Angalia Waafrika Tulivyopitia Wakati Mgumu Sana

ndio,hata wazungu wa asia washapigwa matukio ya kikatili kama hayo,lakini weusi ndio wanakelele.bado pia nchi za Africa zinajitawala na bado wanafanyiana ukatili wa kupindukia.ipo hivyo mkuu.
Noted, ila katika jamii zote waliopata kibano sana ni waafrika nadhani lesi yetu imetapakaa sana duniani kutokana na kuchukuliwa kama watumwa, hao wengine ni kidogo sana.
 
Nani kakumbia siku hizi hakuna adhabu kama hizo? Tena zipo adhabu mbaya zaidi. Soma kitabu cha Mdude Nyagali uone mateso aliyopitia chini ya watu weusi wenzake. Na siyo hilo tu. Leo hii anza kuisema serikali na viongozi wake kwa kuonyesha makosa yao au ufisadi usipojikuta kwenye mateso makali kuliko hata haya. Mbona yule mbunge aliingiza chupa kwenye sehemu ya haja kubwa ya kijana kule Babati? Ni hali imebadilika tu kuwa sasa mwafrika ndiye anamtesa mwafrika mwenzake.
 
inafikirisha sana, lakini binadamu aina na muundo wa maishatuliochagua wa kwenda nao unatupa gharama sana.
Mimi nawaza mwisho wa muafrica huyo sijui hata kama alikuwa anaelewa kilichokuaa kinampata. Kuna muda huwa sitamani kuwasamehe hawa mabwana ila basi tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…