Angalia reaction ya serikali kwenye matukio haya kisha za kuambiwa ongeza na za kwako

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,409
Reaction score
13,262
1. Kushambuliwa kwa Lissu: Kimya mpaka sasa mwanzo Lissu akiwa Ubelgiji walisema hatoi ushirikiano. Sasa Lissu yupo na amewataja kwa majina wabaya wake lakini serikali kimya hakuna hata panya aliyekamatwa.

2. Kutekwa na jaribio la kumuua Sativa: Waziri mwenye mashavu makubwa kasema eti Sativa hatoi ushirikiano. Jiulize upi wakati keshawataja wahusika? Mpaka sasa kimya

3. Kutekwa Deus Soka na wengine mpaka sasa kimya

4. Kuuawa kwa mzee Kibao mpaka sasa kimya

5. Kutekwa kwa Benny saa nane na kupotea na wenzake waliotekwa enzi za jiwe mpaka leo kimya

6. Kuuawa kwa Akwilina kwa risasi za polisi. Mpaka sasa kimyaaa

7. Kuuawa kwa Mawazo

Kwa ufupi matokio yote hapo juu haywezi kuchunguzwa na serikali na kutoa majibu kwakuwa yenyewe ndiyo mtuhumiwa mkuu. Mhalifu hawezi kujichunguza na kujichukulia hatua. Hapo inahitajika vyombo huru kabisa vya kimataifa kuchunguza na sio serikali hii ni kupoteza muda.

Lakini angalia uharaka wa serikali kwenye matukio haya:

1. Kijana kachora mwenyewe picha ya rais kisha kaichana akakamatwa na kuhumiwa haraka kwa muda usiozidi wiki 2

2. Mchungaji alikuwa anapinga kuuzwa kwa bandari haraka haraka kahukumiwa na kufungwa kwa kuendesha kanisa bila usajili lakini kina Suguye walipewa muda wa kusajili na baa iliyokuwa haina keseni ilifungiwa ili isajili keseni lakini wakurugenzi hawakushitakiwa wala kufungwa. Hiyo ndiyo Kusadikika chini ya mtawala kutoka ng'ambo
 
kibaya na cha kuumiza ni kuwapa majonzi na mapengo family zinazo ondokewa na wapendwa wao, mbaya sana.

Uzuri ni kwamba hata wao watakufa tu kamano 1 wao alivuta wao nani ? ,
 
“Serikali ina mkono mrefu”, ukiona mkono wa serikali umeshindwa kufika mahali jua kuna mtu mfuko wake wa shati ni mkubwa sana ameiweka serikali yote mfukoni. (maneno ya JK Nyerere kwenye moja ya hotuba zake)

Kuna “watoto” wanadhani kuwatengenezea viongozi wa CDM kesi kama hizi za mauaji/ ugaidi ni jambo rahisi, mtachekesha watu na ushahidi wa kuunga unga kama ule wa kina Kingai na wenzake.

Narudia tena, viongozi wa CDM wangekuwa na mikono michafu, ingechukua only 3 Business days kupatikana kwa shahidi kedekede za kuwatia hatiani, Kwasababu ni kweli kuwa hawa watu wamefungwa “radar” kila kona wanasubiriwa wateleze tu watu waruke nao.

Rais akiagiza by 05:00 COB niletewe faili, watu wanafanya kazi kama robots. Kigugumizi kirefu, kuna nini? tuelewe nini?

Vyombo vya usalama tuleteeni wahalifu hizi kelele ziishe, ule mkono mrefu kwanini umeanza kuwa mfupi?
 
1. Kushambuliwa kwa Lissu: Kimya mpaka sasa mwanzo Lissu akiwa Ubelgiji walisema hatoi ushirikiano. Sasa Lissu yupo na amewataja kwa majina wabaya wake lakini serikali kimya hakuna hata panya aliyekamatwa.

2. Kutekwa na jaribio la kumuua Sativa: Waziri mwenye mashavu makubwa kasema eti Sativa hatoi ushirikiano. Jiulize upi wakati keshawataja wahusika? Mpaka sasa kimya

3. Kutekwa Deus Soka na wengine mpaka sasa kimya

4. Kuuawa kwa mzee Kibao mpaka sasa kimya

5. Kutekwa kwa Benny saa nane na kupotea na wenzake waliotekwa enzi za jiwe mpaka leo kimya

6. Kuuawa kwa Akwilina kwa risasi za polisi. Mpaka sasa kimyaaa

7. Kuuawa kwa Mawazo

Kwa ufupi matokio yote hapo juu haywezi kuchunguzwa na serikali na kutoa majibu kwakuwa yenyewe ndiyo mtuhumiwa mkuu. Mhalifu hawezi kujichunguza na kujichukulia hatua. Hapo inahitajika vyombo huru kabisa vya kimataifa kuchunguza na sio serikali hii ni kupoteza muda.

Lakini angalia uharaka wa serikali kwenye matukio haya:

1. Kijana kachora mwenyewe picha ya rais kisha kaichana akakamatwa na kuhumiwa haraka kwa muda usiozidi wiki 2

2. Mchungaji alikuwa anapinga kuuzwa kwa bandari haraka haraka kahukumiwa na kufungwa kwa kuendesha kanisa bila usajili lakini kina Suguye walipewa muda wa kusajili na baa iliyokuwa haina keseni ilifungiwa ili isajili keseni lakini wakurugenzi hawakushitakiwa wala kufungwa. Hiyo ndiyo Kusadikika chini ya mtawala kutoka ng'ambo
Kweli kabisaa
 
Namnukuu mzee wa Upako.Kila serikali Duniani ina vikosi vya kuteka na kuwapoteza wajingawajinga,mambo ya kumteka mtu kisa kachoma picha ya Rais ni ushamba, mbona magazeti yana picha ya Rais na watu wanafungia mandazi na vitumbua nao wapotezwe?
 
Back
Top Bottom