Prof Phraoh AI
JF-Expert Member
- Mar 25, 2024
- 1,269
- 2,311
Mwaka 1961, mwanasaikolojia wa Chuo Kikuu cha Yale, Stanley Milgram, alifanya jaribio ambalo lilionyesha jinsi ubongo wa binadamu unavyofanya maamuzi unapokua chini ya mamlaka fulani na kuibua swali zito kuhusu utii wa binadamu kwa mamlaka.
Katika jaribio hilo linalojulikana kama Milgram Obedience Experiment washiriki waliambiwa wanashiriki katika utafiti utakaoonyesha kama adhabu itamfanya mtu akumbuke zaidi kile anachojifunza.
Kila mshiriki alipewa jukumu la “mwalimu,” huku mtu mwingine akiwa mwanafunzi.
Kazi ya mwalimu ilikuwa kumpiga mwanafunzi shoti ya umeme kila alipokosea swali.
Kadri jaribio lilivyoendelea, msimamizi wa jaribio hilo alizidi kumwambia mwalimu aongeze zaidi kiwango cha umeme hatua kwa hatua kutoka kiwango cha chini hadi kile kilichoandikwa kuwa hatari sana ambacho kinaweza kusababisha kifo.
Cha kushangaza ni kwamba, zaidi ya asilimia 60 ya washiriki waliendelea kuongeza shoti ya umeme kadiri wanavyo agizwa hadi kiwango cha juu kabisa. pale walipoonekana kusita kuongeza umeme, mtafiti aliyekuwa amevaa koti jeupe aliyekuwa akiwaongoza aliwaambia kwa sauti ya utulivu "Jaribio linakutaka uendelee"
Ingawa mwanafunzi hakuwa anapigwa shoti ya umeme wa kweli bali alikua mmoja ya watafiti wa jaribio hilo, alitoa sauti za maumivu, kupiga kelele, na hata kuomba asitishwe jaribio. Wakati fulani alionekana kama amezimia kabisa.
Jaribio hili lilionyesha kuwa watu wa kawaida, wasio na historia ya ukatili, wanaweza kufanya mambo hatari kwa wengine wakiamini tu kwamba wanatii mamlaka halali.
Mfano halisi unaoonyesha nguvu hiyo ya ushawishi ni tukio la mchungaji wa Kenya, Paul Mackenzie Nthenge. Kupitia mafundisho yake, aliwashawishi wafuasi wake kufunga chakula hadi kufa akiwaaminisha kwa kufanya hivyo "watamuona Yesu" jambo lililosababisha vifo vya watu wengi. Wengi wao hawakuwa wajinga wala wagonjwa wa akili. Walikuwa watu wa kawaida waliomwamini kiongozi wao kiroho bila kuhoji.
Hapa ndipo tunaona kuwa ubongo wa binadamu hauko huru kama tunavyopenda kuamini. Unategemea mamlaka, mazingira, na mitazamo ya kijamii kufanya maamuzi.
Ukimuweka mtu ndani ya mfumo unaompa uhalalali wa kutii anaweza kufanya jambo ambalo yeye binasfi asingeweza kulifanya kamwe.
Hii inaitwa agentic state. hali ambayo mtu anahisi yeye si mhusika mkuu wa maamuzi, bali ni chombo tu cha kutekeleza maagizo ya mamlaka.
Hivyo mtu anaweza kufanya jambo analoona kabisa si sahihi, lakini akajifariji kwa kusema:
"Mimi nafuata tu maelekezo."