wa wanyamapori namba tano ya mwaka 2009 kama ilivyofanyiwa marekebisho na kifungu cha 59 (a) (b) cha mabadiliko ya sheria ya mwaka 2016.
Kwamujibu wa ushahidi uliotolewa unaeleza kuwa siku ya tukio mtuhumiwa alikutwa na ndoo hiyo yenye vipande 12 vya Swala aliyokuwa akiiuza Karibu na nyumba yake.
Hivyo nyama hiyo ikafikishwa kwa mtambuzi na kubaini ni kweli ilikuwa ni nyama ya Swala na baada ya Tathmini gharama yake ikafika tsh. 900,000.
Kwa upande wake Mtuhumiwa wakati akijitetea alikiri ni kweli alikutwa na ndoo hiyo ambayo alidai alikabidhiwa na mtu aliyemtambua kwa jina la Fute na awali hakujua inanyama ya nini ndani yake.
"Mheshimiwa ni kweli siku ya tukio nilikuwa kata ya Isakalilo na Mama Ziada nikiuza nyama kwenye ndoo sikujua ni nyama ya nini kulikuwa na vipande 13, kimoja akaondoka nacho yeye baada ya muda mwenyekiti wa mtaa akaja na askari wakaniweka chini ya ulinzi wakisema nauza nyama pori mimi nikasema hii ndoo si yangu ni ya Fute wakaniweka kwenye gari hadi kwa huyo Fute" alisema mtuhumiwa
Maria aliendelea kujitetea kuwa baada yakufikishwa kwahuyo mtu licha ya kumtaja na kumtambua mtuhumiwa uongozi ulimlazimisha abebe ndoo hiyo na kufikishwa kituoni na kufunguliwa kesi ya kukutwa na nyara za serikali sambamba na kosa la uhujumu uchumi.
Kesi hii ilisimamiwa na muendesha mashtaka upande wa jamhuri Simon Masinga ambaye aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa Mtuhumiwa ili iwe fundisho kwake.
"Mheshimiwa hifadhi zetu za taifa zinategemea sana wanyama kama swala kuvutia utalii na unachangia pato la taifa hivyo kosa lina athiri uchumi wa taifa hivyo apewe adhabu kali ili iwe fundisho kwake na wengine wanaotarajia kufanya kosa kama hilo" alisema Masinga muendesha mashtaka upande wa jamuhuri.
Hivyo baada ya kusikiliza pande zote mbili ndipo mahakama ikamkuta na hatia na ikamuhukumu kifungo cha miaka 22 Jela.
Hata hivyo hukumu hii imeibua hisia Mseto kwa wadau na wanasheria baadhi kutokana na jinsi shauri lilivyo endeshwa kwani mtuhumiwa hakupata uwakilishi wa kumtetea kipindi chote cha kesi yake hivyo baadhi ya mawakili wamejitolea kukata rufaa na kumsaidia mtuhumiwa katika kesi hii.
Sent using
Jamii Forums mobile app