Angalizo muhimu sana kwa CCM, mwenye sikio atege

Katiba mpya ni kilio na kipaumbele cha wanasiasa walafi na wenye uchu wa madaraka hasa chadema, wananchi kilio Chao na kipaumbele ni umeme wa uhakika, maji, na huduma nzuri za afya na eli
[emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]
 
Katiba mpya ni kilio na kipaumbele cha wanasiasa walafi na wenye uchu wa madaraka hasa chadema, wananchi kilio Chao na kipaumbele ni umeme wa uhakika, maji, na huduma nzuri za afya na eli
Nyie watu duh! Miaka 60 plus, hivyo ulivyotaja vimefanikiwakwa kiasi gani?.msiwe wapumbavu tumieni ufahamu wenu vizuri...Tunaishi nchi moja tunaona, tuna AKILI😳
 
Katiba mpya siyo kipaombele cha watanzania. Ndio maana hakuna bibi yeyote wa kijijini anayeweza kukwambia kuwa kero yako ni katiba mpya.
Akili zako zinatosha kuvukia barabara tu! unajua zaidi ya miaka 60 ya uhuru kuna watu hawana maji safi na salama, hakuna madaraja wala barabara, mfumo mbovu wa elimu,hakuna uwajibakaji wa viongozi haya na mengine mengi ni matunda ya katiba mbovu. Kazi kuimbiana mapambio ya sifa
 
Mwalimu Nyerere alishaonyesha mfano,Maoni yalivyotolewa wakati ule "Eti wengi wanapenda chama kimoja",Lakini yeye akasema Dunia imebadilika ,tusikidanganye moni yakupendelea mfumo uliopo yameratibiwa na kuwahadaa wananchi.

Ukweli,ni kuwa Katiba mpya ni hitaji muhimu kwa sasa.Siku akija Rais mvuta bangi,mwenye kiburi ataivuruga nchi.
 
Maamuzi mengi mnayoyafanya (CCM) ni kwa maslahi mapana ya chama na walioshika madaraka.
Kwa maslahi ya Katiba ya CCM inayoongoza Nchi kwa upande mwingine ni Katiba ya CCM ya Mwaka 1977

Acha niishie hapo.
 
Nyie watu duh! Miaka 60 plus, hivyo ulivyotaja vimefanikiwakwa kiasi gani?.msiwe wapumbavu tumieni ufahamu wenu vizuri...Tunaishi nchi moja tunaona, tuna AKILI😳
Zoezi la kuweka maji, umeme na huduma zote za muhimu ni endelevu, miaka 60 nyuma kuna baadhi ya wilaya zilikuwa ni mapori, pia miaka 30 ijayo kuna mapori yatajaa watu, so itakua ni ajabu kwa mtu huyo mwaka 2060 kushangaa kwamba kwanini ktk eneo hili hamkuweka maji mwaka 2025!
 
Haya fanyeni jambo la akili sasa. Mchakato wa kupata Katiba Mpya uanze mapema kabla ya uchaguzi ujao 2025 ili kuepusha yanayoepukika. Angalizo kwenu ni kwamba Katiba hii itakapokuja kutumia dhidi yenu hakika hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe kwenye ghorofa la barafu mlilolijenga tangu uhuru hadi sasa.[emoji419][emoji375]
 
Ilianguka dola ya umedi na uajem ya nebucadneza, ikaanguka ya mgiriki yake alexanda mkuu , ikaja ya mrumi ya julias kaiza nayo chali . Akina tsar wa romanov wa russia nayo chali. Ukaja utawala wa third reich uliotishia ulaya mpaka marekani nayo haikunusurika. Sembuse chama tawala cha puerto rico few people 's socialist party
 
Kila asikiae maonyo na kushupaza shingo........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…