idoyo
JF-Expert Member
- Jan 13, 2013
- 3,051
- 1,416
Hivi karibuni TBS wamesambaza vijana wao kwenye vituo vya forodha ili kuhakikisha bidhaa zinazoingia zimekaguliwa kwa ubora. Vituo hivyo ni pamoja na 'yards' za magari maarufu kama bandari kavu. Ili gari liruhusiwe kuingia ni lazima liwe limekaguliwa na mawakala wa TBS kwenye 'exporting country' kama Japan n.k. na kukabidhiwa cheti cha ukaguzi, pamoja na 'sticker' ambayo hubandikwa kwenye gari. Kuna baadhi ya watu wanakwepa gharama za ukaguzi na hivyo gari huja bila cheti. Hapa ndipo vijana wanapopata ulaji! Kama gari halina cheti cha ukaguzi, mtuhumiwa anatakiwa kulipa 'offense' (hapa inategemea na cif, cc ya gari). Ili Officer asikuandikie inabidi umpoze, wanachukua kati ya TZS 500,000-1,000,000 kwa gari moja. TBS mnakosa mapato hapa! Fumbueni macho mujenge nchi!
Last edited by a moderator: