Angalizo: Makonda akiendeleza siasa kwenye maandalizi ya Taifa Stars atawagawa watanzania

Angalizo: Makonda akiendeleza siasa kwenye maandalizi ya Taifa Stars atawagawa watanzania

Game tunaweza kushinda sababu Uganda wameleta wachezaji wengi wa kikosi B, hata hivyo tuelewe uamuzi wa kusonga mbele haupo mikononi mwetu ni mpaka Lesotho apoteze au adroo.
 
Ndiyo mana tuko mkiani kwenye records za nchi wananchi wake wenye furaha, kwa hili swala lilivyoandaliwa hata kama timu ya Taifa kwa bahati mbaya ikashinda basi ujue wananchi wengi hawatafurahia, ikitokea tukapigwa kipigo cha mbwa koko basi kila mtu ataibuka kwa furaha, Waganda njooni mtupe furaha kwa kutupa kipigo kitakatifu. Bashite ni shida


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hv lile bomba la mafuta si limetuunganisha sisi na uganda sasa ni ndugu....Kwa kuwa wenzetu tayari wana ziada sioni tukishindwa hapa
 
Nasimama na Tanzania kama mtanzania.
MUNGU ibariki Tanzania,
MUNGU ibariki Taifa stars.
 
siwez ficha mimi mshabiki wa simba kindaki ndaki tena sio kidogo ila nimekaa nimeangalia hili swala lilivyopelekwa sina wasi hii game tunafungwa tena nasema tunafungwa Tukutane hapa jukwaani jumapili jion




Sent using Jamii Forums mobile app
Gemu tulishanunua kelele unazoona watu wanajua tiyari kinachooonde kutokea ina maaana hujaona? Mipango ilishafanyika Ya kisiasa ndio maanaa tunasauti tunasubiria tu kuuza sura Kwa ushindi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina tatizo na hilo, ingawa hiyo ni perception tu..Binafsi mimi sijaona kuwa TFF ni tawi la CCM, ila ni kweli hao TFF nadhani wengi wao hawajui wanachofanya...Hawana mikakati, hawaangalii masuala ya michezo ...nadhani wapo kimaslahi zaidi..Yaani kumleta Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam eti kuwa mhamasishaji??? They are not serious at all...Yaani nimeangalia ile kamati ...nimeshanggaa...yaani eti hata...Mungu anisaidie nisitaje majina...sijui wanenguaji...sijui wengine ni watu wa kujikomba...yaani kimsingi hawana sifa kabisa...watu muhimu wa soka...kama akina Kibadeni, Kitwana na wengine kadhaa hawamo...Hivi kuhamasisha maana yake ni nini hasa??!! My God...Nimesoma leo mahali timu ya Arusha United imejitoa kwenye ligi daraja la kwanza kwa sababu ambazo ukizisikia kama ni za kweli zinatisha kabisa....Ligi Kuu iko raundi ya lala salama sina hakika kama Simba imeshacheza mchezo hata mmoja na Kagera au Mtibwa...Sina hakika kama Yanga imecheza hata mchezo mmoja na Azam...Ni ngumu kuielewa hali hii....Yaani wahamasishaji ni wanenguaji, na baadhi yao hata moral aspect haipo kabisa ndani ya jamii...Ni maajabu...Binafsi nilikuwa na nia kwenda kuishangilia Taifa Stars yetu..lakini siendi kabisa...ikishinda nitashangilia ikifungwa nitasikitika kama Mtanzania....Upo wakati mtu mmoja anaongoza mkoa wa Dar es Salaam Simba na Yanga wanacheza yeye anavaa T shirt ya timu mojawapo...dah ...
Mkuu eti kamati hiyo ina watu kama huyu? Mbona tunaitukana nchi hii?
binamubananga___BvUbC_LBG-h___.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuiombee tu timu yetu ya Taifa ishinde na kufuzu hiyo afcon. Ingawa natambua huo ushindi iwapo utapatikana, tutaambiwa ni kwa sababu ya mafanikio ya mtu fulani pasipo kuwapa heshima wanaostahili (wachezaji na benchi la ufundi). Kila kitu tunatanguliza siasa tu na siyo uzalendo.
Huyo Bashite na timu yake washindwe na walegee hadi mwili mzima. Wapigwe matobo hadi walie damu za wale wanaopotea bila uchunguzi. Wapigwe hadi waseme walikuwa wanafanya Nini Dom wakati Lisu ananyeshewa mvua ya risasi!!!? Ndiyo matamanio yangu, mengine ataamua Muumba.
 
Huyo Karia mwenyewe tayari kesha igeuza tff kuwa kijiwe cha siasa baada ya kutoa maneno ya kumdhalilisha mh lissu
Heshima kwenu wanajamvi.
Natoa tahadhari kwa TFF na watanzania kwa ujumla kuwa makini na propaganda za kisiasa zinazofanywa na mkuu wa mkoa wa Dsm Paul Makonda kila anapozungumzia maandalizi ya mchezo wa Taifa Stars dhididi ya Uganda.

Makonda anatumia nafasi aliyopewa ya mwenyekiti wa kamati ya maandalizi kumsifia rais na serikali badals ya kuwahamasisha watanzania kuisapoti timu ya taifa.

Natoa angalizo kwa TFF kuacha kuwateua wanasiasa kwenye masuala ya mpira kwani kunawagawa watanzania badala ya kuwaunganisha.

In God we trust
 
Back
Top Bottom