Angalizo: TBS, vijana wenu 'wanakula' rushwa

idoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2013
Posts
3,051
Reaction score
1,416
Hivi karibuni TBS wamesambaza vijana wao kwenye vituo vya forodha ili kuhakikisha bidhaa zinazoingia zimekaguliwa kwa ubora. Vituo hivyo ni pamoja na 'yards' za magari maarufu kama bandari kavu. Ili gari liruhusiwe kuingia ni lazima liwe limekaguliwa na mawakala wa TBS kwenye 'exporting country' kama Japan n.k. na kukabidhiwa cheti cha ukaguzi, pamoja na 'sticker' ambayo hubandikwa kwenye gari. Kuna baadhi ya watu wanakwepa gharama za ukaguzi na hivyo gari huja bila cheti. Hapa ndipo vijana wanapopata ulaji! Kama gari halina cheti cha ukaguzi, mtuhumiwa anatakiwa kulipa 'offense' (hapa inategemea na cif, cc ya gari). Ili Officer asikuandikie inabidi umpoze, wanachukua kati ya TZS 500,000-1,000,000 kwa gari moja. TBS mnakosa mapato hapa! Fumbueni macho mujenge nchi!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu we umeanzia kwa Vidagaa.
Hawa jamaa rushwa inaanzia Ndani Ofisini kwao

We ukipeleka Sample yako Pale huwezi amini unakaa hadi unaghairi kuifanya hiyo Biashara,ukitoka hapo unakutana na wazushi Pacha wenzao TFDA ndio balaa.
Kuna watu kibao nawajua walikata tamaa na kuacha kabisaa wazo lao la biashara
 
pole ndugu! nimekosa imani kabisa na hawa watu.
 
kula inauwa hii nchi - mwishoni ni mkulima ndio analipa ulaji wote huu
 
TFDA ndio funga kazi wananuka rushwa kama mzoga wa maiti ya Ebola,wanazuia bidhaa yako kwa sababu ya maandishi,logo,printout au lugha wakati huohuo kuna bidhaa zimesambaa sokoni zikiwa na lugha za kichina,kitaliano,kireno.
Sometimes wanatumiwa na wazalishaji wakubwa ili kukandamiza wadogo.
 
Hahahahahaaaaa Tanzania Naskia hata ukitaka mhuri wa Mkuu waKaya unaupata
 
ivi kumbe tz tuna maengineer wa kukagua ubora wa magari? tunasubiri nn tusianze kutengeneza magari? manake najua hadi ukague ugali kama umeiva lazma ujue kuupika
 
tbs hawakagui hapa. wanaangalia tu cheti cha ukaguzi. wana mawakala wao kwenye nchi magari yanapotoka, na zinakuwa ni kampuni za huko-huko!
 
RUSHWA YAO MPAKA KWENYE USAILI

Hivi karibuni shirika la viwango tanzania(tbs) limefanya usaili wa waombaji nafasi za kazi
kama ilivyotanganzwa ,cha ajabu tuliofanya vema tumeachwa ktk shortlist, wamechaguliwa
watu kwa kujuana na wengine waliokwisha toa rushwa ya ngono kwa wakurugenzi
na baadhi ya wahojaji. Tunaomba vyombo husika vifuatilie ufaulu wa wasailiwa.

Mkweli.
 
Hivi karibuni TBS wamesambaza vijana wao kwenye vituo vya forodha ili kuhakikisha bidhaa zinazoingia zimekaguliwa kwa ubora. Vituo hivyo ni pamoja na 'yards' za magari maarufu kama bandari kavu. Ili gari liruhusiwe kuingia ni lazima liwe limekaguliwa na mawakala wa TBS kwenye 'exporting country' kama Japan n.k. na kukabidhiwa cheti cha ukaguzi, pamoja na 'sticker' ambayo hubandikwa kwenye gari. Kuna baadhi ya watu wanakwepa gharama za ukaguzi na hivyo gari huja bila cheti. Hapa ndipo vijana wanapopata ulaji! Kama gari halina cheti cha ukaguzi, mtuhumiwa anatakiwa kulipa 'offense' (hapa inategemea na cif, cc ya gari). Ili Officer asikuandikie inabidi umpoze, wanachukua kati ya TZS 500,000-1,000,000 kwa gari moja. TBS mnakosa mapato hapa! Fumbueni macho mujenge nchi!

Hao Vijana wa TBS wana Njaa kuliko mchwa ....wanaendekeza sanaa RUSHWA ..kila kitu ...wana Njaa kuliko WAGONJWA wa utapia mlo mkali
 
Last edited by a moderator:
Hao Vijana wa TBS wana Njaa kuliko mchwa ....wanaendekeza sanaa RUSHWA ..kila kitu ...wana Njaa kuliko WAGONJWA wa utapia mlo mkali

nja kali mno. washanunua magari kwa kipindi kifupi tu walichakaa humo!
 
Back
Top Bottom