Angalizo kwa vijana wa kiume; Kuwa makini sana usijekuwa "RETIREMENT PLAN" ya mwanamke yoyote kwenye dunia hii

Angalizo kwa vijana wa kiume; Kuwa makini sana usijekuwa "RETIREMENT PLAN" ya mwanamke yoyote kwenye dunia hii

KikulachoChako

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2013
Posts
19,185
Reaction score
37,239
Habari za muda waungwana wa hapa jamvini........

Hakika ujana una harakati na changamoto nyingi sana.......

Kijana
Umekuwa katika mazingira magumu huku ukiipata elimu kwa tabu kutokana na uchumi wa wazee wako......

Umeyashinda magumu hatimaye umeihitimisha safari yako ya kielimu na kuingia kwenye soko la ajira na kubahatisha ajira inayofanya walau wazazi wako na wewe muendeshe maisha.....

Unaamua kujipanga kimaisha kwa hicho kipato kidogo cha ajira yako huku ukipambana na mihemko ya tamaa na anasa za dunia kwa kujizuia na wakati mwingine kutumia kinga pale unapojikwaa ili usitoke nje ya malengo na mipango yako........

Hatimaye unayafikia malengo na kujiona kuwa una misuli ya kuyakabili mambo ya ndoa hivyo unaamua kuoa.......

Mtihani wa pili mkubwa wa maisha yako ndio unaanzia hapo.....na ndio mtihani ambao ukifeli unaweza kukurudisha nyuma kwa spidi ya mwanga kule ulikotoka au hata kaburini kabisa.....na ukifaulu utajiona duniani hapa kama upo peponi

Unapoliangalia soko la waolewaji ndio unazidi kuchanganyikiwa maana waongo na wa kweli wote wanaongea lugha moja na kutabasamu........

Bila shaka unastahili mwanamke bora atakayekupa utulivu na kujivunia yale uliyoyapigania na sio mwanamke atakayekuongezea mawazo na kuyajutia maisha yako na mafanikio yako........

Katika wakati kama huo kuwa makini sana na utangulize akili yako mbele na sio hisia za mapenzi pekee ili usijekuwa RETIREMENT PLAN ya mwanamke yoyote.......

Nachelea kuyaandika mengi kwani naweza kutafsirika vibaya na baadhi ya watu..... lakini nadhani watu wazima wenzangu washajua RETIREMENT PLAN kwa mwanamke namaanisha nini......

WORD IS ENOUGH FOR THE WISE.......
 
mkuu hebu tuwape break kidogo, sidhani Kama wote wana mienendo mibovu kihivyo.

Kumbuka hata wewe Kuna mabinti Umesha kuwa nao kwenye mahusiano, mbona huja waoa au kubaki nao wote?.

FB_IMG_17388630247000341.jpg
 
Una haki ya kusema hivyo na kukaa na msimamo wako, ikiwa huja fanya miongoni mwa haya.

01, huja mpa binti mimba na kumtelekeza.
02, huja wahi kumwambia binti atoe mimba yako.
03, huja wahi kuchezea mabinti za watu na kuwa acha hovyo.

tofauti na hapo hichi unacho preach ni batili, maana cycle hiyo ya aina ya wadada tuna sababisha sisi wanaume.
 
mkuu hebu tuwape break kidogo, sidhani Kama wote wana mienendo mibovu kihivyo.

Kumbuka hata wewe Kuna mabinti Umesha kuwa nao kwenye mahusiano, mbona huja waoa au kubaki nao wote?.

View attachment 3230474
Sijasema kama wote wana mienendo mibovu bali nimemuambia kuwa makini....na sijamuambia asioe....

Mimi nimelitazama kwa mtazamo wangu wa kiume na wanawake nao wataliangalia kwa mtazamo wao kike...na kuwataadhalisha mabinti.....
 
Una haki ya kusema hivyo na kukaa na msimamo wako, ikiwa huja fanya miongoni mwa haya.

01, huja mpa binti mimba na kumtelekeza.
02, huja wahi kumwambia binti atoe mimba yako.
03, huja wahi kuchezea mabinti za watu na kuwa acha hovyo.

tofauti na hapo hichi unacho preach ni batili, maana cycle hiyo ya aina ya wadada tuna sababisha sisi wanaume.
Life ni experience na wakati mwingine kwenye hiyo experience unafanya maamuzi mabaya ndio maana watu wanatarikiana.....yale tunayopitia maishani ndio vinatupa experience na muongozo wako wa maisha ya mbele.....

Kama mimi nilifanya bad choises na kupata madhara basi ni wajibu wangu kuwataadhalisha watu ili nawao wasiyapitie niliyoyapitia mimi.....
 
Na siku hizi wanatumia nguvu za Giza kwa sababu ya ushindani wa soko hasa kwa kijna aliyejipata kimaisha unashangaa tu umeoa unakuja stukta akili zikirudi ulimuolea nini
 
Hivi ndo binti alivonijibu ana miaka 20 Intelligent businessman KikulachoChako binti anasema hataki ndoa kuna message alinitumia akaniambia ni-invest nikipata hela ndo nitafte just imagine binti kazaliwa 2004
 
Attachments

  • Screenshot_20250209_163612.jpg
    Screenshot_20250209_163612.jpg
    413.2 KB · Views: 4
Back
Top Bottom