ANGALIZO: Namungo FC msibweteke na Majaliwa, bali jifunzeni kilichotokea kwa Singida United iliyokuwa chini ya Mwigulu Nchemba

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Nianze kwa Kuwapongezeni sana kwa Kupanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara na hata kwa aina ya Uwekezaji wenu mzuri ambao unaratibiwa Kiustadi kabisa na Mheshimiwa Waziri Mkuu wa sasa Kassim Majaliwa Kassim. Hata hivyo kwa mbali mno na taratibu sana naanza Kuiona Sumu ambayo imepelekea Klabu ya Singida United ambayo ilikuja kwa Kasi katika Ligi Kuu ya Tanzania bara Kuanguka ( hasa Kihamasa ) itaweza pia kuhamia katika Klabu ya Namungo FC ya Mkoani Lindi.

Si siri hakuna ambaye hajui kuwa Klabu ya Singida United iliundwa na Kukumbatiwa hasa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wakati huo Mwigulu Nchemba ili aweze tu Kuitumia Kisiasa na kweli Klabu hiyo iliweza Kumtangaza vyema kabisa huku Yeye ( Mwigulu ) akiwa anatumia baadhi ya Rasilimali za Wizara aliyokuwa akiiongoza katika Kuineemesha Singida United ila pale alipotumbuliwa tu Maisha ndani ya Klabu hiyo yalianza kuwa mabaya ila Yeye Mwigulu alishakivuna kile alichokuwa akikitaka.

Hata nyie Namungo FC ambayo hakuna Mtu asiyejua kuwa hiyo Timu ni ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na anaihudumia kwa kila namna ili mradi tu aweze Kuitumia Kuweza kumurudisha tena mwakani kama Mbunge na aendelee kuwa Waziri Mkuu mkakati ambao tayari naona umeshakamilika kwani hivi sasa Mkoa mzima wa Lindi ni Namungo na Namungo nzima ni Kassim Majaliwa.

Kwanini nimesema nawapeni ANGALIZO Namungo FC jibu ni rahisi sana kwamba kwakuwa sasa mmeshapanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara hebu anzeni Kujijenga nyie kama nyie pasi na Kumtegemea Waziri Mkuu Majaliwa kwani wala nisiwaficheni endapo Kassim Majaliwa atapita ( atashinda ) Ubunge wake mwakani basi nina uhakika kuwa atawaacheni kwani nia yake itakuwa imekamilika hivyo Yeye kama Mbunge atamalizia muda wake huo pamoja na ule wa Uwaziri Mkuu kisha Rais JPM akimaliza muda wake hapo 2025 na Yeye ( Majaliwa ) nae atamaliza nae na Kustaafu huku akianza sasa Kula Mafao yake kama Waziri Mkuu Mstaafu.

Nyie bwetekeni tu huku mkijiaminisha kuwa Kassim Majaliwa ( Waziri Mkuu ) mtakuwa nae muda wote kisha baadae mje mlie kama Singida United ambayo nayo ilikuwa imejaa Kiburi cha kuwa chini ya Mwigulu Nchemba ( aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ) ambapo baada ya Kutumbuliwa tu na Mheshimiwa Rais JPM maisha ndani ya Klabu hiyo yamekuwa ni Magumu kiasi kwamba hata Lishe ya Wachezaji achilia mbali Mishahara yao na Posho zao ni Shida huku Mtu waliyekuwa wakimtegemea kwa kila Kitu Mwigulu Nchemba Yeye sasa akiwa anawakwepa na anaonekana akikata tu Viuno vyake na Skafu yake katika Matamasha ya Klabu yake pendwa ya Yanga.

Namalizia kwa Kuwaasa Namungo FC kuwa lichukulieni hili Bandiko langu seriously kabisa na tengenezeni Timu yenu ya Marketing ili iweze Kutafuta Wadhamini wa Kutosha mapema kiasi kwamba hata kama Waziri Mkuu Kassim Majaliwa nae atakuja Kuwatoseni ( Kuwaacha Solemba ) kama vile Mwigulu Nchemba alivyowaacha Singida United basi hamtoweza Kuterereka Kiuchumi na badala yake mtaendelea Kusimama Imara vinginevyo msipokuwa makini na hawa Wanasiasa wa Kitanzania mtakuja Kulia baadae na mtanikumbuka Mimi cleverbright kuwa niliwashtueni hivi mapema.

Kila la Kheri Namungo FC.
 
Singida United Mwigulu alikuwa mwenyekiti wa club ila aliyeko nyuma ya ufadhili wa timu alikuwa Mo Dewji,baadaye walishindwana maana mchezaji akinunuliwa Mwigulu anaweza kumtoa hata bure aende Yanga,alikuwa final say,Mo akaona isiwe taabu akakata ufadhili wake ndo timu ikafifia
 
tofauti ya waziri mkuu na mwigulu majaliwa ni mdau wa mpira muda mrefu na ana cheti cha ukocha wa mchezo huowakati mwigulu alianza kushabikia mpira ukubwani.
Singida united ni timu ya muda mrefu lakini mwigulu aliihari pale alipojiingiza kwa malengo tofauti ikiwemo kutoa wachezaji waliosajiliwa kwenda timu ya yanga ndio maana wadau wengine wa michezo wameitosa kuisaidia kwani inaonekana kama ni katawi ka yanga
 
sasa jiandaeni kuna CHATO FC,inakuja na lazima ipande ligi kuu,ndani ya mwaka mmoja ininatoka daraja la tatu hadi ligi kuu!!!!!!uwanja unakamilika timu tayari imeshapatikana
 
Nianze kwa Kuwapongezeni sana kwa Kupanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara na hata kwa aina ya Uwekezaji wenu mzuri ambao unaratibiwa Kiustadi kabisa na Mheshimiwa Waziri Mkuu wa sasa Kassim Majaliwa Kassim. Hata hivyo kwa mbali mno na taratibu sana naanza Kuiona Sumu ambayo imepelekea Klabu ya Singida United ambayo ilikuja kwa Kasi katika Ligi Kuu ya Tanzania bara Kuanguka ( hasa Kihamasa ) itaweza pia kuhamia katika Klabu ya Namungo FC ya Mkoani Lindi.

Si siri hakuna ambaye hajui kuwa Klabu ya Singida United iliundwa na Kukumbatiwa hasa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wakati huo Mwigulu Nchemba ili aweze tu Kuitumia Kisiasa na kweli Klabu hiyo iliweza Kumtangaza vyema kabisa huku Yeye ( Mwigulu ) akiwa anatumia baadhi ya Rasilimali za Wizara aliyokuwa akiiongoza katika Kuineemesha Singida United ila pale alipotumbuliwa tu Maisha ndani ya Klabu hiyo yalianza kuwa mabaya ila Yeye Mwigulu alishakivuna kile alichokuwa akikitaka.

Hata nyie Namungo FC ambayo hakuna Mtu asiyejua kuwa hiyo Timu ni ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na anaihudumia kwa kila namna ili mradi tu aweze Kuitumia Kuweza kumurudisha tena mwakani kama Mbunge na aendelee kuwa Waziri Mkuu mkakati ambao tayari naona umeshakamilika kwani hivi sasa Mkoa mzima wa Lindi ni Namungo na Namungo nzima ni Kassim Majaliwa.

Kwanini nimesema nawapeni ANGALIZO Namungo FC jibu ni rahisi sana kwamba kwakuwa sasa mmeshapanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara hebu anzeni Kujijenga nyie kama nyie pasi na Kumtegemea Waziri Mkuu Majaliwa kwani wala nisiwaficheni endapo Kassim Majaliwa atapita ( atashinda ) Ubunge wake mwakani basi nina uhakika kuwa atawaacheni kwani nia yake itakuwa imekamilika hivyo Yeye kama Mbunge atamalizia muda wake huo pamoja na ule wa Uwaziri Mkuu kisha Rais JPM akimaliza muda wake hapo 2025 na Yeye ( Majaliwa ) nae atamaliza nae na Kustaafu huku akianza sasa Kula Mafao yake kama Waziri Mkuu Mstaafu.

Nyie bwetekeni tu huku mkijiaminisha kuwa Kassim Majaliwa ( Waziri Mkuu ) mtakuwa nae muda wote kisha baadae mje mlie kama Singida United ambayo nayo ilikuwa imejaa Kiburi cha kuwa chini ya Mwigulu Nchemba ( aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ) ambapo baada ya Kutumbuliwa tu na Mheshimiwa Rais JPM maisha ndani ya Klabu hiyo yamekuwa ni Magumu kiasi kwamba hata Lishe ya Wachezaji achilia mbali Mishahara yao na Posho zao ni Shida huku Mtu waliyekuwa wakimtegemea kwa kila Kitu Mwigulu Nchemba Yeye sasa akiwa anawakwepa na anaonekana akikata tu Viuno vyake na Skafu yake katika Matamasha ya Klabu yake pendwa ya Yanga.

Namalizia kwa Kuwaasa Namungo FC kuwa lichukulieni hili Bandiko langu seriously kabisa na tengenezeni Timu yenu ya Marketing ili iweze Kutafuta Wadhamini wa Kutosha mapema kiasi kwamba hata kama Waziri Mkuu Kassim Majaliwa nae atakuja Kuwatoseni ( Kuwaacha Solemba ) kama vile Mwigulu Nchemba alivyowaacha Singida United basi hamtoweza Kuterereka Kiuchumi na badala yake mtaendelea Kusimama Imara vinginevyo msipokuwa makini na hawa Wanasiasa wa Kitanzania mtakuja Kulia baadae na mtanikumbuka Mimi cleverbright kuwa niliwashtueni hivi mapema.

Kila la Kheri Namungo FC.
Wametoa kiungo bora Mudathir
 
Singida United Mwigulu alikuwa mwenyekiti wa club ila aliyeko nyuma ya ufadhili wa timu alikuwa Mo Dewji,baadaye walishindwana maana mchezaji akinunuliwa Mwigulu anaweza kumtoa hata bure aende Yanga,alikuwa final say,Mo akaona isiwe taabu akakata ufadhili wake ndo timu ikafifia
Mo aliishaiuza singida muda mrefu ikachukuliwa na tajiri mwengine wa singida, mwigulu akaidandia kwa mbele.
 
Back
Top Bottom