Angalizo kuhusu kitabu cha “Rich dad - Poor dad”

Angalizo kuhusu kitabu cha “Rich dad - Poor dad”

Ukweli ndio huo, hata uende marekani km huwezi jiongeza utasanda tu.
 
Kuna vitu ambavyo binafsi huwa navifundisha lakini sivifanyii kazi.

Ila kila ninachokufundisha nilishakijaribu kwa vitendo, nikaacha kuendelea nacho kwa sababu maalumu.

Hicho kitabu; kinafungua macho ili kila utakachotenda ujue mbele kuna nini.
 
Rich Dad Poor Dad is surely an eye opener na haijalishi upo Canada au Tanzania, unaweza ukaimprovise some suggested strategies na ukatoka

1. Mind your own business: sio lazima uache kazi kwa haraka ila unaweza ukafungua biashara/other sources of income kuliko kuendelea kutegemea salary tu ambayo haina maisha marefu na chances za kuajiriwa zinapungua as you get older

2. Use other people's money: kama una opportunity ya kukopa, kopa na uitumie vizuri hiyo fedha. Tumia fedha za watu. Utapiga marktime sana kudunduliza vijisenti vyako mpaka uje ufikie minimum target amount uliyoset kufanyia maendeleo

3. Focus on buying income generating assets and not useless stuff (liabilities): epuka kupoteza muda na fedha kununua junkies kama miiphone mikubwa zaidi ya moja, magari, kuhongahonga hovyo etc wakati huingizi chochote

4. Focus on investing your money rather than saving it: well, as long as una idea ya kufanya business, kuweka hela bank zikae tuuu kwa riba ndogo sana au bila riba kabisa ni kupoteza.

5. Your house is NOT an asset: hapa kuna utata kidogo ila alijaribu kufafanua. Asset simply ni kitu inayokuingizia faida na liability ni kitu inayochomoa mpunga kutoka kwa wallet. As long as nyumba yako umeipangisha, hiyo ni asset. Otherwise ni "liability" kwani itahitaji gharama za maintenance. Probably alikuwa anataka kuincourage watu wainvest fedha zao kwanza kwenye assets then faida kidogo inayopatikana lbd ije kutumika kujenga

Hayo ni kwa uchache ila kuna mengi ya kujifunza!
Big up,
 
Kitabu kizuri sana, kimenisaidia sana yaani sasa najiamini kutohangaika na kununua liabilities. Kwa sasa naamini hata nikiwa na pesa ndogo nitaweza kuanzisha biashara ndogo ila inayokua.
ASANTE SANA ROBERT KIYOSAKI maana haukupoteza muda wako kuandika kitabu hiki.
 
Mwanzo wa business yoyote ni kujua Wateja wako wanataka nini na kujua namna Bora yakuwahudumia.

Biashara nyingi zina-fail kwasababu waanzilishi wanadhani wanajua zaidi ya wataja wanaotaka kuwapatia huduma.

Makosa kama haya yanaweza kuepukwa kama utapata mentor mzuri.

Na moja ya mentorship unaweza kutumia vitabu, maandishi au kupata mawasiliano kabisa na role model wako.

Rich Dad, Poor Dad inakufundisha financial literacy.

Lakini hiyo ni kiasi kidogo utakachojifunza kuhusu kuunda business.

Kama upo na wazo la biashara ngoja nikupe tips ambazo zitasaidia sana wewe kuepuka makosa.

1. Eleleza akili yako kwenye kugundua tatizo.

- usiwazie jinsi utakavyotatua tatizo. Juwa kwanza je kuna tatizo sehemu fulani. Write them down on your notebook ili usisahau.

2. Ongea na watu wachache wanaokutana na hilo tatizo na uwaulize je unaweza kuwasaidia vipi?

3. Tengeneza suluhisho la hilo tatizo kama wanavyopenda clients wako.

Ukifuata hizo hatua utaokoa muda na fedha.

Well, kwa ambaye anapenda kupata namna ya kutengeneza hela kwakutumia ujuzi wowote alionao contact me through my email address wiserastarising@gmail.com

I'm building freelance platform ya kwanza ya Kiswahili. And everyone can join. It's FREE.

You won't pay a dime.

Wakuu nahitaji kuwasiliana na walio-interested ili nijie namna nzuri yakufanikisha hili.

Lengo langu ni kutatua hii changamoto ya watu kushindwa kutengeneza kipato wanapoteza muda au kudanganywa na online marketers wasio waaminifu.

Nitajibu ujumbe punde nikipokea.
 
Kitabu kizuri sana, kimenisaidia sana yaani sasa najiamini kutohangaika na kununua liabilities. Kwa sasa naamini hata nikiwa na pesa ndogo nitaweza kuanzisha biashara ndogo ila inayokua.
ASANTE SANA ROBERT KIYOSAKI maana haukupoteza muda wako kuandika kitabu hiki.
Hiyo imekaa poa sana.
 
Hiki kitabu ukikisoma mwanzo mwisho ama kweli kinatia hamasa na kama unaajira ambayo haieleweki unaweza andika barua siku hiyo hiyo

Lakini kitabu hiki kimekaa kinadharia zaidi na vitendo vyote vimeachwa kwa msomaji, sote tunajua ni jinsi gani vitendo vilivyovigumu hata katika masomo yetu ya kawaida.

Sasa huyu anayeitwa poor dad ndo anareflect more than 80% ya maisha ya mwanadamu wa kawaida na ambavo wengi huwa tunafikiri, kwa mfano kiyosak anasema kujenga nyumba ni hasara, mshara mkubwa si lolote, usikope pesa etc etc. mhii sawa.

Sasa ukichagua maisha ya huyu anayeitwa rich dad make sure unatoboa narudia tena make sure unatoboa vinginevyo hawa wanaonekana wanafuata maisha ya poor dad ndo wataonekana matajiri mbele ya macho ya wengi

Zile p;rinciple ukizifuata mwanzoni watu lazima watakuona wa ajabu na usipofanikiwa utakuwa wa ajabu zaidi hadi miti itakucheka, kwa hiyo ndugu zangu tupambane haswa tuanapochagua maisha ya rich dad siyo mziki wa kitoto hakuna lele mama tuset stratege za kueleweka ukifanikiwa maisha ni mteremko mnoo na hawa wanaoonekana matajiri kwa mishara utawaajiri baadae

othrewise follow poor dad life style mabayo ndo maisha ya wanadamu walio wengi.
Mtazamo wa rich dad niliamua kuufuata nikiwa mwaka wa pili chuo. Nivigumu sana but nivilahisi ukizamilia. Sijafanikiwa sana hadi sasa but hadi Leo sijachukua cheti cha kuhitimu chuo na pia mfanyakazi wa mshahara wa 1million siyo kitu kwangu ambaye naendesha maisha ya utafutaji wa kijasiliamali. Jambo linalonifariji kwa kufata mtazamo wa rich Dad I see the Bright future.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zile p;rinciple ukizifuata mwanzoni watu lazima watakuona wa ajabu na usipofanikiwa utakuwa wa ajabu zaidi hadi miti itakucheka, kwa hiyo ndugu zangu tupambane haswa tuanapochagua maisha ya rich dad siyo mziki wa kitoto hakuna lele mama tuset stratege za kueleweka ukifanikiwa maisha ni mteremko mnoo na hawa wanaoonekana matajiri kwa mishara utawaajiri baadae
Je unaposoma kitabu nini ni lengo hasa?
Labda tuanzie hapa.
 
Kuna mambo mengi unaweza kujifunza kwenye kitabu cha Rich Dad, Poor Dad. Nadhani wewe umeangalia jambo moja ambalo linahusiana na msisitizo wa Kujiajiri ni bora kuliko Kuajiriwa.

1. Je dhana ya kufanikiwa inahitaji zaidi ni kiasi gani cha fedha unahifadhi na unawekeza badala kiasi gani unatengeneza nayo ni ya watu wa Marekani?

2. Msisitizo wa kununua Real Assets (kama viwanja, mashamba, nyumba n.k) badala ya Liabilities (gari ya kutembelea kama huna fedha ya kuitunza, nyumba ya kifahari unayoilipia kodi pasipo kukuingizia/hauishi) je hiyo ni kwa Wamarekani tu

3. Dhana ya kujilipa wewe kwanza (Save the amount you want to save, before starting spending your income) je hiyo haiwezi kumsaidia Mtanzania wa Nachingwea ambaye ni muuza korosho?

4. Dhana ya kuwa na jambo ambalo litakupa usongo wa kutaka kutoka kimaisha ni la Wazungu tu? Mfano anashauri wengine wanaweza kutumia mapenzi, wengine waliwahi kufedheheshwa na kudharaulika, wengine wanataka watembelee ulimwengu n.k Kiyosaki anashauri utafute sababu ili upambane kwenye maisha mpaka utoke.

6. Kuwa Mtoaji wa Kihindi (Indian Giver). Ukikopesha hakikisha unarudishiwa, ukisaidia ni pale inapolazimu, usiwe unatapanya mali. Nitatoa mifano ya kibongo, usipende sifa bar kwa washikaji, usipende sifa kwa wanawake, usitoe hela kwa watu hovyo hovyo.

Back
Top Bottom