Angalia Mafundi wa mjini wanavyojua kula

Angalia Mafundi wa mjini wanavyojua kula

BARA BARA YA 5

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2009
Posts
1,174
Reaction score
835
Nimepita gereji mara moja mida ya saa tisa hivi, fundi wangu kaletewa wali maharage na maparachichi kama matatu hivi, akashushia fanta ile nyeusi.

Baada ya kama dakika kumi akapita muuza madafu akanunua moja kanywa maji na ile ya ndani kakwanguliwa, akapita muuza karanga kanunua fungu moja baada muda hivi kaja muuza machenza kanunua mawili, kamaliza kapita dada anauza mihogo mibichi na matango kununua kala.

Wakati naanza kupata wasiwasi ghafla mkaka anauza miwa kaja fundi kachukua vipakti vitatu. Nikijua sasa huu ni mwisho ghafla kaja dada anatembeza mahindi ya kuchemsha bila hata kujistukia fundi kaagiza moja.

Nikiwa nimetoa macho kama mjusi aliyebanwa na mlango ghafla kaja dada anauza uji wa mchele, fundi bila kupepesa macho kaagiza kikombe kimoja.

Wakati najiandaa sasa kuondoka kaja muuza pweza wale vipande na supu kwenye chupa ya chai kanunua kama vipande saba.

Muda huu naondoka nimepishana na muuza kahawa. Watu wanamiliki matumbo wallah.
 
Kawaida mtaani dah ila huyo kazidi
 
Hayo yaliyokupeleka ulifanikiwa au uliondoka na umbea wa kuhamaki mwanaume mwenzako anavyokula?
 
chakula hicho lazima kikimbilie kule kwenye mtalimbo shughuli yake anaifahamu mkewe

ila kwa wale wanaokaa kwenye viti vya sponji masaa sita amekodolea laptop chakula cha mchana wao wanaita fast food sijui akifika home hoooi hata pafomansi nayo inapungua
 
wakisema matumbo au vitambi yalipiwe VAT watu watakimbilia rwanda
 
Yaani mda wote huo unamhesabia aliuliza risiti maana mmmh shauri zako watakuuliza uwapeleke garage.

Halafu wakati wote huu hajaenda beitul raha
 
Huyu atakuwa fundi wa mkoani kaja kwa ancle...
 
Back
Top Bottom