Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao huumba!

Pasco unalakujifunza katika hili Anza mwanzo mpya ukiwa katika Hali ya kujifunza Yule uliyekuwa unamnadi humu kwa kumpigia zumari na kumsifu kwa nyimbo kede kede na kumpachika sifa asizo nazo kisa tu ana Nguvu ya kimamlaka ambayo alikuwa anaitumia ndivyo sivyo kwa kuikanyaga katiba na kuwaumiza watanzania walio wengi Kesha ondoka ulimwengu umemchukua

I hope now utakuwa una wa suppot wale wenye Vision ya kuwafikisha watanzania mahala salama bila ya uwepo wa kuwagawa kwa visasi na chuki
 
Kama ambavyo leo hii Magufuli hayupo, nani ana uhakika mwakani Mama Samia atakuwepo au yeye mwenyewe atakuwepo?

Ukweli ni kwamba, anaweza asiwepo Mama Samia na hata makamu wake
Duh....!. Hii ni kama ile ramli chonganishi!. Tuchunge sana kauli zetu, kauli nyingine huumba hadi vifo!.

P
 
Duh....!. Hii ni kama ile ramli chonganishi!. Tuchunge sana kauli zetu, kauli nyingine huumba hadi vifo!.

P
Tatizo viongozi hawajifunzi magufuli alikuwa na hakika kabla hajatoka madarakani atawapa watumishi stahiki zao. Akaondoka bila kutimiza.

Amekuja mwingine naye naona anafuata nyayo za mwenzake eti mwakani atakuja may mos akiwa na package nzuri. Ana uhakika gani? Linalowezekana leo kwaminj lingoje kesho? Je kama aliyeshikilia uhai kipimo chake kwa uongozi uliomadarakani ni kuona namna gani kiongozi utawapa watumishi stahiki zao? Mshikilia uhai akiona huwezi akaamua kuchukua uhai aliokuazima utalaumu?

Tuachame na hayo. Vipi mkuu ulifuatilia hotuba ya raisi? Kuna kakikohozi fulani ambako huwa sipendi kukasikia hasa mkuu akiwa anahutubia. Nilikasikia tanga pia wakati akihutubia taifa siku chache kabla ya kutangazwa kifo cha magufuli. Je kanaweza kuwa na maana yoyote hasa nyakati hizi ambapo mifumo ya upumuaji haieleweki kwa walio wengi?
 
Niliifuatilia hotuba ya rais mwanzo mwisho, lakini amini usiamini, sikukasikia hako kakikohozi fulani ambako wewe mwenzangu umekasikia na hukapendi. Pia ulikasikia akihutubia Tanga. Hotuba ya Tanga pia niliifuatilia na sikukasikia hako kakihozi fulani.

Kwenye kusikiliza hotuba za kingozi, kila mtu ana maeneo yake ya concentration, uki concentrate anasema nini, anaweza kukohoa na usisikie. Sasa kwa vile wewe tangu Tanga ulimsikia akikohoa, hivyo alipohutubia jana, wakati wenzako wamejikita kwenye kusikilizia anacho hutubia, kumbe mwenzetu concentration yako ni kusikilizia kama atakohoa.

Sio kila kikohozi kinahusiana na changamoto za upumuaji, vikohozi vingine ni alergy ya vumbi, upepo, harufu. Vikohozi vingine ni kupaliwa tuu katika kumeza. Vikohozi vingine ni muasho tuu, ukimeza cofta, vickis kingo, kinakwisha, na vikohozi vingine, haswa prolonged, ndivyo vinaweza kuwa ni infectious, hivyo vinahitaji anti biotics kuvitibu. Kwa vile mimi sio dakitari, naomba hili nisilisemee.
P
 
La kikohozi umejibu vyema kabisa sina nyongeza. Vipi kuhusu swala la kujifunza kutoka kwa magufuli ambaye aliwahakikishia watumishi kuwa kabla hajaondoka angefanya jambo na akaondoka kabla ya hapo?
 
La kikohozi umejibu vyema kabisa sina nyongeza. Vipi kuhusu swala la kujifunza kutoka kwa magufuli ambaye aliwahakikishia watumishi kuwa kabla hajaondoka angefanya jambo na akaondoka kabla ya hapo?
For the sake of kumuacha marehemu apumzike kwa amani, hili naomba nisilijibu.
P
 
Mwingine huyu katika manabii hawa!.
My point is kila binadamu ataonja mauti. Hivi Mbowe akitangulia Mbele ya haki, CCM mtaongea nini?

Je, akifa mtahudhuria msiba wake? Mtaongea nini kwa huyu mwamba siku akiondoka?
Mkuu Cathelin , please achana huu uchuro!. Kuna kauli nyingine huumba!.

Angalia usije kujikuta kumbe na wewe ni mtu wa kundi hili bila kujijua
P
 
Mkuu Pascal Mayalla kwa desturi nyingi Afrika, kuzungumzia kifo huonekana ni uchuro, lakini mwisho wa siku hata usipotamka au kutamkiwa kuhusu kifo bado utakufa. Wamekufa mababu na mabibi zetu, na watu bado wanakufa kila siku. Sidhani kama wote wanakufa kwa uchuro. Muhimu ni kila mtu akubali kwamba pamoja na yote tunayofanya, siku moja tutaonja mauti, hivyo tusisahau kutenda wema kwa wenzetu. Njia yetu ni moja.
 
Mkuu DidYouKnow , kuna kitu watu wengi hawakijui kuhusu kauli. Kuna watu na watu, wengine kauli zao zina nguvu za ajabu, wakiisha lisema tuu jambo, linatokea hivyo jambo hilo, wanakuwa wameliumba kwa kauli zao bila wao kujijua.

Fuatilia baadhi ya kauli katika bandiko hili....
I know you know, what happened thereafter!.
Kauli za kifo kifo ziepukwe, zisije zikawaudia watu vifo!.

P
 
Mayalla...
 
Na mbaya zaidi kaanza kuwa "prophet of doom" he always wishes doomsday to come in Tanzania for his devilish foresight about someone the "damned"

Na wote tuseme Amina ,
Mkuu The imp, kuna kitu umekisema hapa, Pascal Mayala kazeeka haoni mbele tarehe 25 mwezi 9, mwaka 2019 kunihisu mimi, halafu kilikuja kutokea kweli!. Nikisoma hapa ulisema nini kunihusu na nikipima na kilichokuja kutokea, kiukweli, naanza kujiogopa!.
Nakupitisha kwenye baadhi ya mabandiko yangu uangalie tarehe ya mabandiko hayo, nilisema nini lini na nini kimekuja kutokea kuhusu hicho nilicho kisema!.

The most powerful thing in this world is the power of will!.
Japo kuna msemo kuwa kauli huumba, kumbe kiukweli, kinachoumba sio kauli, bali the will ikiyoko ndani ya hiyo kauli.
If the will is strong enough, you can wish anything and it will happen or materialize!

P
 
fungue macho, jambo kubwa lina enda kutokea machoni pa Taifa ktk wakati hakuna angeweza kutarajia au kufikiri hivyo basi ni Maombi yangu na maombi yako yataliponya Taifa.
Mkuu TumainiEl , wewe ni mmoja wa manabii wetu wa ukweli humu, kwanza asante kututip kuhusu hili jambo kubwa linalohitaji maombi ambalo lilitaka kutokea Tanzania. Kufuatia tip yako hii na sisi watu wa maombi tupo, tumeomba, hivyo hilo jambo kubwa haliwezi kutokea tena kama lile!. Tena hata lile kama wasingefanya siri, tungeliweka kwenye maombi, lisinge tokea!.
NB. Kwa vile umezungumzia jambo kubwa za kuhitaji maombi kuliepuka, hala hala usiku kuingizwa kwenye manabii hawa Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao huumba!
P
 
Mkuu Paskali.
Kuiombea CCM ianguke ni sawa na kuliombea TAIFA lianguke?

Mimi ni mwanaCCM na hakika hakuna jipya jema kwa Taifa ambalo chama kinaweza kufanya kwa sasa.

Naungana nawe kutolipeleka Taifa tatizoni lakini nasimama kwenye zamu yangu kuliombea taifa litoke katika matatizo yanayoasisiwa na CCM
 
Tofautisha CCM na watu!. CCM ni chama, hakina tatizo, falsafa, ilani, sera etc, watu ni wanachama na viongozi ndio wanaweza kuwa tatizo, sio CCM kama chama!.
P
 
Tofautisha CCM na watu!. CCM ni chama, hakina tatizo, falsafa, ilani, sera etc, watu ni wanachama na viongozi ndio wanaweza kuwa tatizo, sio CCM kama chama!.
P
Ikiwa taasisi inashindwa kusimamia watu inapoteza uhalali wa taasisi hiyo kuendelea kuitwa imara.

Ilani, falsafa, sera na katiba vyote vipo sawa. Je hivyp vyote vinajisimamia au watu wanasimamia?

Iwapo ndani hakuna utii na dhamira ya kufanikisha yanayopaswa basi ni wazi hakuna mwelekeo wala jipya.


Nikosolewe kama siwazi sahihi
 
Tofautisha CCM ambacho ni chama, na watu ambao ni wanachama na viongozi. CCM ni kama kampuni, haiwezi kufanya makosa, ila viongozi na wanachama wanaweza kufanya makosa na kukosea.

Ni kama kampuni, haiwezi kukosea, lakini viongozi wake ambao ni watu, wanaweza kukosea. Kampuni inaweza kushitakiwa lakini haiwezi kufungwa jela!, wanaofungwa ni wamiliki!. Hivyo CCM kama chama, haina tatizo, tatizo ni watu!
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…