Ni Kupoteza muda kutaka Kuhoji Mahusiano ya Paul Makonda kama RC, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli na Serikali ya Awamu hii ya Awamu ya Tano ( 5 ) ambayo ipo chini ya CCM ambapo Wawili hao ni sehemu ya Chama na wana umuhimu Wao mkubwa tu huku kila wanachokifanya lazima ujue kuwa wanawakilisha vyema Ilani ya Chama. Kwahiyo ili labda uridhike ulikuwa unataka Makonda kila mara awe anamtaja na anamsifia Freeman Mbowe? Kwani CHADEMA tayari imeshashika Dola? Hivi ni mara ngapi huwa tunawaona Wanasiasa wote bila kujali Itikadi zao za Vyama wakijumuika pamoja pale Uwanja wa Taifa kuzishabikia Timu zetu pendwa Simba na Yanga hadi na Timu yetu ya Taifa na huwa hakuna huo Mgawanyiko wako unaojaribu Kuuhubiri hapa? Subirini Kwanza CCM itekeleze Ilani yake kwa Vitendo na kama nanyi pia ipo Siku mtakuja Kushika Dola basi mkiwa mnafanya yenu wala Watu wa CCM hawatowaingilia. Sijaona bado Kosa lolote kwa Mkuu wa Mkoa Paul Makonda juu ya hili sana sana naona tu ' Visununu ' vingi kutoka kwa Watu wenye Chuki nae Kisiasa, Kifikra na Kimtazamo. Kibinadamu Makonda ( RC ) ana mapungufu yake ila naona sasa tunazidisha hivyo tupunguze, tubadilike na mwacheni afanye Kazi yake.